Je, ile 'confidence' ya Kuongea Kiingereza 'fluently' bila kuandikiwa au kusoma akina Nyerere na Mkapa waliitoa wapi nami nikajifunze?

2006 UNESCO iliitangaza Uganda kama nchi yenye grammar bora katika nchi za Afrika zinazoongea Kiingereza. Binafsi nilidhani Botswana wanaongoza lakini nilishtuka kusikia ni Uganda.
Napenda sana MTU akijenga hoja aweke reference, hii reference hata mi naikumbuka miaka kadhaa iliyopita nilipata kupitia BBC
 
Hahahaha ukiachana na UDSM ,tofauti na UDSM chuo nilichosoma mie majuzi kinatumia kiingereza hizo phrase huwa zimeandikwa kwenye kijitabu maalumu anasoma vizuri tu "By power ,virtue and moral authority held in ,,,, "
 
The lady it speak very tough English. Eye am told she educated Canada for PhD. Eye arm also told she pay many money of school fees for daughter educate outside of Tanzania.
Hahahahahaha jamani hebu acheni kunimalizia jokes zangu
 
Ukitaka kuwa fluent kwenye lugha yoyote
SPEAK IT....
For a long time..
Na lazima pia uwe kwenye mazingira ya watu wanaotumia hiyo lugha.
Huwezi ukawa uko buza unajiongelesha peke yako au uongee na watu waliosoma shule za kata halafu ukategemea uijue kama watu walio british utakuwa unajidanganya.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Uganda sio ishu ya elimu kule wanatumia kuongea kiingereza hata mitaani.
Ingawa wako na lugha yao ya Luganda lakini wanaongea kiingereza pia mitaani kwa muda mwingi na wala haihusiani na elimu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 

sidhani unajua unachokisema wewe. Sikiliza matamshi ya kila neno analoongea, chaguzi ya maneno yake na ufasaha wa uwasilishaji halafu unasema kiingereza chake kilikuwa poor?
Nimemsikiliza nimeona anaongea standard english ambayo mtu yeyote msomi ambaye si kilaza anaweza kuiongea.
Sio ya kuisifia kwamba anajua sana.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mie pia nataman sana kua fluent kwenye kingereza. Bado napambana and I can see some improvements. Cha msingi wewe endelea kujifunza huku uki practise na kujichanganya na wanaoongea kingereza kdogo kdogo utajikuta upo vizuri.All the best
Ukishakijua halafu unataka ukakitumie wapi na kwa manufaa gani?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kifupi mimi naona ni utumwa tu kutumia miguvu mingi kujifunza lugha ya nchi za wazungu bila manufaa maalumu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kiingereza ni lugha ya asili ya uingereza.
Sasa je uingereza ni wapi?
Na kitu kingine kiswahili asili yake ni pwani ya afrika mashariki.
Kwa hiyo ukiuliza wenye kiswahili ni wandengereko jibu lake kama wandengereko ni watu wa pwani ni kweli kiswahili ni chao wala hujakosea.
Wengine ambao wako nje ya pwani tunaassume wanajifunza kiswahili ila hawawezi kuwafikia wale wenyewe wa pwani.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilidhani kwa neno hilo ungeacha kuandika kumbe wajifanya mjuaji!![emoji848]

Ulitaka nikuonyeshe kosa lako la kiswahili na nikakuonyesha lakini ukajifanya hamnazo kutokuliona, sasa angalia kosa lako uliloandika, nanukuu; "
Kudadeki JF sihami.
Naona umemuonjesha kidogo ladha ya kiingereza.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Walisoma Arts mpaka chuo kikuu na walikazania kiingereza na kukimudu. Angalia Tundu lissu anavyoongea kwa kujiamini, alichukua Arts na akaweka mkazo katika kiingereza ili kimsaidie katika fani yake. Ukiwa na nia ya dhati utakimudu kiingereza.
 
Kwa hali hiyo watu wote duniani hajaui kiingereza kwa vile hawana lafudhi ya England? Huwezi kumpata mtu ambaye hakukulia England akajua kuongea kwa lafudhi ya England. Hata Tanzania hapa, watu waliokulia mikoa mbalimbali wana lafudhi zao anbazo hazifanani.Kanuni kuu ya lugha ni isimu; nimeshawasikia wandegereko wanaosema "nyimbo ile nimeipenda sana" ambayo ni makosa katika lugha ya kiswahili.
 
Kiingereza cha Nyerere kilikuwa poor, Kiingereza kilikuwa na Augustino Mahiga.
Poor based on what, alikuwa anaongea Kiingereza fasaha with confidence.
Umenifanya nimeingia You Tube kumsikiliza huyo Mahiga, Kiingereza chake ni cha kawaida sana na ana accent vile vile. Acha ushabiki wa kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…