Mkuu hakuna ugumu na gharama inategemea na eneo.
[emoji117]Mimi kodi nimelipa 150k ni kodi ya miezi mitatu mbele ya ile fremu kuna eneo kubwa tu(hili eneo ndo lililokula pesa ya ukarabati vinginevyo ingekua chini ya hapo).
[emoji117]Meza plastic kampuni ya jambo meza 2 kila moja nilinunua elfu 37.
[emoji117]Viti vya plastic 8 kila kimoja nilinunua elfu 14
[emoji117]Sufuria ,sahani,vijiko,vikombe,bakuli nk nilitumia laki 1(hapa baadhi ya vitu nilichukua nyumbani)
[emoji117]Plate ya jiko la gesi nilinunua kwa mtu kwa elfu 30 na mtungi nilichukua wa nyumbani.
[emoji117]Jiko kubwa la chuma(yale yanatengenezwa kwa rim) rim nilichukua kwa bro fundi nilimpa elfu 20(fundi ni baba wa rafiki yangu)
[emoji117]Jiko la mkaa madogo mawili(nilichukua home)
[emoji117]Feni ndogo 1 ya elfu 45
[emoji117]Ukarabati(rangi,tofali,cement,mchanga na ufundi) laki 320
[emoji117]Mahitaji ya misosi(mafuta,mkaa,mchele nk) laki 130+
Nb:Siku 6 za Mwanzo nilifanya biashara ya kanisa nilipata hasara kubwa[emoji16][emoji16][emoji16]..nikifika home nitakupigia picha kitabu cha mahesabu.
Vitu nilivyoongeza Jana Meza 1 na viti vinne.lakini Pia mkuu kama ningetaka makubwa zaidi ingekua hela zaidi ya hiyo ila mimi nilitenga laki 5 nikajikuta nimetumia milioni kasoro elfu 16 hivyo hela inaweza kuongeza kutokana na upatikanaji wa vitu na mazingiro uliyopo.
Mkuu kumbe kuanzisha mgahawa sio kazi ngumu
Maana mimi nilifikiria gharama za kodi ya pango, vyombo, jiko la mkaa + gesi, viti, meza, na mpishi lazima milioni mbili ikutoke,
Wewe uliwezaje kufanya yote hayo plus ukarabati kwa gharama ya 980k
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app