Je, ilikuwa ni dhambi Mfalme Suleiman kuoa Wanawake wengi wakiwamo Masuria 300?

Je, ilikuwa ni dhambi Mfalme Suleiman kuoa Wanawake wengi wakiwamo Masuria 300?

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Kwa mujibu wa Biblia Mfalme Suleiman alipenda sana Wanawake

1 Wafalme 1-25 "Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo"

Naomba mtujuze je aliyofanya Suleiman ni dhambi pia according to vitabu vingine ukiachana na Biblia?

Namaanisha Biblia inahesabu tabia ya Suleiman haikuwa sahihi mbele za Mungu kwa Kitendo cha kuoaoa Wanawake wengi, Sasa je Vitabu vingine vinatoa msi amo gani? Je vinamhesabia dhambi Mfalme Suleiman au vinaona aliyofanya yako sahihi?

Karibuni tupate elimu
 
1 Timotheo 3:2
Mathayo 5:32
Mathayo 19:9
Marko 10:11-12

NB: Kuwa makini sana na maneno yote aliyoyazungumza Yesu alipokuja dunianiani kwa sababu alikuwa anaweka sawa vitu vyote ambavyo watu hawakuelewa kutoka kwenye neno la Mungu. Mathayo 19:8
"
Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi."
 
Si dhambi, alifuata mila na desturi za mababu.
Rejea Ibrahim Yakobo Etc etc. Kuwa na mwanamke mmoja ni matumizi mabaya ya “nguvu pendwa” [emoji4][emoji4]
Safi sana Mfalme Suleiman! [emoji23]
 
Kwenye Ulimwengu wa Roho, kila mwanamke ulielala nae ni mkeo.

Wengine aliwapitia tu ila ilihesabiwa.
 
Mfalme Suleiman anaelezwa kwa sifa tatu kubwa ambazo wafalme wengine wote hawakuwa nazo:
1. Mungu alimjalia hekima na maarifa yaliyomsaidia kuwa kiongozi mwenye sifa nzuri za pekee.
2. Mungu alimjalia utajiri na fahari ya pekee duniani.
3. Ndiye mfalme na binadamu pekee kuwa na wake wengi duniani.
Sifa hizi zilikuwa na matokeo mazuri kwa utawala wake, sifa ya kwanza ilimfanya kuwa mwamuzi na kiongozi mzuri kwa watu wake, sifa ya pili utajiri na fahari yake ilimsaidia kujenga nyumba ya BWANA kwa vigezo vyote vilivyotakiwa, lkn pia kujitosheleza kwa vyote na kukidhi mahitaji ya watu wake na hivyo kuthaminiwa na kuheshimiwa hata na viongozi wa mataifa mengine..na sifa ya tatu, wakati wa utawala wake hakupigana vita hata moja, hii ni kwa sabab maana ya kuwa na wake na masuria wengi ni kwa sabb idadi hyo iliwakilisha namba ya mataifa na koo zote za wakati huo, ili kama kuna taifa au koo ilitaka kupigana na Suleiman, alikuwa akipewa taarifa anauliza ni watu kutoka wapi wamekuja kutuvamia? Walipomwambia ni wa taifa au koo fulani basi alielekeza mke au suria kutoka taifa hilo au koo hiyo aende kuongea na ndugu zake..na alifanikiwa sabb wavamizi walipoletewa mke wa mfalme kuongea nao kwa lugha yao walikuwa wanaahirisha vita na Suleiman kwa kuogopa laana ya kuua watu kutoka kwao..mambo haya yalikuwa mema hata machoni mwa Mungu.
 
Katika story ambazo napata shida kuamini, hii mojawapo.
 
Kwa mujibu wa Biblia Mfalme Suleiman alipenda sana Wanawake

1 Wafalme 1-25 "Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo"

Naomba mtujuze je aliyofanya Suleiman ni dhambi pia according to vitabu vingine ukiachana na Biblia?

Namaanisha Biblia inahesabu tabia ya Suleiman haikuwa sahihi mbele za Mungu kwa Kitendo cha kuoaoa Wanawake wengi, Sasa je Vitabu vingine vinatoa msi amo gani? Je vinamhesabia dhambi Mfalme Suleiman au vinaona aliyofanya yako sahihi?

Karibuni tupate elimu
kuoa siyo dini ni suala la mila
hata sasa ukitaka kuoa huanzii kanisani ,unaanza na mila-unalipa mahari kwa mujibu wa mila, unaposa kwa mujibu wa mila yenu na na ya mdada ,kisha ndo mambo ya kanisani yanafuata
 
Back
Top Bottom