Mfalme Suleiman anaelezwa kwa sifa tatu kubwa ambazo wafalme wengine wote hawakuwa nazo:
1. Mungu alimjalia hekima na maarifa yaliyomsaidia kuwa kiongozi mwenye sifa nzuri za pekee.
2. Mungu alimjalia utajiri na fahari ya pekee duniani.
3. Ndiye mfalme na binadamu pekee kuwa na wake wengi duniani.
Sifa hizi zilikuwa na matokeo mazuri kwa utawala wake, sifa ya kwanza ilimfanya kuwa mwamuzi na kiongozi mzuri kwa watu wake, sifa ya pili utajiri na fahari yake ilimsaidia kujenga nyumba ya BWANA kwa vigezo vyote vilivyotakiwa, lkn pia kujitosheleza kwa vyote na kukidhi mahitaji ya watu wake na hivyo kuthaminiwa na kuheshimiwa hata na viongozi wa mataifa mengine..na sifa ya tatu, wakati wa utawala wake hakupigana vita hata moja, hii ni kwa sabab maana ya kuwa na wake na masuria wengi ni kwa sabb idadi hyo iliwakilisha namba ya mataifa na koo zote za wakati huo, ili kama kuna taifa au koo ilitaka kupigana na Suleiman, alikuwa akipewa taarifa anauliza ni watu kutoka wapi wamekuja kutuvamia? Walipomwambia ni wa taifa au koo fulani basi alielekeza mke au suria kutoka taifa hilo au koo hiyo aende kuongea na ndugu zake..na alifanikiwa sabb wavamizi walipoletewa mke wa mfalme kuongea nao kwa lugha yao walikuwa wanaahirisha vita na Suleiman kwa kuogopa laana ya kuua watu kutoka kwao..mambo haya yalikuwa mema hata machoni mwa Mungu.