Je, inachukua muda gani kuona dalili za maambukizi ya HIV?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
2,591
Reaction score
1,616
Kwenu wataalam wa mambo ya afya!
Hivi inachukua kipindi gani toka siku ya kupata maambukizi ya VVU mpaka kuanza kuonyesha baadhi ya dalili kama kukohoa sana, kupungua uzito mpaka kuwa na magonjwa mengi nyemelezi?
Tufahamishane wadau! MziziMkavu na wengineo njooni muokoe jahazi!
 
Last edited by a moderator:
Kama masikini mwezi hata inzi anatosha kukumaliza kama Tajiri ni muda mrefu upo Kundi gani
 

FAHAMU MAMBO MUHIMU KUHUSU VVU/UKIMWI

Ili mtu ajulikane kuwa ana VVU/Ukimwi atapitia hatua nne za lazima kama nitakavyoziainisha hapa.
Hatua ya kwanza hujulikana kitaalamu kama Primary HIV Infection ambapo mgonjwa hudumu nayo kwa wiki nne baada ya maambukizi. Watu walio katika maambukizi katika hatua hii ni asilimia 20 tu ya wenye maambukizi ya VVU ambao huona dalili za ugonjwa huu.

Mara nyingi walio katika hatua hii madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya VVU kutokana na dalili na viashiria vyake kufanana sana na dalili za magonjwa mengine.

Kutokana na hilo madaktari huwa makini sana kwani aliyeambukizwa akiwa katika hatua hii huweza kuonesha dalili kama vile kuvimba tezi yaani Swollen lymph glands, anaweza kuwa na homa kali, kuumwa koo, yaani Sore throat, kutokwa na vidonda mdomoni au pembeni ya mdomo, kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini, kutokwa na vipele mwilini na pia kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo.

Mgonjwa mwenye dalili hizo kitaalamu hutajwa kuwa amepata ‘Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection.'

Hatua ya pili ya VVU/ Ukimwi kitaalamu huitwa Clinically Asymptomatic Stage na mgonjwa huweza kudumu nayo kwa miaka 10 na wengi wao hawaonyeshi dalili yoyote isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba, yaani Swollen lymph nodes. Lakini ukweli ni kwamba kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana lakini mgonjwa anaweza kumwambukiza mtu mwingine.

Hata hivyo, licha ya mgonjwa kutoonesha dalili za maradhi lakini akienda kwenye vipimo vya VVU vitaonesha kwamba ana maambukizi ya ugonjwa huo katika damu yake.
Wagonjwa wa kundi hili hutakiwa kupima kwa kipimo cha wingi wa virusi vya ukimwi, yaani Viral load test


kwani VVU katika mwili wanapozaliana hujificha kwenye tezi yaani lymph nodes. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.
Akitoka katika hatua hiyo huja hatua inayoitwa kitaalamu Symptomatic HIV infection, hapa kinga ya mwili


huzidi kudhoofika kutokana na kuongezeka kwa VVU kwani tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi kuwa mwilini muda mrefu na virusi hao hubadilikabadilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua seli zinazokinga mwili (T helper cell) kutokana na maambukizi hivyo kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya.

Maambukizo ya VVU na ugonjwa wa UKIMWI

VVU huathiri sehemu nyingi za mwili wa mtu. Vinaweza kufanya hivyo kwa
njia mbili. Njia ya kwanza ni kwa kushambulia moja kwa moja viungo mbali

mbali, njia nyingine ni kwa kudhoofisha mfumo wa kinga na kuruhusu viini
au vimelea vinavyosababisha magonjwa mengine kuingia mwilini. Katika sura


hii, tutaelezea uharibifu wa aina ya kwanza ambao VVU husababisha, katika
nyongeza tutajadili aina ya pili ya uharibifu unaofanywa na VVU.


VVU hushambulia seli za ubongo wa mtu. Hii inaathiri uwezo wa mtu
kufikiri (kwa sababu ya uharibifu uliopo kwenye ubongo). Husababisha maumivu
na ganzi katika mikono na miguu (kwa sababu ya uharibifu wa mishipa


ya fahamu (neva). Husababisha kuharisha (uharibifu ulio tumboni) husababisha
upungufu wa damu na kuvuja kwa damu (husababishwa na uharibifu


unaotokea kwenye damu). Ingawaje VVU, vinasababisha mtu augue, tunafahamu
sio kila mtu, mwenye VVU ni mgonjwa. Ndiyo sababu kuna hatua, za


mtu alieambukizwa anapitia, kuanzia mtu anapoambukizwa na VVU, kipindi
ambacho aliyeambukizwa haonyeshi dalili zozote, hufikia hatua ya alieambukizwa
huanza kuonyesha dalili za mwanzo, na hatimaye UKIMWI.



N i n i - d a l i l i - z a - a l i y e - a m b u k i z w a - n a - V V U ?

Hatua nne za maambukizo ya VVU

1. Wiki chache baada ya kuambukizwa, watu huwa na dalili kama homa ya mafua.

2. Kipindi cha utulivu, wakati kuna dalili chache za UKIMWI.

3. Dalili za awali za UKIMWI.

4. UKIMWI, mwathirika huwa mahututi sana.
Huchukua muda toka kipindi kimoja hadi kingine.



Wiki za mwanzo baada ya maambukizo

Baada ya kuambukizwa VVU, kwa kawaida watu hawawezi kutambua
kwamba wameshaambukizwa VVU; hawawezi kujua kwamba wana VVU
mpaka baadae wanapokwenda kupima au wanapokuwa wagonjwa. Hata


hivyo watu wachache, huanza kuona dalili kuanzia wiki 1-4 baada ya maambukizo
ya virusi. Dalili zinazofanana
na mafua, maumivu ya
koo, homa, maumivu ya kichwa,


maumivu ya tumbo, kuharisha
na kujisikia kuchoka. Baada ya
wiki, vipele vinaweza kutokea


kwenye kifua, uso na shingo. Watu
wanaweza wakatokwa na jasho
usiku, maumivu ya misuli na


viungo, uvimbe wa tezi, kichefu
chefu na kutapika. Dalili hizi
kwa kawaida hudumu kwa muda
mfupi, sio zaidi ya wiki mbili.


Ni nadra kwa hatua ya kwanza
baada ya maambukizo ya VVU
kuwa mbaya sana na kuharibu
mfumo wa neva wa mtu. Mtu


aliyeambukizwa anaweza akawa
na uvimbe kwenye ubongo na
ngozi inayoufunika. Hii inaweza


kusababisha maumivu ya kichwa,
kugangamaa kwa shingo, homa,
kuchanganyikiwa, matatizo ya
mfumo wa neva na kupoteza


fahamu. Mtu anaweza kuwa na
matatizo ya neva kwenye mikono
na miguu na matatizo ya neva za


usoni. Hii inaweza kusababisha
maumivu ya ngozi na shida ya
kutembea, tezi wakati mwingine
huvimba na hubakia zimevimba
kwa miezi au miaka.


Kwa vile dalili hizi huonekana pia kwenye maradhi mengine mbali na
VVU, hatuwezi kusema kuwa kila mwenye dalili zinazofanana na hizi nchini
kwamba ana VVU. Ili mtu afahamu ana maambukizo ya VVU anahitaji


Mitoki
Mitoki mara nyingi huitwa "tezi",
ni kiini cha mfumo wa kinga ya
mtuo. Huwa zina vimba na kuuma
zinapo kabiliana kuondoa viini vya


maradhi. Mfano, mitoki ya shingoni
huvimba mtu anapopata maambukizo
katika koo. VVU husababisha
kuvimba kwa tezi, wakati mwingine
mwili mzima, wakati mwingine kwa
muda wa miaka.



kupima damu. Hata hivyo, kipimo cha kuchunguza VVU, wiki chache baada
ya maambukizo hakiwezi kutoa matokeo ya uhakika. Sababu ni kwamba
kipimo, huangalia kama mtu ana askari dhidi ya VVU (antibodi). Kama ndio


mwanzo tu wa maambukizo ya VVU na mwili wako bado haujatengeneza
askari dhidi ya VVU, kipimo hakiwezi kuonyesha kama mtu ameambukizwa
au la. Watu wengi miili yao huanza kuonyesha kama ina askari dhidi ya


VVU wiki nne baada ya maambukizo. Mtu yo yote anayedhani kwamba
inawezekana ameshaambukizwa na VVU anaweza kupima kwanza na kurudia
baadaye (soma zaidi juu ya kipimo cha VVU sura ya 7 na 8).
Kipindi cha ukimya baada ya maambukizo ya VVU


Siku chache baada ya dalili za
mwanzo zinazoambatana na
maambukizo ya VVU hutoweka na


mgonjwa hujisikia nafuu. Kwa miaka
kadhaa baadaye hujisikia vizuri,
huonekana mwenye afya na kuendela


na maisha ya kila siku. Mfumo wa
kinga unauwezo wa kukabiliana na


virusi kipindi hicho chote na huitwa
kipindi cha ukimya. Ni kipindi
kuanzia maambukizo hadi dalili



za mwanzo za ugonjwa wa UKIMWI. Kwa watu wazima, kipindi hiki huwa
miaka 10 kwa wastani. Kwa sasa watu wengi wenye VVU wako katika kipindi
hiki (cha ukimya). Hawasikii dalili yeyote na wengi hawajui kama wameshaambukizwa
na virusi na wanaweza kuambukiza.



Ugonjwa wa UKIMWI unavyoanza

Baada ya kipindi cha maambukizo, watu wenye VVU huanza kuugua, VVU

hudhoofisha mifumo yao ya kinga, kiasi ambacho uwezo wao ambao kwa
kawaida mfumo wa kinga unaokabiliana na viini hutoweka na kuruhusu
magonjwa mengine, magonjwa hayo huitwa "magonjwa nyemelezi"- na baadhi


ya kansa, ni dalili ya moja kwa moja ya UKIMWI. Tutajadili tiba zake
katika nyongeza. Wakati mfumo wa kinga unadhoofika, watu wenye VVU



Kundi la lishe bora

Protini – Husaidia mwili kukua na kuponya. Vyakula vyenye protini vingi, , ni
samaki na aina nyingine ya vyakula toka baharini, Nyama, mfano, ya ngombe, ya
kondoo na mbuzi. Nyama za kuku, bata, bata mzinga, mayai, maziwa, jibini, jamii
ya kunde, mchele, mbaazi, mchicha mweusi, nafaka, jamii ya karanga, tofu na vitu
vitokanavyo na soya, njegere.


Wanga – ni vyakula vya kutia nguvu mwili. Wanga upo kweye nafaka, mchele,
ngano, mtama, ulezi, uwele, viazi na muhogo.


Vyakula vya kutia joto na nguvu mwilini - husaidia mwili kuweka akiba ya
chakula cha kuupa mwili nguvu. Kuna nguvu mara mbili zaidi kama ilivyo kwenye
protini na vyakula vya kuupa mwili nguvu. Hii ina maana, ulaji wa mafuta husababisha
ongezeko la uzito kwa watu. Ladha nzuri, shida au tatizo la mafuta husabibisha


ugonjwa wa moyo kwa watu na ongezeko la uzito. Kwa watu walio athirika na

VVU hili siyo tatizo lao kwa kawaida kwa sababu, wao wanajitahidi waongezeke
uzito. Vyakula vyenye mafuta ya mgando na ya maji maji ni– siagi, karanga ufuta,
soya, nazi, (embe mafuta) parachichi, krimu, maziwa, nyama nyekundu kama ya
ngombe, nguruwe na kondoo.


Vyakula vya kulinda mwili – ni muhimu sana, mwili huhitaji kiasi kidogo kwa
afya ya mtu, hupatikana kwenye vyakula vya aina nyingi tofauti, ndio maana
vyakula tofauti katika mlo ni muhimu kwa afya ya binadamu, hutoa aina tofauti
(mbali mbali) ya vitamini na madini.



VVU, kupungua uzito na utapiamlo
Watu wengi huishi katika jumuia ambazo zina upungufu wa chakula na tatizo


la utapia mlo. Watu hawahitaji chakula cha kutosha tu, bali pia wanahitaji
aina mbalimbali ya vyakula, mfano, anayetumia muhogo kama chakula na
habadilishi, atadhoofika. Kama mtu anaweza kuwa mgonjwa kwa kutokula


chakula cha kutosha na sahihi, ana ugonjwa wa utapiamlo. Utapiamlo
unaweza kusababisha magonjwa na kupungua uzito. Njia mojawapo ya kudumisha
afya mzuri ni kula chakula bora. Huu ni ukweli hasa kwa wenye VVU


na UKIMWI. Wana uwezekanao wa kuwa na utapiamlo kutokana na kuugua
mfulululizo, kuharisha kunakosababisha mwili usipate lishe iliyopo kwenye


chakula, kupoteza hamu ya kula na vidonda mdomoni husababisha kula kwa
shida. Kupungua uzito ni kawaida kwa wenye VVU, kiasi kwamba baadhi ya
sehemu ya Bara la Afrika ugonjwa wa UKIMWI huitwa "slim".



Kama mtu yeyote ana shida wakati wa kula

Walioathirika na VVU wanaweza kuwa
na kichefu chefu na kutapika. Chai


au dawa yaweza kusaidia. Mwenye
vidonda mdomoni vyakula baridi na
visivyo na viungo hufanya maumivu
kupungua wakati wa kula. Watu wenye


kumeza kwa shida, kusogeza kichwa
mbele, na kula vyakula laini, husaidia
kumeza kwa urahisi. Uangalifu uzingatiwe


wakati wa kunywa ili kuepuka
kupaliwa. Utumiaji mrija wakati wa
kunywa kunaweza kukasaidia wakati
mwingine. Shida ya kula au kunywa


huenda ikawa ni kwa sababu ya ugonjwa ambao waweza kutibika, mfano ukungu
mdomoni; katika hali hii waeleze watu wakamuone mhudumu wa afya.



Kula vyakula bora vya aina mbali mbali; husaidia wenye VVU kuwa na
nguvu na afya. Chakula bora ni mlo mmoja wenye mchanganyiko wa vyakula
vyenye lishe mbali mbali muhimu. Lishe muhimu ni protini, wanga, mafuta
yaliyoganda na ya maji, vitamini na madini.


Wanawake na watoto wanahitaji lishe bora. Kwa sababu wanawake
hupoteza lishe nyingi wakiwa kwenye hedhi, ujauzito na wakati wa kunyonyesha.


Watoto huhitaji chakula cha ziada kwa sababu wanakua haraka. Watoto
wenye VVU huhitaji chakula zaidi ili wawe na afya nzuri, VVU huongeza
mahitaji ya chakula mwilini mwao.
 
Asante Dr,kwa maelezo yakitaalam ninae anko wangu tumemfanyia test tumekuta positive tunatafuta style yakumwambia nayy nadhani yuko kwenye hicho kipindi cha ukimya mwanzo alikuwa anasumbuliwa sana na tumbo kisha kuharisha lkn sasa yuko sawa anaendelea na shughuli zake
 
Asante#mzizimkavu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ubarikiwe sana MziziMkavu kwa hii elimu unayoendelea kuitoa kwa jamii. Hii itasaidia kutujengea uwezo sisi wananchi wote kuhusu huu ugonjwa hatari wa Ukimwi. Be Blessed!
 
Last edited by a moderator:
Duuh, ina maana wakati mnampima yeye alikuwa hajitambui? Au ni mtoto kiasi kwamba mnaweza kuchukua damu yake bila ridhaa yake? Mi nadhani fanyeni mpango siku akiugua mumuungnishe na wataalam wa ushauri nasaha ndio wafanye kazi kuliko nyie ambao huenda hamna uzoefu wa kutoa taarifa mshituko kama hizo! Ni wazo tu lakini, uamuzi bado ni wenu wenyewe!
 

Dada yangu ni Dr,sasa yy anakawaida yakuwapima watt wake kila baada ya miezi mi3 sasa huyu anko anaishi nahao ndg zake ss kuna cku Dada aliamua kuwapima wt Ikaonekana wenzie wako vzr lkn yy ana maambukiz dada alikosa ujasiri wakumwambia Ikabidi aniambie mimi ikibidi nimuite niongee nae then akapime nikamwambia jambo hili ni gumu vunginevyo tumtegee akiumwa tuunganishe huko huko hopt apate majibu then tuanzie hapo lkn tukaona kwamba ataendelea kuusambaza pia ni hatari kwake sasa nimeshauri yy Dada ajaribu kukaa nae aongee nae km mam then amshawishi aende kupima yaani hadi sasa hatujajua kipi tufanye Tunafikiria namna atakavyopokea majibu
 

Dada yangu ni Dr,sasa yy anakawaida yakuwapima watt wake kila baada ya miezi mi3 sasa huyu anko anaishi nahao ndg zake ss kuna cku Dada aliamua kuwapima wt Ikaonekana wenzie wako vzr lkn yy ana maambukiz dada alikosa ujasiri wakumwambia Ikabidi aniambie mimi ikibidi nimuite niongee nae then akapime nikamwambia jambo hili ni gumu vunginevyo tumtegee akiumwa tuunganishe huko huko hopt apate majibu then tuanzie hapo lkn tukaona kwamba ataendelea kuusambaza pia ni hatari kwake sasa nimeshauri yy Dada ajaribu kukaa nae aongee nae km mam then amshawishi aende kupima yaani hadi sasa hatujajua kipi tufanye Tunafikiria namna atakavyopokea majibu
 
Aiseee...sasa hapo nimekuelewa dolevaby...
 
Last edited by a moderator:
Ndio mtihani tulionao manake mambo yakupima lazima mtu akubali mwenyewe na awe tayari kupokea majibu ukimlazimisha then akijidhuru ikigundulika manake serikali itachukua nafasi yake......
 
Duuh hizi dalili ni noma hivi inawezekana ukaenda kupima baada ya miezi 5 ya high risk behavior visionekane hivyo virusi??
 
Mzizi Mkavu, excellent stuff here collegue. Napenda unavojitolea katika swala la afya. Ningependa nikufaham one day.
 
jamani virus au blood enye virus inakuwa kwenye hewa for how long ndio iwe weak,because kuna mzee kumbe anakuaga muathirika humu gari lake limebiringika mtaaani tu sasa katika kumtoa ndani damu yake ikanirukia jichoni na kwenye boil mguuni yaani sielewi niko hosy halafu shida ni ile nurses wananchanganya mimi wengine wanataka nipewe dawa wengine wanasema nisipewe nipeeni ushauri nipo kwenye kuchanganyikiwaπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kunywa pep mapema. Usije ukajutia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…