Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Kwahiyo Mungu hakujua kama Adam atakula tunda?
 
Kwa sababu swali hilo linamaliza mjadala kama imani ni hakika ama la.

Jibu swali tafadhali, usilikwepe.
Hilo swali si kwamba linamaliza mjadala bali linataka kukwepa mjadala,post namba [HASHTAG]#487[/HASHTAG] nimejaribu kukuonesha hilo neno imani linatafsirika vp kwenye ule mfano wako kwa kutumia maana uliyoisema wewe.

Matokeo yake unakuja kuniuliza kama nakubali au nakataa kwamba imani ni kukubali jambo bila kuwa na hakika?
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha.

Kwa sababu hayupo.

Kama yupo, thibitisha.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha.

Kwa sababu hayupo.

Kama yupo, thibitisha.
Wewe hayo ndio unayoyaweza maana ni kazi rahisi.

Ukiambiwa suala la Mungu ni imani unadakia kusema hapa haujadili imani,kumbe hata hilo neno imani hujui lina maana gani.
 
Wewe hayo ndio unayoyaweza maana ni kazi rahisi.

Ukiambiwa suala la Mungu ni imani unadakia kusema hapa haujadili imani,kumbe hata hilo neno imani hujui lina maana gani.
Imani maana yake ni kitu kisicho na hakika, sasa wewe una hakika au huna hakika kwamba Mungu yupo?
 
Imani maana yake ni kitu kisicho na hakika, sasa wewe una hakika au huna hakika kwamba Mungu yupo?
Tangia nianze kujadiliana na wewe suala la uwepo wa Mungu basi nimekuw nikiona maana tofauti tofauti kutoka kwako kwa hilo neno imani,hata hapo umekuja na maboresho tena kwamba ni "kitu kisicho na hakika"na sio tena "kukubali jambo bila kuwa na hakika" au "si hakika".
 
Sasa hapo tofauti iko wapi?

Tofauti ya msingi iko wapi wakati habari zote zinahusu kutokuwa na hakika?

Thibitisha Mungu yupo.

Tangu nimeanza kujadiliana na wewe, hujaweza kuthibitisha Mungu yupo.
 
Sasa hapo tofauti iko wapi?

Tofauti ya msingi iko wapi wakati habari zote zinahusu kutokuwa na hakika?

Thibitisha Mungu yupo.

Tangu nimeanza kujadiliana na wewe, hujaweza kuthibitisha Mungu yupo.
We hizo maana za imani haujaanza kubadili katika huu mjadala tu,miaka yote ndiyo unavyofanya hivyo.

Tatizo wewe hata hilo neno "hakika" nina hakika linakutatiza.

"Nikisema nakuja nyumbani kwako, nina imani upo kunipokea na sitakuta mlango umefungwa na hakuna wa kunipokea...."

Ubadili huo mfano wako hapo kwa kuuondoa kwenye imani na kuufanya ni hakika ili tuone hakika ina maana gani.
 
Kwa hiyo Mungu wenu alikuwa na makusudio mengine Ila yakabadilishwa na wanadamu ambao ni Adam na Hawa!?

Yaani baada ya kumtetea huyo Mungu wenu ndiyo mnazidi kumpoteza kabisa na kutufanya tukubali kuwa hayupo.
 
kama uncle Magu tu hapangiwi anapanga mwenyewe
 
Kwa hiyo Mungu wenu alikuwa na makusudio mengine Ila yakabadilishwa na wanadamu ambao ni Adam na Hawa!?

Yaani baada ya kumtetea huyo Mungu wenu ndiyo mnazidi kumpoteza kabisa na kutufanya tuamini hayupo.
Mkuu, we Mungu wako ni yupi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…