Wewe unasemaje yupo au hayupo.
Mungu anayesemwa kuwa muweza yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote, aliyeumba ulimwengu, hayupi. Ninhadithi tu. Ni dhana.
Kwa nini?
Kwa sababu, habari ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe kabla mimi sijapinga uwepo wake. Ina kitu kwa Kiingereza kinaitwa "contradiction". Contradiction mara nyingi inaonesha habari ina uongo.
Kwa nini?
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, ana uwezo wote, ujuzi wote, uoendo wote wa kuumba ulimwengu ambao baya lolote haliwezekani.
Asiki yake haimruhusu kujinasibisha na chenye ubaya. Hususan kama anaumba viumbe anaowapenda. Angefanya yote ili ubaya usiwezekane.
Tunaona ulimwengu huu una mabaya mengi. Vifo, magonjwa, vita, majinzi, majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi na tsunami etc.
Imekuwaje Mungu huyo akaruhusu ubaya wote huu ilhali alikuwa nanuwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Usijibu hayo mabaya yametokana na uasi au dhambi za watu.
Tushapangua hoja hiyo. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani.
Usijibu kuhusu freewill. Tushaona freewill haipo ni ndoto tu.
Sasa swali linabaki. Mungu mnayemsema yupo alipokiwa anaumba ulimwengu, mwanzo kabisa, kablabya kuumba chochote, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mazuri tu ndiyo yanawezekana. Mabaya hayawezekani.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huo, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?