Je inawezekana kuunganisha kin'gamuzi kimoja TV tatu?

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,418
Reaction score
9,209
Je inawezekana kuunganisha king'amuzi kimoja(mfano Azam) na tv mbili au tatu vyumba tofauti ?
Zote kuonesha channel chaneli iliyo chaguliwa sio shida.
 
[emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Je inawezekana kuunganisha king'amuzi kimoja(mfano Azam) na tv mbili au tatu vyumba tofauti ?
Zote kuonesha channel chaneli iliyo chaguliwa sio tatizo.
 
Je inawezekana kuunganisha king'amuzi kimoja(mfano Azam) na tv mbili au tatu vyumba tofauti ?
Zote kuonesha channel chaneli iliyo chaguliwa sio shida.
Inawezekana tu, ila kwa TV tatu hapo unaweza kuongeza kitu kinaitwa splitter maana nyuma ya decoder ya azam kuna tundu moja la kutoa waya wa kwenda kwenye tv ya pili linaitwa RF out, ukiweka splitter apo litatoa nyingi tu.
 
yap tafuta kitu kinaitwa splitter, tegemea na port utakayochagua kuna hdmi splitter na av cable splitter
 
Haya Si ndo Yale Mmoja Akichange Channel .. wote Zinabadilka kwa TV zote 3
 
Inawezekana tu, ila kwa TV tatu hapo unaweza kuongeza kitu kinaitwa splitter maana nyuma ya decoder ya azam kuna tundu moja la kutoa waya wa kwenda kwenye tv ya pili linaitwa RF out, ukiweka splitter apo litatoa nyingi tu.
Nina shaka na hilo! Azam decoder inayo loop out siyo RF out.Loop out inakuwezesha kutumia LNB /dishi moja na ving'amuzi viwili.
 
Naomba niunge swali langu hapa.
Inawezekana kutumia dish moja kila mtu akawa na king'amuzi chake
mfano dish la azam kila mmoja akawa na kinga'amuzi cha azam mka share dish moja?
 
Fafanua kidogo hapo mkuu, umeniacha tegeta kwa ndevu kabisa huko
mfano king'amuzi cha azam kina port mbili tofauti za output za hdmi na zile za kawaida za audio na video

Photo2047.jpg

hapo utachagua mwenyewe port ya kutumia kama ni hdmi au hio av cable.

kama utaamua ni hdmi itabidi utafute hdmi splitter
hdmi-splitter-1x4-rear-new.jpg

hapo unachomeka waya mmoja wa hdmi na hio splitter inakupa port 4 za output ambazo unaweza eka tv 4 tofauti.

kama utachagua av cable nayo hivyo hivyo utanunua spliter yake na kusambaza japo sijawahi ona hio splitter naona to switch.

njia nyengine rahisi ni kucheza na port za tv connect tv ya kwanza na decoder yako halafu tv ya pili itapata signal toka tv ya kwanza na tv ya tatu itapata signal toka tv ya pili. cheza tu na input na output cable
 
Je inawezekana kuunganisha king'amuzi kimoja(mfano Azam) na tv mbili au tatu vyumba tofauti ?
Zote kuonesha channel chaneli iliyo chaguliwa sio shida.
Inawezekana kwa kutumia splitter wengine wanaita distributer lakini remote itakuwa moja
 
mfano king'amuzi cha azam kina port mbili tofauti za output za hdmi na zile za kawaida za audio na video

Photo2047.jpg

hapo utachagua mwenyewe port ya kutumia kama ni hdmi au hio av cable.

kama utaamua ni hdmi itabidi utafute hdmi splitter
hdmi-splitter-1x4-rear-new.jpg

hapo unachomeka waya mmoja wa hdmi na hio splitter inakupa port 4 za output ambazo unaweza eka tv 4 tofauti.

kama utachagua av cable nayo hivyo hivyo utanunua spliter yake na kusambaza japo sijawahi ona hio splitter naona to switch.

njia nyengine rahisi ni kucheza na port za tv connect tv ya kwanza na decoder yako halafu tv ya pili itapata signal toka tv ya kwanza na tv ya tatu itapata signal toka tv ya pili. cheza tu na input na output cable
Shukrani sana mkuu kwa maelezo.

Sasa inawezekana kila TV kuangalia chanell yake au TV moja mfano ikiwekwa ITV basi wote inabidi muangalie ITV??
 
Inawezekana kwa kutumia splitter wengine wanaita distributer lakini remote itakuwa moja
Inawezekana kwa kutumia splitter wengine wanaita distributer lakini remote itakuwa moja
Decoder ya Azam inayo output tatu:
1.Loop out hii ni ya kuanganisha na king'amuzi kingine.
2.HDMI output
3.RCA (yellow,white, red) output.
-Moja Splitter inatumika na HDMI au RCA cable?
-Pili HDMI na RCA cables ni fupi ,sidhani zipo ndefu ya chumba hadi chumba.
 
Back
Top Bottom