Je, inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?

Je, inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?

Inawezekana zina madhara makubwa sana kweli,lakini nilipokuwa mdogo nakumbuka kuwaona wagonjwa wengi wa UKIMWI wakiwa katika hali mbaya na kufariki(ina maana haya yalikuwa maigizo tu?),baba anaondoka kwa ugonjwa,mama anafatia na dalili zile zile kisha kichanga nacho kinafuatia,na baada ya miaka kadhaa wale waliokuwa vimada wa baba wanafuatia kwa dalili zile zile.Na hayo magonjwa mengine walikuwa wanapimwa na kupatiwa matibabu yake na chakula bora pia na bado walikuwa wanazidi kuugua tu.Watu walikuwa wanafariki hata kabla ya hizo ARV's,na je kabla ya UKIMWI kutangazwa kama HIV/AIDS kuna ushahidi kwamba ulikuwepo na ulikuwa ukijulikana(hata kwa jina lingine) na watu walitambuaje kwamba ndio wenyewe(dalili kwa mgonjwa) na walitambuaje(vipimo vya kugundua kuwa mtu alikuwa nao),hapa nazungumzia kabla ya concept ya "HIV" hajasingiziwa kusababisha AIDS "peke yake".

Mi naomba unijibie swala la hapo juu.... hii nimeishuudia pia mimi na kwa umri nilikua mkubwa tu wa kujitambua!!!! ukinijibu scenario hizo itakua vizuri.
cc: Deception

Nafurahi sana ninavyozidi kupata mifano dhahiri.

Jaribu kufikiria out of the box basi... usifurahie kila kitu, do home work kidogo
 
Last edited by a moderator:
Nafurahi sana ninavyozidi kupata mifano dhahiri.
Unajua kitu kikiwa cha uongo,ni vigumu sana kukitetea.Mfano kama umeiba kuku ukamfunika na shati au kanga,kuna muda tu atalia kwiioo,halafu watu watashtuka "eeh kumbe ameficha kuku huyu".Hii mifano hata mimi ninayo mingi sana lakini nilijua kwamba kutokana na ukweli wa haya ninayosema,lazima kuna watu wataleta mifano yao ili iweze kuakisi yale ninayoyasimamia.Kama nikitoa mifano yangu binafsi,watu wanaweza kusema nimefoji.Lakini mifano inakuja yenyewe humu.
Hata wewe jaribu kuanzisha mada hii katika watu wengi sehemu yoyote ile ambapo unafahamiana na watu,halafu jifanye kama huna uelewa vile,halafu sikiliza watu wataema nini.Hapo ndipo utakapothibitisha kwamba haya mambo ni kasumba tu,na hatupati muda wa kukaa chini kuyazamia kwa kina kwa sababu ya ugumu wa maisha ndio maana hatujui ukweli ulivyo.Ila ukiupa nafasi ubongo wako kuhoji kidogo tu,utaona mwanga wa ukweli huooo unakuja.Basi kila kitu ndivyo kilivyo,ukikipa muda kwenye ubongo tu basi utajua mengi sana yaliyojificha.
Dunia hii watu wabinafsi wameshaiharibu kwa tamaa zao.Kila eneo/sector inaweza kutumika kufanya biashara.Watu hawajui kama sector ya afya duniani nayo ni biashara na ndio maana ni vigumu sana watu kuelewa masuala haya tunayojadili.

Mtu mmoja anatumia ARVs hadi anakufa/maisha yake yote,sasa kuna watu wangapi Tanzania wanatumia ARVs,halafu jumlisha idadi hiyo na wale wa nchi nyingine duniani nao wanatumia kila siku.Halafu idadi hiyo zidisha na gharama za ARVs kwa mtu mmoja.Yaani unapata figure kubwa sana hata kwenye calculator haikai.Hawa jamaa unafikiri kwa faida hii wanayoipata watakwambia kwamba dawa imepatikana?Najua HIV ni feki,lakini pamoja na hayo hawawezi kukwambia kama dawa imepatikana hata siku moja kutokana na faida wanayoipata.

Magonjwa yote halisi yana dawa,ukiona ugonjwa hauna dawa ujue huo ni feki(yaani haupo kiuhalisia).
 
Usijali doctor,najua ni uchovu tu unaotokana na kazi za kutwa ambao hata mimi naweza kuwa nao.Usiku mwema.

mkuu Deception kweli nimeamini mwanzo mgumu kule mwanzo response ya watu ilikuwa ndogo mno ukilinganisha na coverage ya janga hili maana naamini ktk kila familia lipo ama ukoo ama kwa jamaa na marafiki wa wanaJF ila sasa japo nachungulia humu mara moja moja naona dhahiri Mungu kaajaliwa watu sasa wameamka
pia nakumbuka maneno ya raisi flan wa marekani "unaweza kuwadanganya watu fulani kwa muda wote ila huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda wote" wengi wamekuwa wakiwalaani wazungu juu ya kuikoloni Afrika ila kwa mauwaji indirect ly wanayofanya sasa ni zaid ya maovu yote ya ukoloni mkuu nakupongeza kwa moyo wako wa kujitolea mungu akubariki. Gud nait
 
Last edited by a moderator:
Mi naomba unijibie swala la hapo juu.... hii nimeishuudia pia mimi na kwa umri nilikua mkubwa tu wa kujitambua!!!! ukinijibu scenario hizo itakua vizuri.
cc: Deception

Jaribu kufikiria out of the box basi... usifurahie kila kitu, do home work kidogo

Nilishamjibu,au hukuona?
Najua pia hata jinsi ulivyouliza tu,inaonekana kabisa hukujiandaa kuelewa.Sasa kama kweli unahitaji hoja zenye mashiko kati ya mimi na wewe twende taratibu hoja kwa hoja halafu wana JF wajionee wenyewe nani mkweli.Haya,kwa kuwa najua umekuja kupinga na si kujadili,sasa unahitajika ueleze wapi mimi sikusema kweli na wewe useme ukweli ni upi halafu tuanze hoja kwa hoja.
 
Exactly,wewe umeelewa.Halafu kuhusu madhara ya dawa,wala huitaji kukubaliana na mimi,hata wenyewe wameandika hayo madhara,hivyo haihitaji mtu kukushawishi kwamba zina madhara.Halafu chukulia unatumia maisha yako yote.

Huhitaji kujiuliza,wameandika wenyewe,halafu nikwambie kitu.Haya madhara hayapo kwa bahati mbaya,wamedhamiria yawe hivyo ili mwisho wa siku wanaotumia wakifa,watu watajua HIV ndio amehusika na wataendelea kuwa na imani kwamba kweli HIV/AIDS ni ugonjwa usio na tiba.Fikiria mara mbilimbili hapo utaona kitu.

Vinginevyo wataendelea kutupa imani kila mwaka eti "wanasayansi wanakaribia kupata dawa ya ukimwi",yaani upumbavu mtupu,dawa gani inakaribia kupatikana miaka zaidi ya 30 sasa?wanatuchezea akili sana hawa.Wakati dawa ya ukimwi ni uelewa wako kuujua ukweli ulivyo.Kataa kupima,kataa kutumia ARVs,Kula vizuri,fanya mazoezi,kunywa maji safi,weka mazingira safi,acha kutumia madawa ya hospitali mara kwa mara pasipo sababu za msingi.Yaani kamwe hutaugua ugua ovyo.Na ukiugua,ukigusa dawa kidogo tu umepona,yaani kama umeme.

Hawa jamaa wanafanya biashara kupitia serikali za nchi husika.Na ndio maana Thabo Mbeki aling'olewa madarakani kwa kushindwa kutetea biashara ya ARVs,Museveni anajua ukweli huu ninaowapa na ndio maana hataki kabisa kusikia mambo haya lakini amekaa kimya kwa kuwa anajua yatakayomkuta akithubutu kugusa maslahi haya,nadhani mnakumbuka alivyogusa maslahi ya Obama kwenye ushoga kilimtokea nini,alisalimu amri mwenyewe.Lakini yeye mwanzo alikataa kabisa watu kupima HIV.

Sasa watu wanaona kwamba Deception ndio anapotosha watu,vipi kuhusu hawa ma rais nao?Hawa nafikiri ndio wenye influence zaidi na wakipotosha wanapotosha kwelikweli.Si mmesikia wenyewe kuhusu South Africa?Sasa hivi wananchi wa SA wanakwambia "I don't fear HIV/AIDS,I fear malaria",hili ndilo zao la Thabo Mbeki.Hivyo bila kuchelewa World's Tycoons wakamuondoa fasta na kuliweka madarakani lile chizi Zuma likaendeleze biashara.Likaanza na vituko eti limetembea na mwanamke mwenye HIV lakini halikupata eti kwa sababu limewahi kunawa haraka.Linasema hivyo ili watu waamini kwamba kweli HIV yupo na ana madhara.Hii dunia hii,kama huijui vizuri utakuwa kama ng'ombe,utaishi bila consciousness.

Kwa niaba ya wasomaji na wapenzi wa Jamii Forum,,, ambao hawawezi ku reply/ comment chochote hapa Jukwaani....

Tunasema Tunashukuru Sana,,,,

Unatuelimisha na Kutufungua Fikra zetu kwa kiasi kikubwa.

again Tunashukuru sana.
 
Sitaki kukupeleka mbali sana kwa kuwa nitakuchanganya.Siku zote penye ukweli uongo hujitenga.Hebu chukua hiyo postulate namba 3 peke yake.

3.Germ lazima asababishe ugonjwa huo huo kama akidungwa kwenye host mwingine mwenye afya.

Sasa nakuuliza wewe.Je,Kila mtu mwenye HIV ana ukimwi?

No siyo Kila Mtu mwenye HIV ana Ukimwi
 
mkuu Deception kweli nimeamini mwanzo mgumu kule mwanzo response ya watu ilikuwa ndogo mno ukilinganisha na coverage ya janga hili maana naamini ktk kila familia lipo ama ukoo ama kwa jamaa na marafiki wa wanaJF ila sasa japo nachungulia humu mara moja moja naona dhahiri Mungu kaajaliwa watu sasa wameamka
pia nakumbuka maneno ya raisi flan wa marekani "unaweza kuwadanganya watu fulani kwa muda wote ila huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda wote" wengi wamekuwa wakiwalaani wazungu juu ya kuikoloni Afrika ila kwa mauwaji indirect ly wanayofanya sasa ni zaid ya maovu yote ya ukoloni mkuu nakupongeza kwa moyo wako wa kujitolea mungu akubariki. Gud nait

Ha ha haaaa,nimeipenda hiyo kwenye blue hapo.Ila humu wapo watu ambao wanaweza kudanganyika kwa muda wote.
Usiku mwema.
 
Kuna mambo mengi sana hapa lazima utakuwa umeya bypass na hasa pale uliposema ulipokuwa mdogo.Hapa lazima utakuwa umemiss taarifa muhimu sana ambazo zinaweza kuelezea hicho ulichokiona bila mizengwe kabisa.Ningekuwapo kipindi hicho na kuwaona hao watu lazima ningekupatia maelezo sahihi kabisa kuhusu ulichokiona.
Fuatilia taratibu reply hizi utaelewa taratibu,huwezi kuelewa au kuukubali ukweli huu kwa siku moja.Ni sayansi nzito sana imetumika kudanganya kwenye ungonjwa huu feki wa HIV/AIDS.Hivyo si rahisi ukaelwa kwa muda mfupi.Yote yale ambayo wewe unadhani yanakuchanganya,yana majibu yake tena ni sahihi kabisa tofauti na sasa unavyofikiri kwamba HIV ndiye anaye/aliyehusika.
Hapa hujajibu chochote mkuu, nimeona maneno mengi tu ambayo obviously ni siasa.... kusema kuna mambo mengi atakua ameyabypass na kumiss taarifa ni kutojibu chochote....
Nilishamjibu,au hukuona?
Najua pia hata jinsi ulivyouliza tu,inaonekana kabisa hukujiandaa kuelewa.Sasa kama kweli unahitaji hoja zenye mashiko kati ya mimi na wewe twende taratibu hoja kwa hoja halafu wana JF wajionee wenyewe nani mkweli.Haya,kwa kuwa najua umekuja kupinga na si kujadili,sasa unahitajika ueleze wapi mimi sikusema kweli na wewe useme ukweli ni upi halafu tuanze hoja kwa hoja.
Ungeingia into details ni vipi hao wazee walikufa kwa style moja mpaka mtoto na mahawara nao wakafata kwa style hiyo hiyo na wakati walikua hawatumii arv, na madawa ya magonjwa nyemelezi waliyatumia....
 
Katika kazi yangu nakutana na wagonjwa wa aina hio kila siku na hakuna hata mmoja anayelalamikia sideeffects zozote.

Watalalamikaje na kukuletea wakati wao wanajua Ni HIV ndo inawasumbua siyo ARV...

Ndo maana Hujawahi kuona wanalalamika maana wanajua Watakufa tu maana Hatawakileta hayo malalamiko na Wewe utasema ni HIV huyo Chukua tena Hizi ARV
 
Kwa niaba ya wasomaji na wapenzi wa Jamii Forum,,, ambao hawawezi ku reply/ comment chochote hapa Jukwaani....

Tunasema Tunashukuru Sana,,,,

Unatuelimisha na Kutufungua Fikra zetu kwa kiasi kikubwa.

again Tunashukuru sana.

Nashukuru pia kwa kutoa muda wa kusikiliza.Pia nakushauri ili uwe vyema zaidi inabidi ufanye utafiti wewe mwenyewe mtaani na mitandaoni ili kujiridhisha na haya niliyosema.Kama utaweza kuwafuatilia kwa ukaribu wale watu waliopo kwenye vituo vya kupimia HIV(feki) hapo utakuwa umefanya la maana sana.
 
Kwa kweli mjadala mzuri sana

1. Kwa kuna UKIMWI na HIV/UKIWMI

2. Kwamba UKIMWI Ulikuwepo tangu enzi na enzi, na baada ya mwili kupungukiwa na kinga ulishambuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo Mkanda wa jeshi, ukurutu nk, lakini magonjwa hayo yalitibiwa na yalipona bila matumizi ya ARV,

3. Kwamba kuanzia miaka ya 80 kulitokea aina mpya ya upungufu wa Kinga UKIMWI unaosababishwa na Virusi vinavyoitwa HIV, na kwamba magonjwa kama Makanda wa jeshi na Ukurutu sasa hauoponi kwa tiba ile ya zamani, na badala yake ni ARV

Naona Watu wameshaanza Kutumia Kichwa Kufikiri. Kwa Kuhoji kwako tu huku
 
Yan binamu acha tu
Nna case ya MTU mwingine yeye alipima HIV akakutwa positive akashauriwa apime CD4 akakuta zipo juu hospital wakamwambia awe anarud kuchek kama zimeshuka ili aanzishiwe ARV ni toka 2009 hajarud hospital tena yan yeye anakula vizur,mazoez hana stress na yuko poa kabisa na mpango wa kupima tena hana.
Hahahahahahhaha
Mwambie Akapime inawezekana ikawa Imevapour
 
Hapa hujajibu chochote mkuu, nimeona maneno mengi tu ambayo obviously ni siasa.... kusema kuna mambo mengi atakua ameyabypass na kumiss taarifa ni kutojibu chochote....

Ungeingia into details ni vipi hao wazee walikufa kwa style moja mpaka mtoto na mahawara nao wakafata kwa style hiyo hiyo na wakati walikua hawatumii arv, na madawa ya magonjwa nyemelezi waliyatumia....

Mkuu tulia kwanza,unaonekana wazi kabisa kwamba hata ukipewa jibu sahihi utapinga tu,kwa maana umeshakaa stance kabisa,jibu lolote litakalokuja mbele yako ni kupinga tu bila kujali kama ni kweli au la,ha ha haaa.Wenzetu wazungu hawako hivi kabisa,hivi kwa nini sisi weusi tuko hivi?

Sasa inaonekana hujalielewa jibu nililotoa kwa sababu ya bias.Usijali,ili nikujibu kama unavyotaka naomba unijibu swali hili kwanza.Kumbuka kwamba nina nia kabisa ya kukujibu,ndio maana niko humu.

Swali:Naomba unitajie dalili kuu tano za ugonjwa fulani.
 
Swali zuri sana hilo.Sijui kama umemuelewa alivyojibu.

Nimemuelewa hii nafikiri ni ile theory yao ugonjwa umetokea kwa masokwe, huko misitu ya Ikweta kwa ndugu zetu wanaokula Nyama pori za jamii ya manyani. Kitu ambacho kinapingwa na Dr Duesberg na wenzake.
 
Mkuu tulia kwanza,unaonekana wazi kabisa kwamba hata ukipewa jibu sahihi utapinga tu,kwa maana umeshakaa stance kabisa,jibu lolote litakalokuja mbele yako ni kupinga tu bila kujali kama ni kweli au la,ha ha haaa.Wenzetu wazungu hawako hivi kabisa,hivi kwa nini sisi weusi tuko hivi?

Sasa inaonekana hujalielewa jibu nililotoa kwa sababu ya bias.Usijali,ili nikujibu kama unavyotaka naomba unijibu swali hili kwanza.Kumbuka kwamba nina nia kabisa ya kukujibu,ndio maana niko humu.

Swali:Naomba unitajie dalili kuu tano za ugonjwa fulani.
Mkuu kumbuka post yangu ya #93 ndo mana nkasema wewe ni ujanja ujanja kuwatoa watu kwenye mstari.... nimekuuliza swali unajibu kwa swali, kwanini usinijibu kwanza ndo ukauliza na wewe....

Post #93 Nilikwambia hivi wakati nakujibu

*unataka tuamini linki zako ila wengine wakikuwekea unazikataa.... kwanini tuanini link zako na kuacha zingine!??

*Unaulizwa maswali mengi na mengi unajibu kwa kuuliza maswali na wewe, hapo unazidi kujichanganya

.......... nijibu haya tu na kazi imeisha......

*ukimwi ulianza kugundulika kwa mtu wa kwanza kabla ua arv kuwepo.... aliupata kwa njia gani bila ya kuambukizwa kupitia arv!??

*arv ya kwanza kugundulika ilikua 1988 lakini kwa tabzania zilichelewa kufika mpaka miaka ya mwanzo ya 90, je kwa kipindi chote hicho maambukizi yalikua kwa njia gani!??

*TB unayoisema imeanza zamani sana na wagonjwa walikua wanapata dawa mbalimbali, inakuaje kwa tb hii kuuwa watu wengi namna hiyo na kukondesha kiasi hicho.

*kama ni TB mbona ukimwi unasemekana ulianzia Bukoba miaka hiyo, watu wa mikoa mingine walikua hawaugui TB!?? kwanini na wenyewe wasiishe kama watu wa BK walivyokua wanadhoofika

naomba majibu kwanza na usinijubu kwa maswali tafadhari

Madaktari wengi najua wanaipita hii thread kwa sababu ya style yako ya kujibu.... unastory ndefu zisizo na scientific proves
 
Ah well, sichepuki! Though niko vyombo nimepitia pitia hii sread japo kuna mikanganyiko mingi hakuna suluhisho la pamoja!

Wasi wasi ndio akili..... Kanyesha ni kanyesha tu IPO na ilikwepo na itaendelea kuwepo manake bado sijaona jitihada za kuimaliza au ugunduzi wa dawa wala tiba!

Sent from JamiiForums
 
Mbona kwa Tanzania wapo wengi tofauti na tafiti hizo?Yaani ni wengi sana kiasi kwamba hata humu JF wapo.

Kwetu wanaweza wakawepo, ila si wengi kama unavyoiput. Na zaidi si kitu kilichokuwa documented hivyo kufahamu hasa idadi si rahisi. Ila based on cases nilizowahi kuziona clinic naweza kusema mi chache out of watu wote waliokuja kupima. Sasa hao wa jamiiForums unaowasema mkuu, je, ni documented cases au ndo zile za washkaji kuongea wanachojisikia tuu? Na zaidi, kwenye medicine, distribution ya traits mara kadhaa hiwa ni normal...hasa kwa zile ambazo zipo universal. Hivyo ukiona kitu kiko kidogo nje basi na kwetu itakuwa more or less hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom