Je, inawezekana Rais wa Tanzania akajiuzulu kisheria?

Je, inawezekana Rais wa Tanzania akajiuzulu kisheria?

Navyofahamu mimi ni bunge pekee ndio lina weza kupiga kura ya kutokua na iman na rais endapo rais. Endapo serikali itapeleka mswada bungeni (wowote) ukakataliwa Mara mbili ,hapo ni rais kilivunja bunge ama bunge kupiga kura ya kutokua na iman na rais , sijabahatika kuona kifungu cha katiba ambacho kinampa mwananchi mamlaka ya moja kwa moja kupiga kura ya kutokua na Iman na rais isipokua kupitia bunge la jamhuri. Endapo rais akipigiwa kura ya kutokua na Iman bas makamu wa rais atachukua hatamu kumalizia kipindi kilichobaki ili kufikia uchaguzi mkuu. Ni 2/3 ya bunge kupiga kura ya ndio ndipo rais ataondoka madarakan. (Zaid tuwangoje wajuv wa mambo zaid).
 
Ibara ya 37(5) ya katiba ya jamhuri ya muungano qa Tanzania ta mwaka 1977 inasema hivi IEndapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki, KUJIUZULU ,Kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake na shughuli za Rais ,basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yalioelezwa katika ibara ya 40 ,kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la MTU atajayekuwa makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitiwa na Bunge kwa kura zilsizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.kutokana na nukuu hiyo ya katiba bila shaka Rais anaweza kujiuzulu. Pia kuhusu Rais aliyepita kurudi madarakani hauwezekani pia katiba imesema hivi katika ibara ya 40(2) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 Hakuna MTU atakayechaguliwa zaidi ya Mara mbili kushika kiti cha Rais.
Shukran mkuu kwa kufafanua. Ila kwa mfano utendaji wa Raisi ni mbovu, nini majukumu wa Raia kumwajibisha.
 
Mpaka sasa hajatokea mfafanuzi mzuri wa hili swala.
 
Kwakuwa tumewachagua wawakilishi wa kutuwakilisha bungeni basi kupitia wabunge hao tupeleke kero zetu kwao nao kwa sababu katiba imewapa mamlaka ya kumuondoa Rais katika ibara ya 46(A) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.hivyo unaweza kumondoa Rais kwa kupitia mbunge wako au kupitia uchaguzi mkuu. Maandamo ni haki katika demokrasiua lakini maandamano hayakupi mwananchi nguvu ya kumuuondoa Rais kisheria Bali unatimiza tu haki yako ya kidemokrasia ya kupinga au kuunga mkono mtazamo Fulani kitika siasa.Kumbuka tu maandamano pia yanaweza pia kuwa moja ya alama za kuhashiria mapinduzi katika nchi yanakaribia mfano halisi ni Misri ila ole wenu mkashindwa kupindua maana kosa lake linaitwa Uhaini .Kwa taifa letu sikushauri uthubutu hata kujaribu maana Ulinzi wa nchi ni mkali sana na sheria za nchi yetu ni Kali sana katika jambo la Uhaini. Mbinu nzuri na salama kwako ni kusubiri kutumia sanduku la kura au pelaka kero yako kwa mbunge ili watumie haki yao ya kikatiba.
 
Back
Top Bottom