Usahihi ni kwamba kuna kipande cha mfupa wa fuvu (skull-NA SIO UBONGO) kimetolewa kutoka kichwani, na kuhifadhiwa kwenye sehemu ya mbele ya tumbo (anterior abdominal wall-na sio tumboni ndani), ili kisipoteze "uhai" wake kwa mfano blood supply.
Hii hufanyika pale mtu anapopata brain injury na kupelekea ubongo "kuvimba" hivyo kuongeza presha kwenye fuvu; Walichofanya madaktari ni kuondoa kipande cha fuvu ili kuupa nafasi ubongo uweze kutanuka kwa nafasi bila kusababisha madhara, then baada ya muda, ubongo ukishakua vizuri, wanaunganisha tena hicho kipande cha fuvu kilipokua.
Pia, hakuna "communication" yoyote kati ya kipande cha hilo fuvu kilichohifadhiwa kwenye sehemu ya mbele ya tumbo na ubongo, na wala hakuna ubongo wowote kwenye kipande hicho, ni kipande tu cha mfupa.