Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Kwa mujibu upi ? BIBLIA sio Quran

  1. Mungu wa kweli – Yesu ni Mungu wa kweli, sehemu ya Utatu Mtakatifu.
    Aya: Yohana 10:30 - "Mimi na Baba yangu tuko moja."
  2. Muumba wa vitu vyote – Yesu aliumba vitu vyote vilivyoko mbinguni na duniani.
    Aya: Yohana 1:3 - "Vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, wala pasipo yeye, hakika hakuna kilichoumbwa kilichokuwepo."
  3. Mwenye uwezo wa kuponya magonjwa – Yesu alifanya miujiza ya kuponya na kuponya magonjwa.
    Aya: Mathayo 4:24 - "Habari zake zilienea pote, watu walileta kwake wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na walioonewa na mapepo."
  4. Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja – Yesu alikuwapo kama Mungu na mwanadamu, akiwa na asili mbili.
    Aya: Yohana 1:14 - "Neno alifanyika mwili, akakaa kati yetu."
  5. Mfalme wa Amani – Yesu alileta amani duniani, kama Mfalme wa kweli wa Amani.
    Aya: Isaiah 9:6 - "Kwa maana mtoto amezaliwa kwetu, mwana ametupewa; na utawala utakuwa bega lake. Naye ataitwa jina lake, mshauri ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani."
  6. Mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi – Yesu anayo mamlaka ya kusamehe dhambi za watu.
    Aya: Marko 2:10 - "Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi duniani..."
  7. Mchungaji mzuri – Yesu ni mchungaji ambaye hutunza kondoo wake kwa upendo.
    Aya: Yohana 10:11 - "Mimi ni mchungaji mzuri. Mchungaji mzuri huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo."
  8. Mufufuo na Uzima – Yesu anatoa uzima wa milele kwa wale wanaomwamini.
    Aya: Yohana 11:25 - "Mimi ni ufufuo na uzima; ye yote aaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa hai."
  9. Mwenye haki na kweli – Yesu alileta ukweli na haki duniani.
    Aya: Yohana 14:6 - "Mimi ni njia, kweli, na uzima; hakuna ajaye kwa Baba ila kwa njia ya mimi."
  10. Alitoka kwa Baba – Yesu aliletwa duniani na Baba yake kwa kusudi maalum.
    Aya: Yohana 8:42 - "Yesu akawaambia, Kama Mungu alikuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa sababu mimi nilitoka kwa Mungu."
1.Alimaanisha kuwa katika umoja wa maadili na utendaji, lakini sio kwamba ni mmoja kwa maana ya uungu.
2.Nimeshakupa maandiko kuwa aliyeumba ni mmoja tu
3.Aliponya kwa idhini ya Allah si kwa uwezo wake.
4.Haiwezekani Mungu kuwa binadamu.
5."Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nimekuja kumtenganisha mtu na baba yake, na binti na mama yake, na binti-mkwe na mama-mkwe; na adui wa mtu atakuwa wa nyumbani mwake."
Hivyo usiseme yesu ni mfalme wa amani wakati yeye mwenyewe kakataa kuleta amani.
6.Dhambi alikuwa anasamehe Mungu ila yeye alikuwa anafikisha ujumbe tu
Yohana 5:19
"Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Mwana hawezi kufanya neno lolote kwa ajili yake mwenyewe, ila atakacho kuona Baba akifanya; kwa maana mambo yote ambayo Baba hufanya, Mwana pia hufanya vivyo hivyo. "
7.Uchungaji wa Yesu unahusisha uongozi, huduma, na kujitolea kwa ajili ya wafuasi wake. Anawajali na anawafundisha, na anatoa maisha yake kwa ajili yao, akiongoza kondoo wake katika njia ya haki na wokovu.
8.Nikuulize kwanza nani kapata uzima wa milele duniani?
9.Kuleta haki haimaanishi wewe ni Mungu.
10.Watu wote tunatoka kwa Bwana
Zaburi 127:3
"Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa Bwana, na matunda ya tumboni ni thawabu."
 
Yesu sio Allah mungu wa kikureshi

Yohana 10:18:

"Hakuna aniondoleaye uhai wangu, bali mimi mwenyewe niutoa. Nami nina mamlaka ya kuutoa, na tena nina mamlaka ya kuupokea. Amri hii nimepewa na Baba yangu."
Shida ni kwamba alikufa hivyo hana uzima wa milele kama aliokuwa nao Mungu.
 
UNAELEWA MAANA YA ALFA NA OMEGA?

PIA naomba ujibu maswali ninayokuuliza ,

Unauliza maswali tu kujibu hutaki

Nauliza tena Torat ,zaburi na Injili Original ziko wapi tufananishe na hizi unazosema zimeharibiwa

SWALI NI GUMU?
Sasa ndio nakuambia zimeharibiwa na wayahudi kwa kupunguza na kuongeza maneno kwa ajili ya manufaa yao.
 
Hapa ni Yohana 1:1:

"Hapo mwanzo kulikuwa Neno, na Neno alikuwapo pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu."

Aya hii inaonyesha kuwa Neno (ambalo ni Yesu) alikuwapo tangu mwanzo, na alikuwa pamoja na Mungu, na alikuwa Mungu.
Isaya 44:24 inaonyesha aliyeumba ni mmoja tu peke yake
Kwa hiyo usiniambie kuwa yesu kashiriki katika uumbaji.
 
Unejuaje au kwa ushahidi upi kuwa viliharibiwa, ni mwaka gani
Taurati na Injili zilivyopotoshwa

Taurati na Injili zilizo teremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu bila shaka ni maneno yake na zina ukweli ndani yake. Hata hivyo, Wayahudi na Wakristo—Mwenyezi Mungu awalaani—waliziharibu, wakazibadilisha, wakaziongeza na kuziondoa sehemu fulani, na kufanya kila moja kuwa na nakala nyingi zinazo kinzana na kukanusha baadhi ya mafundisho yake. Hivyo basi, ukweli ndani ya vitabu hivyo umechanganyika na batili, na haiwezekani kutofautisha kati ya kweli na uongo isipokuwa kupitia sheria yetu (Qur'an), ambayo imehifadhiwa kutokana na mabadiliko na upotoshaji kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

"Hakika Sisi tumeliteremsha hilo onyo (Qur'an), na hakika Sisi tutalihifadhi." (Al-Hijr: 9)

Hivyo basi, Qur'an inatosha kama mwongozo, kwani Mwenyezi Mungu amesema kuhusu kitabu hiki:

"Hatukuacha chochote katika Kitabu." (Al-An’am: 38)


---

Hadithi ya Umar Ibn Al-Khattab

Imepokelewa kutoka kwa Jabir bin Abdillah (RA) kwamba Umar Ibn Al-Khattab (RA) alimletea Mtume Muhammad (SAW) kitabu alichopata kutoka kwa baadhi ya watu wa Kitabu (Wayahudi na Wakristo). Mtume alikisoma na akakasirika, kisha akasema:

"Je, mmekosa imani na sheria yetu, ewe Ibn Al-Khattab!? Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, nimekujeni nikiwa na ujumbe huu safi na wenye nuru. Msiwaulize wao chochote, kwani wanaweza kuwaambia ukweli na nyinyi msiwaamini, au wakawaambia uwongo na nyinyi mkawaamini. Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, lau Musa (AS) angekuwa hai leo, asingekuwa na budi ila kunifuata."

(Riwaya ya Ahmad na wengineo, imepokelewa kwa njia nyingi na, mkusanyiko wake unaonyesha kuwa ina asili yake.)

Hadithi hii inaonyesha kuwa sheria ya Kiislamu ni kamilifu, imehifadhiwa, na haina haja ya kurejea katika vitabu vya kale vilivyochanganyika na batili.


---

Dalili za kupotoshwa kwa Taurati na Injili

1. Kutoelewana kwa yaliyomo na migongano katika Taurati na Injili

Ikiwa zingekuwa na uhalisia wake wa kwanza kutoka kwa Mwenyezi Mungu, zisingekuwa na mizozo ya ndani. Qur'an inasema:
"Je, hawaizingatii Qur'an? Na kama ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi." (An-Nisa: 82)



2. Kauli ya Mwenyezi Mungu:

"Katika wale walioyahudishwa wapo wanaopotosha maneno katika sehemu zake." (An-Nisa: 46)

Hii inaonyesha kuwa Wayahudi waliharibu maana ya maandiko yao.



3. Uongo wa wazi katika vitabu vyao

Mfano ni hadithi ya uwongo katika Taurati inayodai kuwa Nabii Lut (AS) alifanya zinaa na mabinti zake baada ya kulewa.



4. Kauli ya Ibn Hazm kuhusu kupotoshwa kwa vitabu hivi

Ibn Hazm anasema: "Tumeambiwa kuwa baadhi ya Waislamu wanapinga kuwa Taurati na Injili zilipotoshwa. Wanaosimamia maoni haya hawajali maana ya Qur'an na Sunnah, ambazo zinasema waziwazi kuwa watu wa Kitabu waliharibu maneno ya Mwenyezi Mungu."



5. Qur'an inathibitisha kuwa Muhammad (SAW) ametajwa katika Taurati na Injili

"Wale wanaomfuata Mtume, Nabii asiye na elimu ya kusoma wala kuandika, ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili." (Al-A'raf: 157)




Kwa hivyo, kupotoshwa kwa vitabu hivi ni jambo lililokubaliwa na wanazuoni wa Kiislamu, ingawa kuna mitazamo tofauti kuhusu kiwango cha upotoshaji.


---
 
Ndio maana anaitwa Emmanuel,MUNGU PAMOJA NASI
Hilo jina linatumika kuleta ujumbe kuwa Mungu yupo pamoja na hawaachi waja wake lakini haimaanishi kuwa anayeitwa jina hilo ni Mungu kwa mfano;

Elisha (Elisha) – "Mungu ni wokovu"
Ezekiel – "Mungu ana nguvu"
Daniel – "Mungu ni mwamuzi wangu"
Gabriel – "Mungu ni nguvu yangu"
Raphael – "Mungu ameponya"
JE, WENYE MAJINA HAYO NAO PIA NI MIUNGU?
 
Aya hii inaonyesha kuwa Yesu ni ufunuo wa Baba, na kwa kumjua Yesu, mtu anamjua Baba. Yesu alikuja kumfundisha Mungu kwa njia ya maisha yake na mafundisho yake.
Alitumwa kumfundisha Mungu kwa wanaadamu lakini yeye si Mungu
 
Aya hii inasema kuwa Yesu ndiye aliyemfunua Mungu kwa watu, kwani alikuja kutangaza tabia na asili ya Mungu kwa ulimwengu.
Mungu alimpeleka yesu kwa wana wa Israel ili awasadikishie yaliyopo katika Taurat na kama ulivyosema ili wamfahamu Mungu kupitia yeye lakini yeye si Mungu bali ni Mjumbe wake tu.
 
Kwenye miziki yenu ya Mwaipaja, gozbert hayo maneno yapo? Sana sana hazina tofauti na miziki ya shetani kuiongelea dunia na ufahari wake mfano Ipo siku ya good luck gozbert, oludumare inapigwa mpka night club, nyingine inaitwa Upo single 😁
Kunachokutesa wewe ni wivu kuona injili inapenye kila mahali,nani aliyekwambia nyimbo za injili ziishie makanisani.

Kwa taarifa yako mkakati maalumu ni kufanya kila sikio lisikie ukuu wa Mungu,kupitia mwanawe Yesu kristo..kupitia uimbaji hasa nyimbo za injili.

Asante na endelea kusikiliza neno la Mungu kupitia gosple songs hata ukiwa gest.
 
Kinacho wachanganya ni ile miujiza Kutoka kwa Mungu huenda Hata Mussa wangemuita Ni Mungu..

zamani watu walikuwa wanatamani sana kumuona Mungu Ndo maana kila Chenye miujiza waliita ni Mungu
Musaa alifanya miujiza mingi sana ndio iliyempa nguvu ya kuwafanya wana waisrael wamuamini.
 
Ujinga mtupu uliopandikizwa kwenye vichwa vya waafrika eti injili ndiyo maana wanaosali makinisani na misikitini ndiyo masikini zaidi kuliko wachungaji na masheikh
 
Umeona umejibu vzuri sana so tuseme tu mnahangamia kwa kuyakosa maarifa..

hzo pesa mnazo wapa wale matajiri mle kanisani wale Ndio wenye njaaa?

Biblia ndo inasema usaidie wenye uhitaji wewe unasema usimpangie mtu pa kupeleka hamuoni kama mnapishana na biblia yenu au hamuiamini?

Hauwezi kukuta kanisa fulani limepeleka msaada kwa wahtaji zaidi utakuta ni taasisi flani imefanya charity yani ni project na ni kwa lengo la kupata Grants au kujitangaza sio kwa imani yenu
Kama sio imani yetu wewe mbona unateseka..ukitoa msaada wewe inatosha.

Acha tupeleke kanisani ili injili isonge mbele.
 
Matendo ya mitume ya mitume 2:29-30
Ndugu zangu, napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa, akazikwa, tena kaburi lake liko papa hapa petu mpaka leo. Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.



Kwa hiyo na hapo wamedanganya au?
Pakada jibu swali hili kimeshakulamba tayari
Kujifanya mtaalam kumbe hujui lolote one sasa ulivyodhalilika kwa kusema eti wanaosema Daudi alikuwa nabii ni waongo
 
Back
Top Bottom