Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Huwa mnatumia nguvu nyingi sana kujaribu kutetea ujio wa huyo muarabu na uzombi wake alioambukiza dunia, alitabiriwa ujio wake kama mpinga Kristo.
Kwanza maisha yake hayaendani kabisa na Ukristo, ukizingatia alikua anagegeda katoto Aisha kakiwa na umri wa miaka tisa, pili alihusika kwenye mauaji ya Wayahudi, pamoja na mauchafu mengine mengi.
 
Mungu alikuja duniani kupitia nyeti ya kiumbe aliomuumba ( kwa mwenye akili huu ni uchafu sio dini)

Kwanini asinge kuja kimiujiza.? Tuu asijulikane alipotokea?

Kama mwamuita mungu kisa kazaliwa bila baba mbona Adam hana baba wala mama kwanini msimfanye yeye ndio mungu.

Maana yeye ndio wa ajabu zaidi, Bi hawa nae hakuwa na mama

Hivyo ndio Allah anavyo onesha uwezo wake katika Uumbaji? Ila mnamkufuru

Allah hakuna aliewahi kumuona

Mariam ndio alie ambiwa ata mwita (Yesu) yaani mungu pamoja nasi ni tafsiri ya jina la yesu ila sio mungu

Ila nyie mmemuita Mungu pamoja nasi


Mfano mtu akiitwa Pendo
Haina maana eti anaupendo Bali ni tafsiri ya jina lake

Taja muujiza mmoja wa yesu
Umeelewa hata ulichoandika,ebu kisome vizuri
 
Matendo ya mitume ya mitume 2:29-30
Ndugu zangu, napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa, akazikwa, tena kaburi lake liko papa hapa petu mpaka leo. Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.



Kwa hiyo na hapo wamedanganya au?
Tutayaamini vipi mandiko unayodai sio halali?
 
Huwa mnatumia nguvu nyingi sana kujaribu kutetea ujio wa huyo muarabu na uzombi wake alioambukiza dunia, alitabiriwa ujio wake kama mpinga Kristo.
Kwanza maisha yake hayaendani kabisa na Ukristo, ukizingatia alikua anagegeda katoto Aisha kakiwa na umri wa miaka tisa, pili alihusika kwenye mauaji ya Wayahudi, pamoja na mauchafu mengine mengi.
Yatolee ushahidi wa wazi hayo uliyoyasema wewe!!!
Sio maneno tu!!!
 
Kwa hiyo huyu ni mungu wa waisrael tu

Hapana. Ni description inayolenga kumtofautisha na miungu wengine, pia anaitwa Mungu wa Eliya, Mungu wa Yakobo nk. Kwa kuwa kuna miungu wengi mfano Allah, sijui miungu wa baharini, miungu jua nk ambayo yote ni miungu fake), kuna ulazima wa kuspecify ni mungu yupi hasa unayemzungumzia. Waisraeli wana historia ndefu sana na Mungu wa kweli, ndiyo maana kuwafanyia reference ni sahihi kabisa.
 
Hapana. Ni description inayolenga kumtofautisha na miungu wengine, pia anaitwa Mungu wa Eliya, Mungu wa Yakobo nk. Kwa kuwa kuna miungu wengi mfano Allah, sijui miungu wa baharini, miungu jua nk ambayo yote ni miungu fake), kuna ulazima wa kuspecify ni mungu yupi hasa unayemzungumzia. Waisraeli wana historia ndefu sana na Mungu wa kweli, ndiyo maana kuwafanyia reference ni sahihi kabisa.
Unatumia criteria gani kujua yupi ni fake na yupi si-fake?
 
Kwa mujibu upi ? BIBLIA sio Quran

  1. Mungu wa kweli – Yesu ni Mungu wa kweli, sehemu ya Utatu Mtakatifu.
    Aya: Yohana 10:30 - "Mimi na Baba yangu tuko moja."
  2. Muumba wa vitu vyote – Yesu aliumba vitu vyote vilivyoko mbinguni na duniani.
    Aya: Yohana 1:3 - "Vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, wala pasipo yeye, hakika hakuna kilichoumbwa kilichokuwepo."
  3. Mwenye uwezo wa kuponya magonjwa – Yesu alifanya miujiza ya kuponya na kuponya magonjwa.
    Aya: Mathayo 4:24 - "Habari zake zilienea pote, watu walileta kwake wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na walioonewa na mapepo."
  4. Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja – Yesu alikuwapo kama Mungu na mwanadamu, akiwa na asili mbili.
    Aya: Yohana 1:14 - "Neno alifanyika mwili, akakaa kati yetu."
  5. Mfalme wa Amani – Yesu alileta amani duniani, kama Mfalme wa kweli wa Amani.
    Aya: Isaiah 9:6 - "Kwa maana mtoto amezaliwa kwetu, mwana ametupewa; na utawala utakuwa bega lake. Naye ataitwa jina lake, mshauri ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani."
  6. Mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi – Yesu anayo mamlaka ya kusamehe dhambi za watu.
    Aya: Marko 2:10 - "Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi duniani..."
  7. Mchungaji mzuri – Yesu ni mchungaji ambaye hutunza kondoo wake kwa upendo.
    Aya: Yohana 10:11 - "Mimi ni mchungaji mzuri. Mchungaji mzuri huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo."
  8. Mufufuo na Uzima – Yesu anatoa uzima wa milele kwa wale wanaomwamini.
    Aya: Yohana 11:25 - "Mimi ni ufufuo na uzima; ye yote aaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa hai."
  9. Mwenye haki na kweli – Yesu alileta ukweli na haki duniani.
    Aya: Yohana 14:6 - "Mimi ni njia, kweli, na uzima; hakuna ajaye kwa Baba ila kwa njia ya mimi."
  10. Alitoka kwa Baba – Yesu aliletwa duniani na Baba yake kwa kusudi maalum.
    Aya: Yohana 8:42 - "Yesu akawaambia, Kama Mungu alikuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa sababu mimi nilitoka kwa Mungu."
Hongera zako Kwa kuwa na Mungu
1) Alikaa tumboni Kwa mama yake miezi 9 so Mungu wako ana mama yake

2)Ana wadogo zake hapa Duniani wa kuzaliwa nae tumbo Moja

3) Alijinyea na kujikojolea alipokuwa mtoto mchanga

4) Alivalishwa nepi na mama yake

5) Alikuwa anakula chakula alafu anaenda chooni kunya

6) Alicheza kombolela na watoto wenzake katika mitaa ya Galilaya

7) Alikuwa fundi seremala akichonga vitanda na makabati Ili ajipatie ridhiki yake

8) Wakati wewe ni Mungu wako Kuna wengine ni mjomba wao maana dada zake walizaa watoto


Ila tambua kuwa sisi waislam na Yesu Mungu wetu ni mmoja na ndio maana hata stail zetu za kumuabudu Mungu wetu zinafanana

Mathayo 26:39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Alafu na andiko hili nakupa kama zawadi Ili ujijue kuwa wewe haufati mafundisho ya Yesu ila unafuata uongo wa wazungu

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
 
Waislam tafitini Jambo hili litawasaidia pia...Achaneni na Biblia....Masheikh wenu wanapokuwa wanahitimu masomo Yao hula viapo tena wakati mwengine mbele ya viumbe wasio binadamu.....Jambo ni hili ""Masheikh wenu hula Yamini Kwa kiapo kutunza Siri za uislam"""

*Tafitini kwamba Siri hizo ni zipi???

**Zimefichwa Kwa ajili ya kina Nani???
(1) Mlio ndani??
Kama ni nyie Kwa nini??? Lengo gani??
Faida ipi??
(2)Au makafiri kama Mimi ambae kamwe sitoukubali uislam???
Kama ni Sisi!!! Kwa faida gani??

****Je!! Kuna Jambo limefichwa nyuma ya pazia???

****Kuna hasara gani Katika kuujua hio ukweli????

****Kuna reward gani Kwa Masheikh wenu kufa na hizo Siri????
Mkuu kwenye hii hoja yako nina swali.

Kwanini kauli hizi zipo pande zote yani utasikia Masheikh wamekula kiapo wasiseme ukweli. Hali kadhalika Mapadri wamekula kiapo wasiseme ukweli.

Unatoa tamko gani ?
 
Kwanini unaswma ni mpango wa shetani? Shetani ana nguvu kubwa kiasi hicho?
Mpango wa shetani ni kuwarubuni binadamu waende naye motoni. Ana nguvu sana ukilinganisha na uwezo wa binadamu. We angalia mnavyopelekeshwa na majini (minions) mnayoyafuga hadi mnacomply kuishi yanavyotaka. Sisi hao wala hatuwaogopi maana tunaye Yesu.
 
Mpango wa shetani ni kuwarubuni binadamu waende naye motoni. Ana nguvu sana ukilinganisha na uwezo wa binadamu. We angalia mnavyopelekeshwa na majini (minions) mnayoyafuga hadi mnacomply kuishi yanavyotaka. Sisi hao wala hatuwaogopi maana tunaye Yesu.
Umetumia neno kama "mnavyopelekeshwa". Nikiweka kumbukumbu sawa sidhani kama nimefafanua mimi nipo upande gani zaidi ya kuuliza swali.

Huyu shetani hii nguvu ya kufanya hivyo kapewa na nani? Na kwanini?
 
Kuna mengi yanayosemwa kuhusu Quran ambayo ni ya uongo. Habari ya sijui quran kuwa iliteremshwa toka mbinguni, nayo ni uwongo. Kwa sababu Mohammad anasema aliambiwa achukue kalamu aandike, naye akasema kuwa ataandikaje kwa kuwa hajui kuandika (Mohammad hakujua kusoma wala kuandika). Katafute historia ya uandikaji wa Quran. Mohammad alienda kusimulia yale aliyodai kuwa aliambiwa, na mtu mwingine ndiye aliyeandika. Lakini mpaka leo waislam wengi wamedanganywa kuwa eti Qurani ilishushwa!!

Kwenye imani, huwa kunahitaji umakini sana, maana hata shetani hutumia yale unayoyaamini ili kukuangamiza. Kumbuka hata Yesu alipofunga siku 40 akiwa jangwani, shetani alienda kumjaribu ili amwangushe. Na katika kutaka kumwangusha alitumia maneno ya kwenye biblia, akamwambia, "jirushe mpaka chini, maana imeandikwa kuwa malaika wa mbinguni watakudaka". Yesu akamjibu kuwa imeandikwa, usimjaribu Bwana Mungu wako. Hivyo shetani hutumia maneno ya Mungu ili kumhadaa mwanadamu. Quran imecopy na kuyachukua machache kutoka kwenye biblia, kisha ikaongeza mengine yaliyo kinyume na maagizo ya Mungu.

Kuna aya katika Quran zinazoelezea sifa za Allah, ambazo kwa kaduri ya biblia ni sifa za shetani/ibilisi. Swali la kujiuliza, je Muhammad alikutana na malaika Jibril kama inavyosemwa, au alikutana na shetani aliyejiita kuwa ni malaika?

Yesu, hakusema kuwa eti kuna nabii mwingine atakayekuja, bali alisema kuwa Mungu aliwatuma manabii, wanadamu hawakuwasilikiliza, baadaye akamtuma mwana wake, wanadamu hawakumsikiliza, wakamwua, na kisha aliwauliza, mnadhani Mungu atawatenda nini watu hao? Yesu alipokuwa anapaa mbinguni aliwaambia mitume kuwa anawaletea mfariji atakayewakumbusha yote aliyowafundisha, kisha akawavuvia akawaambia, pokeeni Roho Mtakatifu. Kwa hiyo mfariji na mwenye kuwakumbusha mitume wake, yale aliyowafundisha alimtaja wazi kuwa ni Roho Mtakatifu, hakuna habari ya Ahmad.

Kosa la Lucifer ilikuwa ni kutaka kuwa kama Mungu, yaani aabudiwe, asifiwe na kuwa na wafuasi watakaomfanyia ibada, na kumjengea nyumba za kumwabudu, kama anavyofanyiwa Mungu. Mungu akamtupa Duniani, na Duniani ndiko aliko na ufalme wake. Biblia inasema mfalme wa Ulimwengu ni shetani. Quran inasema Allah ni mfalme wa Ulimwengu!!

Tuombe sana neema ya kumjua Mungu wa kweli. Tutambue kuwa shetani, ufalme wake na mawakala wake, wapo Duniani wakiimarisha ufalme wake kwa mafundisho ya uwongo, mafundisho yaliyo kinyume na mafundisho na amri kuu ya Mungu, ambayo ni UPENDO.

Hakika unesema yote. Upendo, ni amri kuu mpya ambayo inapingwa kabisa na waislam. Wao wanaamini revenge , na fake until you can make it. Ukiona mwislam anakuchekea be careful, probably anakulia timing, au kuna wale (nina marafiki kadhaa waislam) hawajui vizuri dini yao so naturally wanapractice upendo kwakuwa hawajui dini yao inataka nini kwneye hilo.
 
Kwenye ukristo hakuna mafundisho ya kiislam na biblia haitambui utume wa mohamad zaidi ya kumuona ni nabii wa uongo anayeupotosha ulimwengu. Ni pro ant christ
 
Hakika unesema yote. Upendo, ni amri kuu mpya ambayo inapingwa kabisa na waislam. Wao wanaamini revenge , na fake until you can make it. Ukiona mwislam anakuchekea be careful, probably anakulia timing, au kuna wale (nina marafiki kadhaa waislam) hawajui vizuri dini yao so naturally wanapractice upendo kwakuwa hawajui dini yao inataka nini kwneye hilo.
Mkuu juzi niliuliza hili swali ngoja ni quote
Swali nje ya mada.
Kila pande inavutia kwake kwa kumsikitikia mwenzake na kumuona kapotea na kumuombea kwa Muumba amsaidie afahamu ukweli.

Je Lengo la Muumba kuruhusu uwepo wa dini tofauti ambazo watu wa miaka ya mbele wanakuja kupata mkanganyiko ni nini?
cc DR Mambo Jambo
Swali langu umejibu hoja ya bams kwakukubaliana naye, lakini katika paragragh yake ya kwanza mbona kapotosha na wewe umekubaliana naye

Je hapa tatizo lipo wapi yeye kukupotosha? , wewe kukubali kupotoshwa?, The Almighty kuruhusu zoezi zima?
 
Katika historia, kumekuwa na mijadala kuhusu kama maandiko ya zamani yalitabiri ujio wa nabii wa mwisho. Watu wengi wamechunguza vitabu vya kale wakitafuta dalili zinazoelezea mtu atakayekuja na mwongozo wa kiroho kwa mataifa yote. Katika makala hii, tutaangalia aya mbalimbali kutoka Injili zinazoonyesha utabiri wa ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

1.Kumbukumbu la  Torati 18:18 -  Nabii  kama Musa

"Nitawainulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)

Katika aya hii, Mungu anamwambia Musa kwamba nabii mwingine kama yeye atainuliwa kwa watu. Wanazuoni wanaeleza kuwa nabii huyu:
Atakuwa kutoka kwa ndugu wa Waisraeli → Ikiwa Waisraeli wanahusiana na Isaka, basi ndugu zao wa karibu ni kizazi cha Ismaili, ambacho kilizaa Waarabu.

Atakuwa kama Musa → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na Musa wote walikuwa manabii waliopokea sheria mpya na waliongoza jamii zao kwa mwongozo wa Mungu.

Atakuwa na maneno ya Mungu kinywani mwake → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alipokea Qur’an kwa ufunuo wa Jibril, kama Musa alivyopewa Taurati.


2.Isaya 42:1-13 -  Nabii  kutoka Kedar

Katika sura hii ya Isaya, kuna maelezo kuhusu mtumishi wa Mungu ambaye atakuwa nuru kwa mataifa yote:

Isaya 42:1 – “Tazama, mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake, naye atawatolea mataifa hukumu.”
Huyu ni mtu ambaye Mungu amemchagua kwa kazi maalum.

Ataleta hukumu kwa mataifa yote, akimaanisha atakuwa na ujumbe wa kimataifa.


Isaya 42:11 – “Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao, na vijiji anavyokaa Kedari; na wakaao katika miamba na waimbe, wapige kelele kutoka vilele vya milima.”

Kedar alikuwa mtoto wa Ismaili na kizazi chake waliishi Arabia, ambapo Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alitokea.


3.  Isaya 21:13-17 - Ujumbe wa Arabia na Parani

Katika sura hii ya Isaya, kuna utabiri wa matukio yatakayotokea katika Arabia:

Isaya 21:13 – "Ufunuo juu ya Arabia. Mtapiga kambi nyikani, enyi watu wa Dedani."

Hii inaonyesha kuwa Arabia ni eneo la tukio kubwa la kiroho.


Isaya 21:14 – “Mleteeni mwenye kiu maji, enyi wenyeji wa Tema, mleteeni mkimbizi chakula chake.”

Tema ni sehemu ya Hijaz, ambako mji wa Madina upo.

Hii inahusiana na jinsi wakazi wa Madina walivyompokea Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na kumpa hifadhi.


4.  Yohana 14:16, 16:7-14 - Msaidizi (Parakletos)  na Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Yesu alisema:

Yohana 14:16 – “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele.” Yohana 16:7 – “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda, nitamtuma kwenu.”

Msaidizi huyu atafundisha ukweli wote (Yohana 16:13) → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikuja na Qur’an kama mwongozo wa mwisho.

Neno Parakletos (Παράκλητος) linaweza kuwa Periklytos, ambalo linamaanisha "Aliyesifiwa"
(kwa Kiarabu, Ahmad – jina jingine la Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)).


Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Katika Qur’an, Mtume Isa(amani iwe juu yake) alitabiri kuja kwa mtume baada yake aitwaye Ahmad:

Surah As-Saff 61:6 "Na (wakumbuke) Isa bin Maryamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nikiwahakikishia yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na nikitoa habari njema ya (ujio wa) Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad."

Ahmad ni jina lingine la Muhammad.

Yesu anatabiri nabii anayekuja baada yake, ambaye atakuwa na ujumbe wa Mungu.


5.Ufunuo 12:5 & 19:15 - Fimbo ya Chuma

Ufunuo 19:15 – "Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili aweke mataifa chini, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma."

Hii inahusiana na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye atatawala kwa haki na nguvu za Mungu, na Qur’an inamtaja kama mtawala wa haki.

Hitimisho
Biblia ina maandiko ambayo, kwa muktadha wa tafsiri, yanaonyesha wazi dalili kuhusu ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Aya kutoka Kumbukumbu la Torati, Isaya, Yohana, na Ufunuo zinaweza kueleweka kama utabiri wa ujio wa Muhammad, hasa kwa vile anapatikana katika maeneo ya Arabia, anahusiana na Kedar, na anaitwa Ahmad, jina lingine la Muhammad.








 
Kwenye ukristo hakuna mafundisho ya kiislam na biblia haitambui utume wa mohamad zaidi ya kumuona ni nabii wa uongo anayeupotosha ulimwengu. Ni pro ant christ
Fundisho la kiislam katika Bibilia hili hapa

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma

Wewe siku utakapo liamini hili andiko na kuyakubali haya ambayo Yesu amekuambia uyamini kuwa Mungu ni mmoja na yeye Yesu ametumwa na huyo Mungu mmoja
Na wewe utakuwa Muislam kama Yesu
 
Back
Top Bottom