Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Kiukweli tu nikwambie tu hadithi ya kwenye biblia ya mtu aliyezaliwa na bikra kisha baadae kusulubiwa kisha kufufuka si za kweli.
Ukweli ni kwamba huyo mtu aliyezaliwa na bikra hakusulubiwa bali alipazwa na Allah mpaka mbinguni ili kuokolewa dhidi ya wayahudi na wala hakuwa mungu.
Nonsense
 
Alah anawahidi wafuasi wake kwamba atawapa
Katika historia, kumekuwa na mijadala kuhusu kama maandiko ya zamani yalitabiri ujio wa nabii wa mwisho. Watu wengi wamechunguza vitabu vya kale wakitafuta dalili zinazoelezea mtu atakayekuja na mwongozo wa kiroho kwa mataifa yote. Katika makala hii, tutaangalia aya mbalimbali kutoka Injili zinazoonyesha utabiri wa ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

1.Kumbukumbu la  Torati 18:18 -  Nabii  kama Musa

"Nitawainulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)

Katika aya hii, Mungu anamwambia Musa kwamba nabii mwingine kama yeye atainuliwa kwa watu. Wanazuoni wanaeleza kuwa nabii huyu:
Atakuwa kutoka kwa ndugu wa Waisraeli → Ikiwa Waisraeli wanahusiana na Isaka, basi ndugu zao wa karibu ni kizazi cha Ismaili, ambacho kilizaa Waarabu.

Atakuwa kama Musa → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na Musa wote walikuwa manabii waliopokea sheria mpya na waliongoza jamii zao kwa mwongozo wa Mungu.

Atakuwa na maneno ya Mungu kinywani mwake → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alipokea Qur’an kwa ufunuo wa Jibril, kama Musa alivyopewa Taurati.


2.Isaya 42:1-13 -  Nabii  kutoka Kedar

Katika sura hii ya Isaya, kuna maelezo kuhusu mtumishi wa Mungu ambaye atakuwa nuru kwa mataifa yote:

Isaya 42:1 – “Tazama, mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake, naye atawatolea mataifa hukumu.”
Huyu ni mtu ambaye Mungu amemchagua kwa kazi maalum.

Ataleta hukumu kwa mataifa yote, akimaanisha atakuwa na ujumbe wa kimataifa.


Isaya 42:11 – “Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao, na vijiji anavyokaa Kedari; na wakaao katika miamba na waimbe, wapige kelele kutoka vilele vya milima.”

Kedar alikuwa mtoto wa Ismaili na kizazi chake waliishi Arabia, ambapo Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alitokea.


3.  Isaya 21:13-17 - Ujumbe wa Arabia na Parani

Katika sura hii ya Isaya, kuna utabiri wa matukio yatakayotokea katika Arabia:

Isaya 21:13 – "Ufunuo juu ya Arabia. Mtapiga kambi nyikani, enyi watu wa Dedani."

Hii inaonyesha kuwa Arabia ni eneo la tukio kubwa la kiroho.


Isaya 21:14 – “Mleteeni mwenye kiu maji, enyi wenyeji wa Tema, mleteeni mkimbizi chakula chake.”

Tema ni sehemu ya Hijaz, ambako mji wa Madina upo.

Hii inahusiana na jinsi wakazi wa Madina walivyompokea Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na kumpa hifadhi.


4.  Yohana 14:16, 16:7-14 - Msaidizi (Parakletos)  na Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Yesu alisema:

Yohana 14:16 – “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi milele.” Yohana 16:7 – “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda, nitamtuma kwenu.”

Msaidizi huyu atafundisha ukweli wote (Yohana 16:13) → Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikuja na Qur’an kama mwongozo wa mwisho.

Neno Parakletos (Παράκλητος) linaweza kuwa Periklytos, ambalo linamaanisha "Aliyesifiwa"
(kwa Kiarabu, Ahmad – jina jingine la Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)).


Uthibitisho wa Ahmad Kwenye Qur’an

Katika Qur’an, Mtume Isa(amani iwe juu yake) alitabiri kuja kwa mtume baada yake aitwaye Ahmad:

Surah As-Saff 61:6 "Na (wakumbuke) Isa bin Maryamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nikiwahakikishia yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na nikitoa habari njema ya (ujio wa) Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad."

Ahmad ni jina lingine la Muhammad.

Yesu anatabiri nabii anayekuja baada yake, ambaye atakuwa na ujumbe wa Mungu.


5.Ufunuo 12:5 & 19:15 - Fimbo ya Chuma

Ufunuo 19:15 – "Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili aweke mataifa chini, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma."

Hii inahusiana na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye atatawala kwa haki na nguvu za Mungu, na Qur’an inamtaja kama mtawala wa haki.

Hitimisho
Biblia ina maandiko ambayo, kwa muktadha wa tafsiri, yanaonyesha wazi dalili kuhusu ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Aya kutoka Kumbukumbu la Torati, Isaya, Yohana, na Ufunuo zinaweza kueleweka kama utabiri wa ujio wa Muhammad, hasa kwa vile anapatikana katika maeneo ya Arabia, anahusiana na Kedar, na anaitwa Ahmad, jina lingine la Muhammad.
Alah anawaahidi wafuasi wake kama wewe kwamba atawapa wanawake 72 na pombe..Imagine watu 10 ×70=700.sasa hiyo mbigu yenu si itakuwa ni virugu tu?Alah is fake na ni mfanyakazi wa shetani.ukitaka kujua mtu wa kuabudiwa ni Yesu tu.taja Jina hilo kwenywe tatizo lolote na tatizo linaisha.
 
Mathayo 20:23
"Akawaambia, Hakika mtakunywa kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume, na mkono wangu wa kushoto, si langu kuwapa; bali watapewa waliowekewa na Baba yangu."

Yohana 5:30
"Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo, ndiyo nihukumu; na hukumu yangu ni ya haki; kwa sababu sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka."

Mwenyewe hapo amekiri mambo asiyoyaweza
Wapi hapo kakiri mambo asiyoyaweza?usisome Biblia kama gazette au kuran
 
Sawa nimekuelewa mkuu.
Kwa hiyo inatakiwa nikubaliane nalo tu hata kama najua ni uongo.
Kati yenu hapo Hakuna anaejua chochote, bali mnaamini tu, tofautisha kujua na kuamini, wewe hapo haujui kama ni uongo au nikweli, bali unaamini ni uongo, hata mwenzio anavyosema yesu atamfufua Mohammad, hasemi kanakwamba anajua bali anaamini hivyo.
 
Muhamad alikuwa mhuni tu ,alikuwa anafanya biashara, baada ya mtaji lumuishia kwa kuhonga vitotozi akaja na plan B, ya kujifanya mhubiri . Ila ukweli kwa kiswahili cha kileo tunasema alikuwa amefuria
Usipoleta ushahidi wa maana basi wewe ndio muhuni
 
Kati yenu hapo Hakuna anaejua chochote, bali mnaamini tu, tofautisha kujua na kuamini, wewe hapo haujui kama ni uongo au nikweli, bali unaamini ni uongo, hata mwenzio anavyosema yesu atamfufua Mohammad, hasemi kanakwamba anajua bali anaamini hivyo.
Mimi najua na naamini
 
Waislamu kazi Yao ni kupigania dini tu😂 hapo anatetewa mtume,unatetewa uislam, wakati mtume aliwaandikia waislam kwamba Yesu ni roho wa MUNGU.

Hadithi ya mtume BUKHARI 3435 Kuna verse huwa hawaisomi. Hawa wafia dini wa kiislamu ni vichaa sana.
Hadithi za Mtume Ziliandikwa Na Mtume 🤔🤔🤔👋
 
Back
Top Bottom