Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Je, Injili Ilitabiri Ujio wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)?

Ukichaa siyo tusi. Waislam wengi ni vichaa Kama wewe😂 wanasema mbinguni Kuna kusenyentana😂😂 Mara ooo mbinguni lugha inayozungumzwa ni kiarabu😂😂😂 mmeshazoea porojo tu.
Sawa lakini ushahidi uko wapi
 
Kwanini mnapata shida? Kwenye imani ya kikikristo unatakiwa kujua na kutofautisha kati ya haya makundi, Yaani
Nabii
Masihi
Mitume.

Kwenye biblia takatifu manabii wote walikuja kwaajili ya utabiri wa ujio wa masihi yaani Yesu kristo,

Pia kwenye biblia takatifu mitume ni wale wanafunzi wa Yesu kristo 12 ambao waliwakilisha idadi ya makabila 12 ya wayahudi.

Nabii wa mwisho kwenye biblia takatifu ni Yohana mbatizaji ambae alipata bahati ya kipekee ya kuuona utabiri wake na ndiye aliembatiza yule aliemtabiri kuwa atakuja, Yaani "Masihi".

Kwahiyo kusema kuwa Injili ilitabiri ujio wa Muhamad huko ni kuikosea heshima imani ya kikristo. Utabiri uliisha kwa utabiri wa Yohana mbatizaji na baada ya Yohana alikuja kristo yaani masihi Yesu kristo.

Baada ya Yesu kristo, wakristo tuliletewa Roho mtakatifu, Note: Roho mtakatifu hakutabiriwa bali aliletwa na mwenyezi Mungu baada ya kuondoka kwa Masihi.

Kuhusu siku ya mwisho au kiama, hakuna utabiri kwenye siku ya mwisho kwa maana tumeambiwa na masihi yaani Yesu kristo kuwa twapaswa kujiandaa maana hatujui siku wala saa hivyo tuenende kwenye utakatifu kwa kutendeana yaliyo mema na kumuabudu bwana Mungu wetu kwa roho na kweli.

Hakuna utabiri wowote kwenye ukristo baada ya utabiri wa Yohana mbatizaji ambao ulitabiri ujio wa masihi, baada ya kuondoka Yesu kristo tulibakiwa na mitume na roho mtakatifu ambae kwa sasa aliebakia ni roho mtakatifu pekee ambae hatuwezi kumuona kwa macho ila tunaweza kumhisi yu ndani yetu kwakuwa yeye ndio mlinzi na kiongozi wetu.

Ukiujua ukristo na mpangilio wake kuanzia Uungu, malaika,manabii,mitume,masihi na roho mtakatifu kamwe hutopata shida kubisha na watu either wawe ni wakristo wenzako au hata hawa wa upande mwingine.
 
Katika Qur’an tumeambiwa tufuate mila ya Ibrahim عَلَیهِ‌السَّلام.
"...(fuateni) mila ya baba yenu Ibrahim..." (Qur'an 22:78)
Na katika mila hizo ni kutahiriwa kama ambavyo tumeamrishwa sisi.
Mtume ﷺ alisema:
"Fitrat tano ni hizi: Kutahiriwa, kunyoa nywele za sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha, na kunyoa nywele za kwapani." (Sahih al-Bukhari na Muslim)
Chief unaamini Hadith za kutungwa? Unajua Bukhari hakuwahi kumuona Mohamed,hakuishi Saudi Arabia. Alikuwa mtu wa Uzbekistan huko,km zaidi ya 1000 kutoka Mecca.

Hizi Hadith zimeandikwa miaka Zaidi ya 200 baada ya Mohamed kufa, kali kuliko ni hadithi za Bukhari ni karibia miaka 400 baadaye. Wewe leo unaleta hapa kama authentic source ya maneno ya Allah 🤔🤔!!!
 
Hivyo ni vitabu vya Allah alivyoviteremsha kwa wayahudi kama yeye mwenyewe anavyokiri kwenye Qur’an
نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾
3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na Akateremsha Tawraat na Injiyl.(Qur’an 3:3)

وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na Tukamfuatishia katika njia yao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl yenye mwongozo na nuru ndani yake, inasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na Tumeifanya mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.(Qur'an 5:46)

حَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾
163. Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw,[55] (kizazi chake) na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr.(Qur’an 4:163)
Injeel ni nini? Pia injeel iko wapi?
 
Mwenyezi Mungu hana roho.
Labda unaweza kunielezea hiyo roho ipoje?
Quran 3:45-47 kasome hii sura kwa kiarabu,sio tafsiri za kiswahili/English ambazo neno Gabriel limepachikwa. Kisha uje hapa utwambia Ruh maana yake nini?
 
MAANDIKO SAHIHI
1. Imani kwa Mungu Mmoja (Tawhid) – Yesu alifundisha kuwa Mungu ni Mmoja, jambo linalothibitishwa katika Biblia (Marko 12:29): "Sikia, Ee Israeli; Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja." Hii inafanana na Qur’an (112:1): "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee."


2. Yesu Alikuwa Nabii wa Mungu – Yesu (Isa, amani iwe juu yake) alikuwa Mtume wa Mungu, si Mungu mwenyewe. Qur'an (5:75) inasema: "Masihi mwana wa Mariamu si chochote ila ni Mtume; wamekwisha pita Mitume kabla yake..."


3. Sheria ya Musa (Taurati) Ilikuwa Sahihi – Yesu alisisitiza kufuata Taurati (Mathayo 5:17): "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la! Sikuja kutangua, bali kutimiliza."


4. Adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa Wakosefu – Yesu alifundisha kuwa kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake, jambo linalolingana na Uislamu (Mathayo 12:36): "Basi, nawaambia, kila neno lisilo na maana watakalolinena watu, watatoa hesabu yake siku ya hukumu."


5. Unyenyekevu na Ibada kwa Mungu Pekee – Yesu alisali kwa Mungu na kufundisha wengine kumsujudia Mungu peke yake (Luka 6:12): "Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko anasali kwa Mungu."


6. Kufufuliwa kwa Wafu na Siku ya Mwisho – Yesu alifundisha kuhusu Siku ya Kiyama na malipo ya waumini na makafiri, jambo linalothibitishwa pia na Uislamu (Yohana 5:28-29): "Msistaajabu kwa hili; kwa kuwa saa inakuja ambayo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake, nao watatoka..."

MAANDIKO YALIYOPOTOSHWA
1. Dhana ya Upatanisho wa Dhambi (Atonement) – Ukristo unafundisha kuwa Yesu alisulubiwa ili kufuta dhambi za wanadamu. Uislamu unapinga dhana hii na kusisitiza kuwa kila mtu atawajibika kwa dhambi zake (Qur'an 53:38-39): "Kwamba hapana mbebaji wa mzigo atakayebeba mzigo wa mwengine."


2. Yesu ni Mungu (Uungu wa Kristo) – Wakristo wanadai kuwa Yesu ni Mungu au sehemu ya Mungu, jambo ambalo linapingwa na Uislamu. Qur'an (5:116) inasema kuwa Yesu atakataa kudai uungu: "Sikuwambia lolote ila yale uliyoniamrisha..."


3. Dhana ya Roho Mtakatifu Kama Sehemu ya Mungu – Wakristo wanaamini katika Utatu Mtakatifu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu). Qur'an (4:171) inasema: "Msiseme utatu, acheni! Itakuwa bora kwenu. Mwenyezi Mungu ni Mungu Mmoja tu."


4. Mtazamo wa Dhambi ya Asili – Ukristo unafundisha kuwa kila mtu amerithi dhambi ya Adamu na Hawa, jambo ambalo Uislamu unalipinga. Qur'an (2:286) inasema: "Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake..."


5. Kusema Yesu ni Mwana wa Mungu kwa Maana ya Kiungu – Wakristo wanamuita Yesu Mwana wa Mungu kwa maana ya kiungu, lakini Uislamu unasema kuwa Allah hana mwana (Qur'an 19:35): "Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Ametakasika!"

Hayo ni baadhi tu!
Uislam ni mpinga kristo halisi kwa sababu unapingana na mafundisho ya Yesu. Hapa umesahau hoja moja ya muhimu sana, Yesu alikuwa anamwita Mungu wake baba. Allah hana mwana,huyu Allah sio Mungu wala baba yake Yesu .
 
Injili ya asili iliyoteremshwa kwa Nabii Isa (عَلَیهِ‌السَّلام) haipo tena katika umbo lake la awali.Maandiko yaliyopo sasa yamepotoshwa na kubadilishwa na wanadamu kwa nyakati tofauti.
Aidha Qur’an ni kitabu kingine cha Allah kama ilivyokuwa Injil asilia.
Leta hapa aya kutoka kwenye Quran inayosema injeel imepotoshwa? Umekaririshwa uongo na upotoshaji tu,hakuna mahali kitabu chenu kinasema enjeel imepotoshwa,pili injeel waislam hamuijui japo mnasema imepotoshwa.

Imepotoshwa wakati hamuijui wala hamjawahi kuiona!! Imani yenu imesimama kwenye msingi dhaifu sana na ndiyo maana mnajitafuta kwenye kitabu cha wakristo.
 
Qur’an imesema ni roho kutoka kwake na sio roho yake halafu kwa nini umeishia njia na hujataka kumalizia umeishia "wala msiseme..." halafu hukumalizia.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّـهُ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖسُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٧١﴾
171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msimzungumzie Allaah isipokuwa ukweli. Hakika Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam ni Rasuli wa Allaah na ni Neno Lake (la Kun!) Alompelekea Maryam na Ruwh (roho Aliyoumba kwa amrisho) kutoka Kwake. Basi mwaminini Allaah na Rusuli Wake. Wala msiseme: ‘watatu’. Komeni! Ni kheri kwenu. Hakika Allaah ni Mwabudiwa wa haki Mmoja Pekee, Ametakasika na kuwa na mwana![58] Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Na Anatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa wa yote.
(Roho aliyoumba kwa uandishi) Imeongezwa kwa tafsiri ya kiswahili na English 🤔. Kwenye Quran ya kiarabu hakuna hayo maneno.
 
Leta hapa aya kutoka kwenye Quran inayosema injeel imepotoshwa? Umekaririshwa uongo na upotoshaji tu,hakuna mahali kitabu chenu kinasema enjeel imepotoshwa,pili injeel waislam hamuijui japo mnasema imepotoshwa.

Imepotoshwa wakati hamuijui wala hamjawahi kuiona!! Imani yenu imesimama kwenye msingi dhaifu sana na ndiyo maana mnajitafuta kwenye kitabu cha wakristo.
Ndio nimemwambia Imani Yao ni dhaifu sana ,thus why wanalazimisha Yesu ni Isa ,maana wakisema wasimame na Isa wao hakuna atakayewaamini
 
Saa 12:00 jioni haimaanishi kuwa Yesu alikufa muda huo, bali ni muda ambao giza lilianza kutanda duniani, kama inavyosemwa katika Mathayo 27:45 na Luka 23:44. Hili giza lilidumu kwa masaa matatu, kutoka saa 12:00 jioni hadi saa 3:00 mchana, na baada ya hapo Yesu akafa
Unazidi kudanganya mkuu ,yaani ameanza kusubishwa saa 3 asubui au saa sita mchana? Na kama alianza kusubishwa saa 3 asubui na kufa saa 9 mchana hiyo saa 12 jioni imehusikaje? Kwa sababu mchana huanzia saa 6 na jioni huanzia saa 10 jioni.
Ama unataka kusema alisulubiwa saa 3 asubui mpaka saa 12 jioni Kisha akafa saa 9 mchana siku hiyo hiyo? Na kama hivi mbona unaleta uongo wa wazi
 
Unazidi kudanganya mkuu ,yaani ameanza kusubishwa saa 3 asubui au saa sita mchana? Na kama alianza kusubishwa saa 3 asubui na kufa saa 9 mchana hiyo saa 12 jioni imehusikaje? Kwa sababu mchana huanzia saa 6 na jioni huanzia saa 10 jioni.
Ama unataka kusema alisulubiwa saa 3 asubui mpaka saa 12 jioni Kisha akafa saa 9 mchana siku hiyo hiyo? Na kama hivi mbona unaleta uongo wa wazi
Nikukosa kwako elimu tu ,sio kosa langu Mzee,

Unaulizia

"Ameanza kusulubishwa saa 3 asubuhi au saa 6 mchana?"


Biblia inaonyesha wazi kwamba Yesu alisulubiwa saa 3 asubuhi (Marko 15:25), na kuanzia saa 6 kulikuwa na giza (Mathayo 27:45).

Saa 6 si muda wa kusulubiwa bali ni muda ambapo giza lilianza kutanda.


"Na kama alianza kusulubiwa saa 3 asubuhi na kufa saa 9 mchana, hiyo saa 12 jioni imehusikaje?"

Saa 12 jioni haijatajwa kama muda wa kusulubiwa au kufa, bali jioni inaanza baada ya saa 9, wakati mwili wa Yesu ulipoandaliwa kwa mazishi (Marko 15:42-43).

Kwa mfumo wa Kiyahudi, jioni huanza baada ya saa 9 na kabla ya machweo (takribani saa 12 kwa saa za Kisasa).


"Ama unataka kusema alisulubiwa saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni, kisha akafa saa 9 mchana siku hiyo hiyo?"


Hapana, Yesu alisulubiwa saa 3 asubuhi, giza likaanza saa 6 mchana, akafa saa 9 alasiri, na jioni mwili wake ukaondolewa msalabani na kuzikwa kabla ya Sabato.


"Na kama hivi mbona unaleta uongo wa wazi?"

Hakuna uongo hapa, bali ni kutoelewa mpangilio wa muda wa Kiyahudi na maandiko yanavyotaja muda wa matukio.

NAMALIZIA KWA KUSISITIZA SITEGEMEI UJE TENA ,LABDA KAMA UNALETA UBISHI ,MAANA MUDY ALISHAWADANGANYENI NA MKAAMINI

Yesu alisulubiwa saa 3 asubuhi (Marko 15:25).

Giza lilianza saa 6 mchana hadi saa 9 alasiri (Mathayo 27:45).

Yesu alikata roho saa 9 alasiri (Luka 23:46).

Mwili wake uliombwa na kuzikwa jioni kabla ya Sabato (Marko 15:42-43).

Kwa hiyo, hoja inayodai kuwa kuna mkanganyiko wa muda wa kusulubiwa kwa Yesu ni kutoelewa mfumo wa Kiyahudi wa kuhesabu saa na uhusiano kati ya matukio yaliyotokea.
 
Yesu wa Kwenye Quran Sio Yesu aliesulubiwa na Ponsyo Pilato Mrumi....Huyu Mnamjua nyie na Mtume Wenu alikuja 500+ baada ya Yesu Kufa na Kufufuka...Na akaja anataka tumwamini yeye ambaye ajawai mwona wala kukaa na kumsikiliza mmoja alieishi na kunsikiliza Yesu wa kweli
Mkuu yesu mwenyewe hakufa wala hakusulubiwa na yeye alisema kabisa.
Soma YOHANA 7:30
 
UISLAMU NI PROJECT YA UKATOLIKI KUITEKA YERUSALEMU

Wanazuoni wote wanajua hili
 
Nikukosa kwako elimu tu ,sio kosa langu Mzee,

Unaulizia




Biblia inaonyesha wazi kwamba Yesu alisulubiwa saa 3 asubuhi (Marko 15:25), na kuanzia saa 6 kulikuwa na giza (Mathayo 27:45).

Saa 6 si muda wa kusulubiwa bali ni muda ambapo giza lilianza kutanda.




Saa 12 jioni haijatajwa kama muda wa kusulubiwa au kufa, bali jioni inaanza baada ya saa 9, wakati mwili wa Yesu ulipoandaliwa kwa mazishi (Marko 15:42-43).

Kwa mfumo wa Kiyahudi, jioni huanza baada ya saa 9 na kabla ya machweo (takribani saa 12 kwa saa za Kisasa).





Hapana, Yesu alisulubiwa saa 3 asubuhi, giza likaanza saa 6 mchana, akafa saa 9 alasiri, na jioni mwili wake ukaondolewa msalabani na kuzikwa kabla ya Sabato.




Hakuna uongo hapa, bali ni kutoelewa mpangilio wa muda wa Kiyahudi na maandiko yanavyotaja muda wa matukio.

NAMALIZIA KWA KUSISITIZA SITEGEMEI UJE TENA ,LABDA KAMA UNALETA UBISHI ,MAANA MUDY ALISHAWADANGANYENI NA MKAAMINI

Yesu alisulubiwa saa 3 asubuhi (Marko 15:25).

Giza lilianza saa 6 mchana hadi saa 9 alasiri (Mathayo 27:45).

Yesu alikata roho saa 9 alasiri (Luka 23:46).

Mwili wake uliombwa na kuzikwa jioni kabla ya Sabato (Marko 15:42-43).

Kwa hiyo, hoja inayodai kuwa kuna mkanganyiko wa muda wa kusulubiwa kwa Yesu ni kutoelewa mfumo wa Kiyahudi wa kuhesabu saa na uhusiano kati ya matukio yaliyotokea.
Kwamba mda wa sasa tunaoutumia ni tofauti na wakiyahudi
 
Mkuu yesu mwenyewe hakufa wala hakusulubiwa na yeye alisema kabisa.
Soma YOHANA 7:30
USISOME biblia kama Quran au hadithi

Yohana 7:30 inasema:
"Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyemshika mkono, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado."

Aya hii inamaanisha kuwa wakati huo Yesu alikuwa bado hajafika kwenye muda wake wa kusulubiwa, lakini haimaanishi kuwa hakusulubiwa kabisa. Katika mafundisho ya Biblia, kuna nyakati ambazo watu walitaka kumkamata Yesu lakini hawakuweza kwa sababu muda uliopangwa na Mungu haukuwa umefika.

Hata hivyo, maandiko yanaonyesha wazi kuwa baadaye alikamatwa, akahukumiwa, na kusulubiwa. Kwa mfano:

1. Mathayo 27:35 – "Wakam-sulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura."


2. Marko 15:25 – "Na ilikuwa saa tatu walipomsulubisha."


3. Luka 23:46 – "Yesu akapaza sauti yake, akasema, 'Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.' Akiisha kusema hayo, akakata roho."


4. Yohana 19:30 – "Basi Yesu alipokwisha kuupokea ule siki, akasema, ‘Imekwisha.’ Akainama kichwa chake, akatoa roho."


Aya hizi zote zinathibitisha kuwa Yesu alisulubiwa na akafa. Kwa hiyo, Yohana 7:30 haipingani na kusulubiwa kwa Yesu, bali inaonyesha kuwa wakati huo hakuwa bado amekamatwa kwa sababu muda wa
ke haukuwa umefika.
 
Back
Top Bottom