Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa?

Siku mtakayotuonesha MAZIWA NA ASALI walioahidiwa waisrael hapo jangwani Middle East ndipo tutaamini hilo ndilo lile Taifa lao la ahadi.
Tukiweka facts na points kihistoria hao wazungu wenu pamoja na hao walowezi wa kipalestina hiyo ardhi hawana uhalali nayo.

Wote wezi ndiomaana hawataacha kutwangana mpaka mmiliki halali apatikane ambaye ni Mmisri wa kale(black people) na sio hao walowezi.
 
Hahaa...Taifa Teule, sasa iweje Mungu ambaye hana upendeleo awe na taifa teule tena? Ina maana kuna watu wengine wanakuwa na maana zaidi kwake kisa wamezaliwa sehemu fulani ya Dunia tu na sio matendo yao?
Kuna jambo haliko sawa kwenye hii dunia mkuu...biblia ilikuwa ni andiko la kuipa nguvu za kiutawala Ili watu waiogope. Kwa akili yangu huû ni mpango wa nchi za magharibi na Israeli yenyewe...nachelewa sana kuiamini dunia
 
Kwahiyo Plan ya kwanza ya Mwenyezi Mungu ilikua kuwakomboa waisrael tu!!!sema walivomkataa yesu ndo kukawa na change of plan kuwa hadi na sisi tukombolewe!!So Mungu alikua hajui kuwa hawa waisrael watamkataa yesu na plan yake ya kwanza ingekua kukomboa dunia nzima???@
 
Sahihi kabisa....

Taifa teule la Mungu kwa Sasa ni 'Kanisa la Kristo' ....
 
Mi kwa fikra zangu naona swala la mtoto wa kwanza kupoteza haki yake inatokana na laana ya Abeli aliyeuwawa na Kaini, Yaani Abel damu yake inalia dhidi ya uovu aliofanyiwa na kaka yake ndio maana watoto wa kwanza wanapata shida ya baraka kwa sababu ya laana juu ya Kaini, hivyo Sheria ya asili ikawa inapendelea mdhaliwa mdogo dhidi ya mzaliwa mkubwa, mpaka pale ambapo Yesu Kristo alikuja kama Adamu wa pili na mzaliwa wa kwanza halisi kutoka tumbo la mwanamke kufuta laana hiyo
I stand to be corrected.
 
Mkuu sorry sikuiona post yako mpaka Leo nilipokuwa napitia kusoma Kwa taratibu comments za wadau...
Naweza kusema hivi...YESU au mwana wa MUNGU hakuja kuishi hapa duniani kama watu wengine,,alikuja atolewe sadaka...Kilichohitajiwa kwake Sana ni damu yake.......Rejea """Kwa maana jinsi Hii Mungu aliupenda ulimwengu,,hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminie asipotee Bali awe na uzima WA milele"""
Kwa hio wayahudi kumuua YESU walikuwa wakitekeleza wajibu na jukumu lao la kuwepo....Kwa sababu MUNGU aliupenda ulimwengu na sio Israel pekee... Israel ukiiangalia ndipo maisha yalipoanzia na ndipo maisha yatakapoishia...YESU alitakiwa aje azaliwe,,asalitiwe,,atundikwe msalabani atobolewe kichwani,,mikononi,,mbavuni na miguuni ili lengo la kuipata Ile damu lifikiwe..,Na wakulitekeleza walikuwa wayahudi na walilitekeleza....Na kama unadhani wamekataliwa basi hata mitume 12 walioeneza injili mpaka Greece,, Macedonia na Italy walikuwa wayahudi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…