AFTERMATH
Hivyo basi kwa kuwa Mungu alikwisha dhamiria kurudisha uhusiano na mwanadamu ikabidi ageukie mataifa mengine ambayo ndio yangeendeleza agano lile na hapo ndipo likapatikana agano jipya ambapo neema ya wokovu haukuwa wa Wayahudi pekee sababu walimkataa bali ukawa wa mataifa yote as long as watamfuata Yesu (Yohana 1:11-12) pia Mathayo 21:42-43 ambapo tunaona ufalme wa Mungu umehamishwa kutola Israel kwenda kwa mataifa mengine.
42
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
View attachment 929907
Swali linaibuka je Israel inabakia taifa la Mungu??
NDIO ni kweli Mungu aliendelea na agano na taifa la Israel ila tafsiri ya taifa la israel ni lipi limebadilika kupitia agano jipya.
Warumi 9
6
Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.
7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
Na pia hapa ndipo tunaona kunazaliwa waisraeli wa kimwili (mashariki ya kati) na Israel ya Kiroho (wakristo)
Warumi 2:28-29
28
Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Hivyo kufikia hapa tunaona kuna wayahudi/waisrael aina mbili sasa je ahadi za ISRAEL ya agano la kale anarithi nani za kuwa taifa teule,chaguo la Mungu n.k
Galatia 3
6
Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
.......................................
13
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.Ahadi kwa Abrahamu
..............................
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Kupitia mistari hii tunaona sasa ahadi zote walizopewa Abraham na Israel zinarithiwa rasmi na wale wote wamfuatao Yesu yaani wakristo ambao ndio wale paulo kawaita waisrael wa Kiroho sio kimwili. Hivyo ningependa nichukue fursa hii kutoa msimamo wangu kwamba Israel hii ya kimwili sio taifa la Mungu na halitokaa liwe unless na wao wamfuate Yesu hapo ndipo watakuwa NCHI YA AHADI na taifa la Mungu. Kwa kuhitimisha kupitia agano jipya ambapo sasa wanaomfuata wote Yesu bila kujali ni muisrael au lah ndio wanakuwa TAIFA TEULE ama ISRAEL hivyo baraka zote ahadi zote na unabii wote wa TAIFA LA ISRAEL sio tena wa hii Israel ya yakobo bali ni wote wamfuatao Yesu kristo na hii ni kwa mujibu wa Biblia.
However upande kinzani unasema Israel ya mashariki ya kati bado ni taifa teule kama zamani na hakuna kilichobadilika na wanatumia mstari huu.
Warumi 3:3-4
3
Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?
4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.
Nakubaliana na Mstari huu unaosema Mungu hajawaacha wayahudi licha ya kumkataa lakini bado msimamo uko pale pale kwamba ni lazima wamkiri massiah ndio wawe teule till then hawana tena hadhi ya kuitwa taifa teule kulingana na vifungu nilivyoweka.
View attachment 929908
ANGALIZO
Kumekuwa na interpretation nyingi sana za unabii kuhusu Israel ya kimwili yaani hii ya mashariki ya kati na nina hofu kuwa na wakristo pia wameingia mkenge kama wa wayahudi wa kale kwa kutoelewa unabii na wakatafsiri kwa akili zao kiasi kwamba Yesu alipokuja hawakujua na wakamkataa. kuna wakristo wengi leo wanaamini vita na matetemeko yaliyotabiriwa kwenye ufunuo ni ya kimwili au hekalu litajengwa kimwili hivyo watashituka Yesu amekuja kivingine wao bado wanasubiri vita ya amragedon sijui kujengwa hekalu ilihali hizo mambo zina maana tofauti kabisa ingawa hii ni mada ya siku ingine ila nachoweza hitimisha ni kwamba Biblia imeandikwa kwa codes nyingi hivyo kuitafsiri inahitaji umakini na utulivu sana sio kwenda kichwakichwa mfano inapotabiri kuwepo kwa njaa na kiu haimaanishi njaa ya kimwili ila ukisoma Amos 8:11 utajua njaa inaongelewa ni ya kusikiliza neno la Mungu such phrases mtu akisoma kwenye ufunuo ana conclude kuwa kutakuwa na njaa,vita matetemeko,ukame huu wa kimwili kumbe zina maana nyingine kabisa hivyo nilitaka kuliweka hilo sawa. Kwa kusema hayo naomba kuwasilisha mada kwa ajili ya michango na maoni ya wanajukwaa letu pendwa.
Cc cc
Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI