KENGE 01
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 1,705
- 4,217
Anaandika KENGE,
Katika ulimwengu wa sasa upendo umeingia doa,Upendo hakuna tena,Visa vya ukatili haviishi.Dharau,Majungu na najigambo kuanzia kwa mtu mmoja kwa mwingine(Individually) mpaka mataifa kwa mataifa(internationally).Mataifa yamekosa utu na kuviziana,kupigana na kuuana imekuwa kama tabia sasa
Lakini Nchini JAPAN mambo ni tofauti kidogo.Hawa watu wamekua wakishika vichwa vya habari kwa nyakati tofauti tofauti kwa matendo yao ya UTU na Ubinadamu
Moja ya habari iliovutia wengi mtandaoni ni picha inayowaonesha wafanya kazi(Staff) wa Japan Airline wakiwaomba abiria wao msamaha baada ya ndege kuchelewa kufika uwanjani kutokana na mvua na hali ya hewa kuwa mbaya.
Sio hivyo tu,Kwa wapenzi wa Soka mtakumbuka kombe la dunia lililopigwa nchini Qatar.kuna tukio moja lilifanywa na mashabiki wa japan.Tukio ambalo liliibua hisia za watu wengi na kupelekea Japan kupewa TUZO ya timu yenye nidhamu.
Ilikua ni baada ya ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Germany,baada ya mchezo mashabiki wa Japan walianza kusafisha uwanja kwa kuokota uchafu wa makopo na makaratasi waliotupa wakati wa kuangalia mpira.Huku kauli mbiu yao ikiwa ni 'Triple C' yani Cheer,Chant,Clean wakiwa wanamaanisha tunashangilia,tunafanya lolote lakini mwisho tutaacha tumesafisha
Tofauti na nchi zetu,Africa mchezaji akifunga atatupiwa chupa,mawe na kumulikwa tochi.Na kama ni derby Mfano Simba na Yanga zinacheza pale taifa timu moja ikifungwa shabiki wanang'oa viti yaani ni vurugu mwanzo mwisho.
Matukio ni mengi ya kuelezea UTU wa watu hawa.Miaka ya nyuma walipitisha sheria wafanyakazi wa kucontrol marobot wanatakiwa wawe ni vilema.Ili kusaidia walemavu kwahiyo ukienda viwandani waendesha robot utakuta ni wengi ni walemavu.
Yapo mengi ya kuelezea UTU wa waJAPAN lakini licha ya kuwa nchi zenye acient ya Asia yaani wachina,Wakorea wamekuwa wakitafuta chokochoko na mataifa mengine.Yani kuvimbiana lakini ni tofauti kwa wenzao JAPAN sio watu wa skendo kabisa
JE kwa karne hii JAPANESE ndio watu wanaothamini UTU na UBINADAMU
Nawasilisha
Wako mtiifu