benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Kwanza kabisa nikiri wazi nakubali sana uchapakazi wa Jerry Silaa (Mb) hasa alivyokuwa Wizara ya ardhi. Lakini kama tujuavyo mteuliwa hana maamuzi ni wapi afanye kazi, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu aliamua kumuondoa Wizara ya Ardhi ambapo sote naamini tunakumbuka hekaheka zake akamhamishia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Tangu Jerry apelekwe huku ni kama AMEGOMA au AMEZIRA kufanya kazi, sio tu hajitumi wala kuonesha nia ya kujituma bali pia wenye sekta hiyo, yaani wanahabari WANAMLALAMIKIA.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limeeleza kusikitishwa na mwenendo wa Waziri Jerry Silaa kutohudhuria matukio muhimu ya kihabari anayoalikwa.
1. Jerry Silaa ameshindwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa TEF uliofanyika jijini Dar es Salaam (alitumwa mwakilishi)
2. Jerry Silaa ameshindwa kuhudhuria Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) zilizotolewa Septemba 28, 2024.
3. Jerry Silaa ameshindwa kuhudhuria Kikao Jumuiya wa Maofisa Uhusiano (PRST) jijini Arusha.
4. Jerry Silaa alialikiwa Mbeya kwenye mkutano wa Wahariri hakwenda
Jerry ninayemfahamu ni mchapakazi lakini anavyoonekana ni kama hajapenda kuletwa kwenye Wizara hii kwani hata ukiangalia Kurasa zake za mitandao ya kijamii hakuna lolote linalohusu Wizara yake hii (Mpya) tofauti na alivyokuwa Ardhi, Kutokana na yote haya swali ni JE, JERRY SILAA AMEMGOMEA RAIS SAMIA KUFANYA KAZI WIZARA YA HABARI?
Pia soma
- Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF): Waziri Silaa ameshindwa kuwa karibu na Waandhishi wa Habari