Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Hana baya maana wengi wanafanya maovu wanamsingizia yeye labda tuanze na ww ubaya wa shetani upi embu niambie na mm nijue
Kibiblia Shetani si ndio alimshawishi Hawa pale bustani ya eden ale tunda walilozuiwa na Mungu,wakamtenda Mungu dhambi na kupitia yeye dhambi zikaingia Ulimwenguni,kwahio yeye ndio chanzo cha dhambi zote uzijuazo.
 
Mimi jina langu la Bantu lady linaniwakilisha nilivyo, kuanzia rangi yangu ya chocolate, nina natural hair na umbo ni full bantu. Kwahiyo najiwakilisha mwenyewe.
Duh, kumbe wewe ni mkongwe sana humu ? Itakuwa kuna wakati uli-mute sana. BTW jina linasadifu mkuu.
 
Hii ID ni ya pili sasa kubadili toka nime jiunga JF 2013
nime ichagua hii baada ya kua inspayadi na mtwango mkali wa HIMARS kule Ukraine warusi wameipata pata freshi yake sasa kuna midude hiyo yakuitwa Atacms hii ikianza kazi warusi wataomba hifadhi mozambique maana sio kwa kipondo wanacho pokea kila likitumika dude la HIMARS
 
Yule jamaa anajiita Mafian cartel ningependa kuona comment yake

Sent from my CPH2095 using JamiiForums mobile app
 
Duh, kumbe wewe ni mkongwe sana humu ? Itakuwa kuna wakati uli-mute sana. BTW jina linasadifu mkuu.
Naelekea miaka 10 sasa humu ERoni πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ umeenda fukunyua ya miaka hiyoooo... kuna miaka hapo kati, sikuwa naingia ubusy tu. Za jumapili lakini, mmeamka salama.
 
Naelekea miaka 10 sasa humu ERoni πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ umeenda fukunyua ya miaka hiyoooo... kuna miaka hapo kati, sikuwa naingia ubusy tu. Za jumapili lakini, mmeamka salama.
Hongera, sikujua kama wewe ni mkongwe humu, kumbe "bantu redi" ni mkongwe kabisa, sijafukunyua..huu uzi kuna mtu kaufufua huko🀣🀣 tuko poa kabisa, heri ya jumapili kwako.
 
Hongera, sikujua kama wewe ni mkongwe humu, kumbe "bantu redi" ni mkongwe kabisa, sijafukunyua..huu uzi kuna mtu kaufufua huko🀣🀣 tuko poa kabisa, heri ya jumapili kwako.
Salama kabisa, kumbe siku zote unajua miye mgeni, wa juzijuzi?
Tena nilikuwa 2010, ID nikaisahau ndiyo 2014 nikaweka ambayo, itakuwa rahisi kukumbuka πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Salama kabisa, kumbe siku zote unajua miye mgeni, wa juzijuzi?
Tena nilikuwa 2010, ID nikaisahau ndiyo 2014 nikaweka ambayo, itakuwa rahisi kukumbuka πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
2010 ulikuwa bado binti mbichi sana, hukutakiwa kuwa huku🀣🀣
 
Salama kabisa, kumbe siku zote unajua miye mgeni, wa juzijuzi?
Tena nilikuwa 2010, ID nikaisahau ndiyo 2014 nikaweka ambayo, itakuwa rahisi kukumbuka πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
hivi ukitaka kuweka hako katiki unafanyaje?
 
2010 ulikuwa bado binti mbichi sana, hukutakiwa kuwa huku🀣🀣
Baba yangu ndiyo aliniambia, kwa mara ya kwanza kuhusu JF.
Nikawa nasoma tu, yeye pia huwa anasoma tu, hajajiunga.
Yeah nilikuwa kabinti tu πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…