Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Hana baya maana wengi wanafanya maovu wanamsingizia yeye labda tuanze na ww ubaya wa shetani upi embu niambie na mm nijue
Kibiblia Shetani si ndio alimshawishi Hawa pale bustani ya eden ale tunda walilozuiwa na Mungu,wakamtenda Mungu dhambi na kupitia yeye dhambi zikaingia Ulimwenguni,kwahio yeye ndio chanzo cha dhambi zote uzijuazo.
 
Mimi jina langu la Bantu lady linaniwakilisha nilivyo, kuanzia rangi yangu ya chocolate, nina natural hair na umbo ni full bantu. Kwahiyo najiwakilisha mwenyewe.
Duh, kumbe wewe ni mkongwe sana humu ? Itakuwa kuna wakati uli-mute sana. BTW jina linasadifu mkuu.
 
Hii ID ni ya pili sasa kubadili toka nime jiunga JF 2013
nime ichagua hii baada ya kua inspayadi na mtwango mkali wa HIMARS kule Ukraine warusi wameipata pata freshi yake sasa kuna midude hiyo yakuitwa Atacms hii ikianza kazi warusi wataomba hifadhi mozambique maana sio kwa kipondo wanacho pokea kila likitumika dude la HIMARS
 
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukumbi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
Yule jamaa anajiita Mafian cartel ningependa kuona comment yake

Sent from my CPH2095 using JamiiForums mobile app
 
Duh, kumbe wewe ni mkongwe sana humu ? Itakuwa kuna wakati uli-mute sana. BTW jina linasadifu mkuu.
Naelekea miaka 10 sasa humu ERoni 😄😄😄😄😄 umeenda fukunyua ya miaka hiyoooo... kuna miaka hapo kati, sikuwa naingia ubusy tu. Za jumapili lakini, mmeamka salama.
 
Naelekea miaka 10 sasa humu ERoni 😄😄😄😄😄 umeenda fukunyua ya miaka hiyoooo... kuna miaka hapo kati, sikuwa naingia ubusy tu. Za jumapili lakini, mmeamka salama.
Hongera, sikujua kama wewe ni mkongwe humu, kumbe "bantu redi" ni mkongwe kabisa, sijafukunyua..huu uzi kuna mtu kaufufua huko🤣🤣 tuko poa kabisa, heri ya jumapili kwako.
 
Hongera, sikujua kama wewe ni mkongwe humu, kumbe "bantu redi" ni mkongwe kabisa, sijafukunyua..huu uzi kuna mtu kaufufua huko🤣🤣 tuko poa kabisa, heri ya jumapili kwako.
Salama kabisa, kumbe siku zote unajua miye mgeni, wa juzijuzi?
Tena nilikuwa 2010, ID nikaisahau ndiyo 2014 nikaweka ambayo, itakuwa rahisi kukumbuka 😄😄😄😄😄
 
Salama kabisa, kumbe siku zote unajua miye mgeni, wa juzijuzi?
Tena nilikuwa 2010, ID nikaisahau ndiyo 2014 nikaweka ambayo, itakuwa rahisi kukumbuka 😄😄😄😄😄
2010 ulikuwa bado binti mbichi sana, hukutakiwa kuwa huku🤣🤣
 
2010 ulikuwa bado binti mbichi sana, hukutakiwa kuwa huku🤣🤣
Baba yangu ndiyo aliniambia, kwa mara ya kwanza kuhusu JF.
Nikawa nasoma tu, yeye pia huwa anasoma tu, hajajiunga.
Yeah nilikuwa kabinti tu 😄😄😄😄
 
Back
Top Bottom