Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kwa Muda sasa nimekuwa obsessed na Identity ya mwanadamu haswa ktk self consciousness. Hapo nikaangukua ktk essays za philosopher John Locke ( Locke's general theory of Identity) hapo nikajitambua na kuthamini sana Origin yangu ( Uafrica na Utanzania wangu) ila conflict inayonisumbua kichwa kama wengi wetu ni hali za kisiasa na maendeleo ya uchumi, selfishness, greediness, uonevu, ignorance etc etc. Waafrica wengi hawana huruma na wenziwao, hawana huruma, upendo, ari na nchi au bara lao llililojaaliwa. Wee need to be Loyal na nchi zetu Ukereketwa ukereketwa wajameni! tuijali nchi yetu. LoyalTzCitizen


Ahsante sana Mkuu hili ni moja ya majina ambayo nayapenda hapa ukumbini kwetu.

 
Ha ha ha ha ha 🙂 umenikumbusha njemba mmoja kazini tulikuwa tunamuita kiwavi kwa jinsi alivyokuwa mzima kwenye kula. Yeye aliamini kutupa chakula ni dhambi. Hivyo tulikuwa tukienda kula mahotelini katika safari za kikazi katika mikoa mbali mbali nchini alikuwa akiomba mtu ambaye anaona chakula chake ni kingi hivyo hataweza kumaliza aombe sahani safi na kukiweka pembeni. Yeye atakishughulikia akishamaliza share yake. Wakati mwingi tulikuwa watu wanne au watano. Na kweli alikuwa anavipitia vyote na kisha kushusha kwa chupa mbili za maji baridi. Kuna watu wamejaliwa appetite ya hali ya juu.
Kule Dar (Bongo) maeneo ya temeke kuna jamaa ukifika muda wa maakuli...anaenda kuwaambia wateja kua anaouwezo wa kula jungu zima na ndoo ya maji peke yake.
Sasa mtampinga kua hawezi...weee! Jamaa mwembamba ana katumbo kadogo...kaMa utani mtampuuza!
Anakula jungu na ndoo anamaliza sijui na hiyo ni APPETITE?
WAKTI HUO INAKUA AMEWAAHIDI AKISHINDWA KUFANYA HIVYO ATALIPIA YY...ILA AKIWEZA MNALIPIA NYIE...MATOKEO YAKE MNAKOSA MSOSI.
 
Fundi Mchundo ni fundi mchundo kweli kitaaluma. Kweli kabisa, ingawa nashukuru kuwa kuna baadhi wanaotaka kunipandisha kufikia uhandisi! Huko sikuwezi.

Amandla......

Amandla....sijaijua nini maana yake.
Nmeikuta sana kwenye historia za Sheikh Dr. Mohamed Said za waasisi wa Tanu-.....!
 
N-handsome ---------N my both 1st n surname -------handsome is handsome
 
My real name, ila sijui maana yake. Kwa nini tustume majna yetu jamani? Mnaogopa nini? Ni mtazamo tu, kama nimewakwaza nisameheni.
 
Ahsante kwa nyuzi kuhusu kutafiti maana za majina mbalimbali ukumbini.
Kama wasanii wafokaji "rap musicians" huwa na majina zaidi ya moja kuwasaidia kushamiri mbele ya wapenzi wa muziki wao.
Kwa JF labda ni chanzo kizuri cha majadiliano kuwa Watanzania tuna uhuru wa kutoa hoja zetu bila woga ukizingatia kuna uhuru wa vyombo vya habari, hivyo majina ni just stage names wala si alias za kuficha majina haswa.
Nionavyo majina mengi yanamaana au dhamira ya kuburudisha kama vile wasanii walivyo na stage names zao.
Ahsante.
 
My real name, ila sijui maana yake. Kwa nini tustume majna yetu jamani? Mnaogopa nini? Ni mtazamo tu, kama nimewakwaza nisameheni.

Freedom ya kuchangia itapungua sana...si unajua tena bongo yetu watu wanaweza kupoteza kazi, kuambiwa si Watanzania (kumbuka lile sakata la Jenerali Ulimwengu) na hivyo kufukuzwa nchi na si ajabu hata kupoteza maisha yao. Si unakumbuka yule Kolimba alipotamka hadharani kwamba CCM haina mwelekeo basi wakamkolimba. Inatisha kutumia jina la kweli na sidhani kama jamvi hili lingekuwa na umaarufu kiasi hiki.

 
Amandla....sijaijua nini maana yake.
Nmeikuta sana kwenye historia za Sheikh Dr. Mohamed Said za waasisi wa Tanu-.....!
Amandla is a Xhosa and Zulu word meaning "power". The word was a popular rallying cry in the days of resistance against Apartheid, used by the African National Congress and its allies. The leader of a group would call out "Amandla!" and the crowd would respond with "Awethu" or "Ngawethu!" (To us), completing the South African version of the rallying cry Power to the People!. The word is still associated with struggles against oppression - Wikipedia
 
Ilikuwa ni shule ya sekondari ya girls tukapata wageni kutoka nje ambao tulitakiwa kuwa nao katika michezo mbalimbali na football ikiwemo. Hapo ndipo husninyo lilipozaliwa.
 
langu linamaana nayoijua mimi na nadhani wengi wanachagua majina humu kwa ajili fulani
 
Mhafidhina: Hili ni neno la kiarabu. Linatokana na neno Hafidhi au Hifadhi.

So Mhafidhina maana yake ni mtu anaehifdhi na kuheshimu mambo kwa uhalisia wake. Kwa kiingereza maana yake ni Conservative. Conservatives ni watu ambao wanapenda kusimama katika misomamo yao na sio rahisi kuwayumbisha yumbisha.

Nilichagua jina hili kama chachu ya kuhimiza hifadhi ya maadili kwa viongozi wetu ambao wengi wamesahau ni kukimbilia Wizi, ufisadi, na ubadhirifu wa mali za umma. Uongozi na cheo sio dhamana tena bali ni faraja na utajiri.

So mimi lengo langu ni kusisitiza hifadhi ya Uongozi safi na uwajibikaji wa viongozi pale wanaposhindwa kutekeleza wajibu wao.
 
niligundua kabila langu si maarufu sana na sehemu nyingi nikijitambulisha wengi hawajui ni kabila upande la gani wa tanzania na wengine hudhani labda ni mkimbizi hapo nikaamua kujimbulisha kwa kabila langu (MYAO) na wilaya chimbuko la ukoo wangu (TUNDURU)
 
Kuna mbuga kubwa kiasi pembeni mwa kijiji chetu inaitwa Kakalende na hapo ndio nilikuwa nachungia ng'ombe na kila nikipita pale niendapo likizo naikumbuka safari yangu ya maisha ilivyoanzia mbali.
Tumetokea mbali, wengine kama sio sera sahihi za Baba wa Taifa tusingeenda shule. Huko kijijini kwetu wengi wetu tulianza kuchunga ng'ombe na huendi shule hadi mzee wako aitwe kujieleza kwenye ofisi ya Chama. Ninapochangia katika ukumbi huu, vilevile nakumbuka viongozi wetu wa leo pamoja na ulafi wao na ufisadi, wametokea huku huku Kakalende, na sera sahihi za Mwalimu Nyerere wazichanachana na kuzitupilia mbali!
 
Mwenzetu,nipo nanyi wana- Jf wakati wowote, popote na kwa lolote,Kheri ya mwaka 2011
 
Jina la Funzadume nilijipa mwenyewe baada ya mzee wangu kutunga shairi na kuniomba nimpelekee radio Tanzania kipindi hicho ili lisomwe kipindi cha mashairi, ktk jina lake kule chini aliweka aka Washawasha sasa baada ya hapo na mimi nikatunga shairi na chini ya jina langu nikaweka aka funzadume kama kumlipa mzee wangu ile aka ya washawasha nilipomwonyesha lile shairi mzee alicheka sana ilo jina la funzadume kwa hiyo nilipojifunza kufungua e-mail miaka ya nyuma sana wakati mtandao ndio unapata umaarufu Bongo nilijaribu kwa kutumia e-mail funzadume@yahoo.com

Toka hapo kila mtandao naoingia natumia jina la funzadume, inachekesha na wengine wanaliponda ila kwangu lina historia sana na nyumbani uwa wananiita kifupi funza

kwa hiyo jina ni Funzadume mwana wa Washawasha
 
Back
Top Bottom