CPA- inamaana ni certified public accountant, mi ni muhasibu. Naipenda kazi yangu. Nimetumia jina hilo na cpa, kuonyesha uma kuwa tupo wahasibu tuopinga na hii hari ya baadhi ya wahasibu wenzetu wakishikiriana na mafisadi kuchota mahela ya walipa kodi walio maskin sana hapa nchini, kwa kujinufahisha wenyewe na familia zao. Nawakilisha
jeji ni jina la utani la mtoto wangu wa kwanza, mdogo wake wkt ana
mwaka 1 alikuwa anashindwa kulitamka vizuri jina lake akawa anamwita
jeji, basi ndio limezoeleka kuliko hata jina lake original.
MNAMBOWA,, ni jina la ukoo fulani katika kabila moja huko singida ambalo lina maanisha watoto wa mbwa, nimeamua kutumia jina hilo, kwanza mm ni mmoja ktk uko huo, na pili kwa kuwa hii jamii f. Ni haki yangu kutangaza utamaduni wa mwafrika kutumia majina yenye asili yetu
Haya banaaa! Mrembo sana...kuna wengine kadri wanapoongeza umri ndio wanapendeza zaidi kama Tina Turner na Denzel Washington...naona nawe labda una genes kama zao ππ
Nimejaribu la kwangu likakataa ikaonyesha tayari kuna mtu
nikajaribu mengine matano yote yakakataa la mwisho nakumbuka
ni vuvuzela likakataa ndo nikajaribu GAZETI, Kimsingi sikulikusudia hili jina
hivyo halina maana yoyote zaidi ya utambulisho tu ingawa wengine
wananiita JARIDA.
Avatar yangu ndo ina maana maalum!
Malingumu, msemakweli, mwendapole na songambele ni baadhi tu ya swaga za majina ya kwetu hususani enzi hizo.
Kipindi tuko form 3 mie nilikuwa sipendi kabisa bookkeeping lakini nilikuwa noma katika kukotoa makabati a.k.a a/c sasa katikapast papers kulikuwa na swali la songambele lugaha na mwendapole kapori ndio masela wakiangalia ninapotoka na hilo jina ikabidi wanibatize. Nililikataa sana lakini jamaa wakanipa jina na kuhadi daima utasonga mbele.
Naamini katika kusongambele, na nyie msongembele na pamoja tunasongambele.