Iruru, hili ni jina la aina mojawapo ya ndizi zinazolimwa mikoa ya arusha na Kilimanjaro. Ndizi hii huwa hailiwi na binadamu iwe ni kwa kupikwa ama ikiwa mbivu, ilinaonekana kama ndizi isiyo na maana na wengine huita ndizi ng'ombe! Aina hii ya ndizi hata hivyo huwa haina faida muda wote, ni ndizi muhimu sana hasa kipindi cha njaa, wakati huu iruru huliwa hata ikiwa mbichi pamoja na ukakasi mwingi iliyonao.
Niliamua kutumia hili jina jf kwa maana kubwa moja, nilijiunga jf mara kadhaa kuanzia 2010 lakini kutokana na magwiji na wataalamu wa hoja niliyowakuta huku niliojiona iruru kwani hoja zangu hazikuwa na mashiko saaana! Hata hivyo, 2012, niliguandua kuwa hata iruru kuna wakati huonekana dhahabu hasa wakati ndizi pendwa zikiwa zimehadimika! Leo nafurahia, nami hujiokotea like kutoka kwa wachache kwenye michango yangu hasa wale magwiji wanapoadimika! Mie ndo iruru bhana hahahaaaaa.....