Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Ramea ni jina la marehemu babu, alikuwa magician maarufu, sifa yake kubwa ilikuwa akipiga mtu hata kama ni Kofi lazima ukalazwe ICU, akikunyooshea kidole kukukaripia lazima uumwe. Alikufa na meno yote 32 na miaka karibu 100 na alikula sana nyama pori kuliko nafaka kwakuwa alikuwa na gobole la kupigia ngiri, paa n.k
 
Makanya Jr. jina la Babu yangu la Ujana, Marehemu kwa Sasa hv huwa napenda kujiita ili kumkumbka na Kulikuza zaidi Japo Sio langu majina yangu tofauti
 
Ilikuwa ni wakati wa vita ya Kagera, nikiwa secondary school wenzangu walinipachika jina la Kamanda Chakaza wakinifananisha na general mmoja sikumbuki vema ni Mayunga, Twalipo au Msuguli ambaye alikuwa anatumia jina hilo.
Sababu kuu ni kuwa yalipokuwa yanatokea mambo ya kupigania haki zetu walikuwa wananitanguliza nichakaze
 
Teetotaller=never drink alcohol!


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Gungu ni eneo nililozaliwa....lipo mkoa wa kigoma municipal ya kigoma ujiji....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mimi Ni binadamu mwenye uwezo MKUBWA wa kusurvive na kushinda kuliko binadamu wa kawaida, Huwa nakutana na mambo magum like Misiba, kugombana, kupoteza kitu chochote, Ni rahis kuona magum na kusonga mbele hata iweje ila hua nabaki kawaida as if hakuna kilichotokea
 
natokea MOROGORO milimani kule sehemu fulani AMAZING
nikiwa na miaka 9 tu nilizimia miezi 2 MILIMANI kwenyewe nikifundishwa Mitishamba na kupokea MAELEZO mbarimbari kuhusu mwanadamu na KIUMBE kiitwacho jinni
ndipo nilipofikisha miaka 12 nikakabidhiwa ZANA kamili na MZIMU WA KOLELO na ZOEZI la kwanza nililofanyia FIELD nikiwa na KIONGOZI mkuu ni KUTULIZA kifimbo cha BABA YETU wote
kilichozua taharuki huko kwake ilikuwa ni mwaka mmoja toka afariki uko UK
tukamkabidhisha mwanae

nadumisha mila

wenyewe kule wananiita MKOLELO lakini mkuu mwenyewe ananiita MWANADAMU 7bu mimi na yeye VIUMBE wawili tofauti

Ila mimi najiita MZIMU wa KOLELO
 
Rutabazi aise uyu ni msomi mmoja kabobea sana apo mtaani kwetu, alimalza degree yake ya kwaza ifm akaendelea na cpa kwaiyo jmaa yuko vizur sasa kilicho nafanya hasa nilitumie ili jina nakumbuka kwenye mchakato wa kuwapat wawakilishi ktk bunge la katiba huyu jamaa aliongea sana tena kwa mifano km msomi na kutuelekeza mambo kadha wa kadha lkn alikuja kijana tu elimu yake ni four feliya akaonge kihuni bla bla pale tukapiga kura cha kushangaza rutabazi akapata kura tatu tu yule kijana akiibuka mshindi na kura zakutosha daah hi Kwangu sikuitegemea....
Jina rutabazi ndio likawa maskioni kwangu tokea apo namkubali sana huyu mhaya aise ni kichwa lkn figisufigusu pale kachezewa live
 
Back
Top Bottom