Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Mritimieke=neno la kimakua lenye maana ya unamfanyia mtu wema au kazi lakini hakulipi chochote au kukushuru .nilichagua jina hili baada ya kuona ufisai mkubwa wa wanasiasa huku wapiga kura wakibaki maskini
Munna, nnera chani!? Enyuva uri vai? Njoo pm
 
Jina la kijiji kimoja nchi fulani hivi nilioenda kikazi kutoa misaada ya kibinadamu
 
KWEZISHO - Kitongoji katika kijiji chetu na ndipo kulipo na chemchem ya maji mengi inayotegemewa na watu wengi kipindi cha kiangazi, ila kando tu ya hilo eneo kuna shamba langu.
-Kwa kisambaa ina maana kwenye jicho.
 
ZaBeast (the beast):- wanyama wanashutumiwa saana na wadamu tunapenda kuwashutumu lakini makosa ni yetu siye wanadamu.

Sababu tumepewa utashi na uwezo wa hali ya juu kuliko kiumbe yoyote lakini kwakuwa hatujitambui sisi hulalamika na mara nyingi tunaishi china ya uwezo halisi tulio nai.


Binadamu ambaye anajitambua yeye anakaribia sifa za mnyama hana cha kumsimamisha hellooo..

Be yourself....know thyself...

Hapo wapata neno the beast... yaani that animal that monster who is pretty giant... he does overcome all that ya can expose him to.


Zabeast
 
Kiluuj
KILUU ni ufupisho wa jina langu la kuzaliwa ilhali J ndio herufi ya kwanza ya jina langu la ubatizo.
In most cases, kwenye biashara zangu natumia JAYZED ikiwa na maana 'J na Z' yaani J,herufi ya kwanza ya jina langu na Z ya mke wangu.

E.g.
JAYZED BEADED LEATHER SPECIALISTS,
JAYZED COMMUNICATIONS,
JAYZED SWAHILI DISHES AND BARBEQUE JOINT.
 
KWEZISHO - Kitongoji katika kijiji chetu na ndipo kulipo na chemchem ya maji mengi inayotegemewa na watu wengi kipindi cha kiangazi, ila kando tu ya hilo eneo kuna shamba langu.
-Kwa kisambaa ina maana kwenye jicho.
Safi sana mkuu.
 
N'yadikwa ni mbegu hata hiyo avatar ni mbegu japo watu humu hudhani ni p.u.mb.u, ni jina nililopewa kwa sababu ya kuwafundisha kazi (ufundi) vijana wengi jamaa akanambia wewe ni mbegu jamaa angu Mnyalu akanipa jina hilo hadi kesho hiyo ndo a.k.a
 
Mi ni mtu mchokozi mchokozi...ambae humuwezi ukimchokoza..."MSHARI"
 
Back
Top Bottom