Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Mimi ni jina nilalosubir kwa hamu kumpa Mtoto wangu wa kiume
 
Msomi uchwara;,wakati nipo chuo nilikua naonekana wakati wa presentation, test na UE, yani hadi quiz wenzangu walikua wananifanyia ,,,nikapata upper second na tokea hapo nikaanza kujiita msomi uchwara
Avatar:, huyo dogo ni Mk yupo katika season inaitwa into the Badland,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani mpo salama weekend hii ila mi nimejaribu kujiuliza kwanini watu tumejipa majina haya tunayotumia hapa je yana maana katika maisha yako? Vipi kuhusu Avatar yako?

Mimi kudo lina maana katika maisha yangu hasa nyakat za shule kila tulipojadiliana kitu basi mwishon lazima niseme neno KUDOS kama heko kwa majadiliano yetu na wengi wakapenda kuniita hivyo KUDO

Avatar yangu inasadifu tabia yangu ya kupenda kusoma sana vitabu

Je wewe jina lako na Avatar kwanini umependa kuvitumia?
Alaaa kumbe ndio wewe uliembaka mtoto wa mwenyekiti wa kijiji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukumbi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
Na BAK maana yake hujatoa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaabad= smart,tough and intelligent , mind game player [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] inshort me ni janjajanja

KAABAD THE GREATEST
 
-jimmie ni jina langu halisi

-gatsby ni character ya leonardo dicaprio kwenye the great gatsby (james gatsby)

-avatar..hyo ni Glock G19 Gen4 9x19 pistol maarufu kama glock 9mm
 
SMART PASSENGER = Niliwahi kusafiri kutoka Mwanza kwenda Dar. Sasa tukafika katika eneo moja ambapo matrafiki hukagua abiria...! Aisee huwezi amini Mimi pekee ndo nilionekana kua nmevaa mkanda na tiketi yangu niliyokua nmeishika mkononi barabara tulikuwamo wanavyuo wengi kwenye basi hilo ambao ni watani wangu mmoja tunaye humu JF basi walicheka tulipotoka wakanitania kwa jina hili toka siku hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom