Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kipindi cha miaka ya 1994, lilikuwepo kundi maarufu sana la waigizaji nchini Kenya. ambao walikuwa wanarusha vipindi vyao kupitia KBC. Baadhi ya waliokuwepo kwenye kundi hilo ni Mzee Ojwang, Mama Kayayiii (mke wa mzee Ojwang), Masaku, Otorong'ong'o, Maliwasa, Makanyaga........
Kuna member aliitwa Otorong'ong'o
 
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukumbi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
Jina langu nadhani linafahamika BLACK JACKAL ni A.K.A ya mwamba mmoja hivi alishafanya matukio mengi sana na alipotafutwa alitumiwa wauwaji mahiri na walenga shabaha mashuhuri lakini hawakufua dafuuu 😂
 
tam- initials ya majina yangu rasmi.
sana- niliweka baada ya kuonekana jina 'tam' lilikuwa limesasajiliwa humu. Ili kijitofautisha nikajiita tamsana.
 
Balehe iliniendesha vibaya sana ilinifanya niwe mtu wa mademu na kuangalia porno, kitaa nilishafumaniwa mara kadhaa na vibinti habari zikazagaa mtaani

Nilipofikisha miaka 16 nikaanza zoea la kwenda mtaa wa Ohio Posta kununua malaya, habari zikafika hadi kitaa mbaya zaidi hadi nyumbani. Nikawekwa kikao kwanza na wazazi kisha wakaanza kuletwa wajomba, mashangazi na ndugu wengine wa ukoo

Nikaona isiwe taabu nikabadilisha chimbo la kununua malaya nikaanza kwenda Magomeni kwa Macheni

Pia nilikuwa kuwadi fundi kwenye kuwaaunganishia wengine mademu

Kwa sababu ya hizo mambo wadau wakanibatiza jina la utani mzee wa kupambania utamu (kumá)
Legend 🤣🤣🤣🤣
 
Bubbly mi ni mcheshi napenda story lazima tuongee tu with a vibe.... Molly 😂😂😂😂😂 iykyk.....
 
Kwa sababu natembelea namba 9 namba yenye nguvu kuliko namba zote, herufi za hilo jina ukizijumlisha zote inaleta namba 9
 
Kwa upande wangu, nimeamua kujiita jina la mji ambao upo Uturuki kutokana na kupendezwa na eneo hilo kwani nilishafikaga mara moja kwa shughuli za kibiashara.

Funguka tupe mawazo yako.​
Hatutoi codes yq majina yetu.

Tutabaki kuwa keyboard worrior daima
 
Back
Top Bottom