Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Shansarie ....Jina la mtu muhmu sana ktk maisha yangu amenifanya niwe hivi nilivyo bila yeye nisingekuwa hivi nilivyo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Abarikiwe sana kwa kukufanya uwe hivyo ulivyo mpaka mwenyewe ukajikubali hivyo ulivyo.

Shansarie ....Jina la mtu muhmu sana ktk maisha yangu amenifanya niwe hivi nilivyo bila yeye nisingekuwa hivi nilivyo
 
Hili jina nililitoa kwenye sehemu za starehe, kuna jamaa alikuwa akiingia sehemu yenye yale maji ya rangi ya mende. Haijalishi ana kiasi gani atazitumia zote hadi kufikia hatua ya kukosa hata nauli ya kurudi home.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
nimefurahishwa na uzi huu besti imenibidi nami nijisemee kwanini niilijipa jina hili hapa jf
binafsi nami nilikuwa mwanachama wa jf kitambo kirefu sana wakati ilikuwa inaitwa jambo chat enzi zile
niliona michango ya wenzangu humu jamvini yaliyonipa hamasa kubwa na mi kujiunga nilikuwa bado niko guest katika forum hii mnamo mwaka 2006 hadi 2009 ndipo nikaamua kujiunga rasmi 2011 nikijipachika jina hili la Ladyfurahia ambalo maana yake halisi ni mtu mwenye furaha, upendo, mkarimu, mvumilivu na mcheshi kwa watu wote hivyo ndivyo nilivyo hata sasa wewe muuulize Simplicity atakwambia kwani mtu wangu wa karibu sana
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukubi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hongera zako best naamini hivyo ndivyo ulivyo best hata michango yako mingi hapa inatoa picha hiyo.

nimefurahishwa na uzi huu besti imenibidi nami nijisemee kwanini niilijipa jina hili hapa jf
binafsi nami nilikuwa mwanachama wa jf kitambo kirefu sana wakati ilikuwa inaitwa jambo chat enzi zile
niliona michango ya wenzangu humu jamvini yaliyonipa hamasa kubwa na mi kujiunga nilikuwa bado niko guest katika forum hii mnamo mwaka 2006 hadi 2009 ndipo nikaamua kujiunga rasmi 2011 nikijipachika jina hili la Ladyfurahia ambalo maana yake halisi ni mtu mwenye furaha, upendo, mkarimu, mvumilivu na mcheshi kwa watu wote hivyo ndivyo nilivyo hata sasa wewe muuulize Simplicity atakwambia kwani mtu wangu wa karibu sana
 
Such a wonderful thread. And a creative name BAK. The thread provided a glimpse of the creativity behind most usernames as well as the history of JF. You are such an inspiration.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Jawilat ni name ya my sweet and lovely daughter,by the time i had her in my womb nilikua napenda sana kukaa humu Jf,thats why nikamtafutia jina linaloanza na "Ja" na nlipojiunga rasmi ndo nikalitumia as my ID...
 
My appreciation Karucee 🙂🙂



Such a wonderful thread. And a creative name BAK. The thread provided a glimpse of the creativity behind most usernames as well as the history of JF. You are such an inspiration.[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
siko na siku nyingi toka nijiunge na Jf. Nilipojiunga nilitaka kutumia jina la firstlady mbaya zaidi nikamkuta ndani. Hili nilitaka kulitumia sababu they used to call me that name chuoni kwetu. Nikaona sio mbaya, because l am charming let me use charminglady, lol napo pia nikamkuta ndani ya mjengo, nikaona si mbaya, they have my names and l am nameless so l called myself nameless girl.
 
zedovish don=means a leader or a university/collage teacher or aperson who use peaceful means to solve da problem rather dan fightng or using force
 
Mimi jina langu la Bantu lady linaniwakilisha nilivyo, kuanzia rangi yangu ya chocolate, nina natural hair na umbo ni full bantu. Kwahiyo najiwakilisha mwenyewe.
 
Back
Top Bottom