Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Jina langu linawakilisha kijiji kimoja huko Sengerema. Ni mahali penye asili ya ukoo wangu.
Tulihamo bhanamhala.
 
mimi wakati nipo darasa la sita nilianguka na kuvunjika jino bac washkaj shule nzima walikuwa wananiita kipengo baadae wakafupisha kipe lakini katika kuweka swagga zaid ndo ikawa kimpe lkn kiukwel heruf zote za kimpe zipo kwa jina la baba yangu kasoro I thats all
 
Ipocku, ni jina ambalo niliamua kutumia baada ya kuumizwa na mtu niliempenda. IPOCKU atakumbuka upendo wangu wa dhati, wema, fadhili zangu zote kwake. na hata asipokumbuka IPOCKU nitampata atakae thamini upendo wangu kwake. Mbali na hayo ipocku ni neno la kutia tumaini kuwa mda ukifika kile kitu ulichokuwa ukitamani kwa mda mrefu kitatimia. Ni jina ambalo linanifariji kiukweli.
 
wapi nimesema hivyo angel bana!!

afu unijibu pm yangu ya toka wiki iliyopita..! lols..

We si useme tu kama umechapia.

Pm umenitumia mie haswaa? Labda umekosea direction
 
Last edited by a moderator:
Mimi jina langu nimelimaanisha..am Gender Sensitive na kweli niko hivyo...na hata nikisajisajili kwa jiana lingine nitakuwa namaanisha. My name suggest who iam ..hata kama ningepata fursa ya kujichagulia jina kwenye jina langu halisi basi ningechagua jina lenye maana...pamoja na hayo I like my real name so much ingawaje halina maana yeyote ya msingi.
Roho yake ilale mahala pema peponi

Pumzika kwa amani uko ulipo mkuu
 
Hahhhhahhhhahhha mi ndio languu hivi hiviiii Dinazardeee
 
Mujemaso: ni jina la utani la babu yangu mzaa baba. Maana yake ni Kaeni chonjo/Kuweni macho.
 
Kila wakati nilikuwa mkali sana juu ya wafanyakazi wenzangu ambao wako chini yangu juu ya kutokujali muda. Kuja kazini wanachelewa na kuchelewa huko kunasababisha pia tuchelewe kurudi nyumbani. Kazi zangu ni Engineering so kila wakati unarudi home ukitoka site mida mibovu ambayo nilikuwa naita SaaMbovu hii nikalale mpaka subordinates wangu wakawa wanacheka. Siku nafungua profile hapa nikaipa kitu cha SaaMbovu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi napenda kuchungulia nyuma ya pazia ili kutafuta ukweli wa sarakasi tunayochezewa. Ndiyo maana yake Jasusi.

Ndio maaana ya ujasusi,
Sasa mkuu kwamfano umegundua nn nyuma ya pazia Au hizo sarakasi tunazochezewa manake wengi tumefungwa macho, sio mbaya ukatujuza unajua...¿¿:what:
 
MZIMU, Mama Mzaa Bibi yangu Mzaa Mama Yangu Mzazi (anaitwaga Mama Mkubwa), alikua anamiliki mizimu zaidi ya 90. Baadhi ya Mizimu hiyo inanitembelea kujadili mambo mbali mbali ya Maisha haya. Hapo zamani clan yangu ilikua inaishi katika kisiwa flani katika bahari ya Hindi. Sio Zanzibar, Pemba wala Mafia.
 
Back
Top Bottom