- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliendelea na Operesheni ya Katiba Mpya kwa Kanda ya Victoria tarehe 17 Mei 2026 Geita Mjini, ikiongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho John Heche akiambatana na viongozi wengine.
Madai
Kumekuwapo na taarifa iliyochapishwa na ukurasa wa simpleetz katika mtandao wa X na Facebook ukieleza kuwa akiwa Geita mjini John Heche alisema pesa za tonetone zitajenga nyumba ya Lissu na kuzigawa kwa viongozi.
"Pesa za tonetone mnazochanga tutatumia kununua magari na kumjengea nyumba TUNDU LISSU (Mwenyekiti wa CHADEMA) na zinazobaki tutagawana sisi viongozi wengine maana hatuwezi kufanya kazi bure"
Je, ni kweli kauli hiyo imetolewa na Heche?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video ya mkutano wa CHADEMA Geita mjini umebaini kuwa nukuu hiyo si ya kweli kwani Heche hakutoa kabisa kauli hiyo.
Nukuu hiyo inapotosha uhalisia wa kilichozungumzwa na kiongozi huyo ambaye akizungumza kwenye mkutano huo alisema,
"Haya ndugu zangu wana-Geita tumekuja kwenu kuwaomba jambo la mwisho kabisa. Kiungeni chama hiki mkono, kichangieni chama hiki mkono. Tuko mstari wa mbele tunahitaji mafuta twende kufanya kazi hii.
Tunahitaji kila mtu ajiunge na namna ya kuchangia chama kila mwezi. We dada utatoa shilingi 1,000 utakufa kwa mwezi? [Watu: Aaah, hapana!] Hata ukitoa 5,000 kwa ajili ya ukombozi wako. Na wanakiburi hapa, niliona sijui nani wa CCM anasema "ooh wamegeuka ombaomba", amesahau Mwalimu Nyerere. Mwalimu Nyerere alitumia michango ya wananchi kutafuta uhuru wa nchi hii. Uongo kweli? [Watu: Kweli!] Na ndio maana watu waadilifu kama mzee Warioba, wakiona nchi waliyoipigania inatafunwa right, left and center, wanaumia.
Tunataka ndugu zangu. mchangie chama chetu.... Wananchi wa Geita mimi nawashukuru sana. Asanteni kwa kuja na mkaribishe Lema atuelekeze."