Je, Jua ni Mungu?

Salamu, Humble African .

Swali lako ni gumu sana ndugu yangu, ma'na linataka jibu la ndiyo au hapana. Nisingependa kukubali wala kukataa, ushahidi ninao?.

N'nachoweza kusema ni kwamba, Mungu anaishi juani. Sababu haswa ni baadhi ya vifungu vya Biblia (kwa waaminio) vinavyoelezea alikokaa Mungu. Mimi si nabii, You may agree or dis-agree.

1 Timotheo 6:16

Ambaye yeye peke yake (Mungu) hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, wala hakuna mwanadamu aliyemuona wala awezaye kumuona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

Nuru isiyoweza kukaribiwa ni ipi?..Questions, questions, questions.

Waebrania 12:29

Maana Mungu wetu ni moto ulao.

Moto ulao ni upi?..Questions, questions, questions.

Karibu..
 


Kama huyu Mungu mnaemsemea ndio anahitaji elimu na IQ kubwa namna hii kumuelewa,hanifai kabisa.

Simtaki na wala sitaki kabisa ajihusishe na mimi!

Yaani usipokua Msomi maahiri huwezi mjua MUngu kabisa kama ni hivi!

Mungu gani baguzi namna hii,lenye kujipambanua kwa wenye akili na IQ tu wakati yeye yeye kaumba wanadamu 95% ni wajinga kama mimi hapa tunaenda motoni!

Mungu bwege kabisa hili!
 
Maji yanayopatikana chini kabisa ya Ardhi yana relationship gani na jua kama ilivyo Maji ya Mvua?

Sasa kama kuna watu wanaoishi kwa kutegemea maji ya ardhini tu na wasiohitaji mvua kwa namna yoyote ile si wanaweza kusurvive bila jua inayoleta mvua?
 
Asee!! Mpwa umeandika kitu kikubwa sana. In a simple form.

Jua lina ukuu na utukufu mkubwa sana wa kimungu. Sema watu tuna ignore its reality.

Nimefurahi kuona maandishi yako.
 
Duuu.
Jua sio mungu but coz wanasema hata jua nalo inafikia kipindi linakufa.
Nani kasema jua ni mungu?.

Hapa wanajadili je, jua ni Mungu?. Nb; zingatia herufi kubwa katika jina "Mungu" ili kuondoa utata.

Huko kusema, nani kasema?. Unafahamu fasili ya neno kufa?. Ni kipindi gani inafikia jua linakufa?.

Asalaam.
 
Mkuu hapa nimemwongelea Mungu kwa uelewa wa kisayansi sambamba na religious perspective.

Ila naamini wote tuna IQ sawa ni sawa na Simu zinpotenegenezwa zinakuwa na memory sawa ila inategemea na unavyoitumia memory yako...kuna watu hadi simu inakufa inakuwa na nyimbo tano tu wakati memory yake ni GB 10... This is injustice..!

Mungu atakuuliza hizo GB zilizobaki zilienda wapi?
 
Mpwa..kwa concept ya kuumbwa na kwa kutumia spiritual energy sisi tuna uungu ndani yetu maana Mungu ni spiritual energy pia.

Nakubaliana na kauli yako ila nataka ujue yupo mmoja ndio the most supreme being..The God.
Hahaha una akili lakini wewe ni muoga. Kubali kwamba sisi ni miungu, ila tunazidiana ufahamu.
God yuko wapi sasa kwenye jua?! Huo mwanga upo hata sayari ya kwanza mbona hakuna uhai?!
Hakuna ajuaye uhai ni nini, damu au oxygen?! Hapo ndio tuna mleta God, kila tunaposhindwa kwenda nje ya fikra zetu tuna mleta mungu, na kunawalio shindwa kabisa uabudu wenye uwezo na kuwapa uungu. Na wapo wanaosema ukifikili extraordinary wewe ni shetani. Wapo wanaosema wazungu ndio shetani(lucifer) eti wanaakili kama mungu na mengi wayafanyayo mungu hakutaka tuyajue, leo wana tengeneza ndege, satelite, dawa kuponya, wanaotesha cell kuponya magonjwa, wanazalisha artificially by insemination na in vivo au in vitro, wana fanya grafting, dialysis na mengine mengi.
Sasa uwezo huo wapo wanaouona ni baraka za mungu kwa mwanadamu, na wapo wanaoona huo ndio uungu, na wapo wanaoona huo ndio ushetani wenyewe.
Sasa inategemea unafikiri vipi na reasoning yako ikoje.
Jua na mionzi yake linaweza kuwa ni source of something au ingredient of life lakini lenyewe pekeyake siyo mungu.
 
Asee!! Mpwa umeandika kitu kikubwa sana. In a simple form.

Jua lina ukuu na utukufu mkubwa sana wa kimungu. Sema watu tuna ignore its reality.

Nimefurahi kuona maandishi yako.
You nailed It, Man of God.

Ujue jua ni Tukufu?. Binadamu hawezi kusogelea jua na hakuna uchafu wowote utakaosogea iliko jua. Tutaenda mwezini, ardhini na kadhalika, ila juani hapana. Huu ni utakatifu.

Sina la kuandika zaidi. Labda niendelee kusoma mawazo ya wanabodi wengine na pengine nitaongeza kadhaa, kwa baadae.
 
Nadhani watu walipaswa kuabudu mvua maana inaleta chakula pia..jua huwa watu hawalipi kipaumbele sana maana likizidi ni lawama tofauti na mvua.
Mkuu ukifatilia pia hakuna mvua vila jua....lazima jua lipige kwenye uso wa maji au mimea ndipo utapatikana mvuke ambao baadaye utashuka kama mvua!?
 
Mkuu ukifatilia pia hakuna mvua vila jua....lazima jua lipige kwenye uso wa maji au mimea ndipo utapatikana mvuke ambao baadaye utashuka kama mvua!?
Huu ndio ukweli wa wazi. Sun is mystical..sun is Godly.

Jua ni takatifu...halitaki uchafu wenu wa Duniani. Linachoma na kula kila kitu.. Satellite za wazungu zilizothubutu kukaribia jua zimechomwa sana.

Nakushukuru mkuu kwa mchango jadidi.
 
Ushasema hazina ukweli alaf bado unataka kuwajua waliopima..mzee vip uko sawa kweli? Ebu tuambie ww umbali wa kutoka lilipo jua mpaka duniani ni km ngapi??
 
acha kutudanganya ...miaka bilion aliekwambia dunia ilikuepo nan?? kifaa gani kinatumika kupimia umri wa dunia
 
Not all water comes from evaporation+ condensation then precipitation with the help of sun. ua talking about Rainfall...right?

What about underground water? water about surface water?
Pamoja na yote hayo, hakuna mmea utaweza kukua pasipo na jua. Jua lina play part kubwa sana kwenye uhai mzee
 


Mkuu

Kuchukua mfano wa memory ya simu kufananisha na IQ ya mwanadamu ni kosa.Ni vitu viwili totally oxymoronic!

Binadamu wote wana IQ sawa?Hii assertion umeitoa wapi?Binadamu wote hawafanani,na hawana IQ identical,ndio maana kuna IQ scale.

Kumbe Mungu anaongelewa kisayansi?Nikiwa mwanasheria naweza muongelea Mungu kiuanasheria na nikawa sawa na wewe mwanasayansi?Unaona raha sana kudanganya watu eee?

Hoja yangu inasimama palepale,inakuaje huyu Mungu mpaka umuelewe uwe na IQ kubwa namna hii,na uwe msomi unaejua kusoma na kuandika na mwenye kujua dunia kisayansi na elimu zingine chungu nzima!Ndio nikatoa rai,inakuaje sisi wanadamu 95% ya population ya dunia tuliumbwa na yeye yeye kama wajinga wenye IQ ndogo au wastani isiyoweza kujua elimu zote hizi za ulimwengu,ni lazima twende motoni..Nyie wasomi 5% tu ndio mtamjua yeye vizuri maana mna akili na ndio mtaenda mbinguni.

Ndio maana nikasema huyu Mungu wenu ni baguzi namba moja,mkae nae nyie vichwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…