Je, Jua ni Mungu?

Je, Jua ni Mungu?

Kwanza kabisa lazima uelewe maana ya mungu. Ukishajua maana ya mungu, ndio utapata jibu kuwa jua ni mungu au sio mungu

Kwa upande wangu mimi naamini kuwa mungu ni yupo kwenye fikra tu. Ni sawa na muda ulivyo kwenye fikra. Au mipaka ya nchi ilivyo kwenye fikra.

Yaani mtu alifikiri nini chanzo cha yote haya. Baada ya kukosa jawabu, ikabidi afikirie kuwa kuna kitu chenye uwezo mkubwa ambacho aliamua kukipa jina mungu kama utambulisho.

Kiuhalisia hakuna kitu kinaitwa mungu. Ni mawazo tu na fikra ndizo zinatambulisha uwepo wa mungu.

Hivyo basi, ukiamua kulifanya jua kuwa mungu unaweza maana sijui wewe sifa za kitu kuwa mungu ni zipi
 
Mkuu

Kuchukua mfano wa memory ya simu kufananisha na IQ ya mwanadamu ni kosa.Ni vitu viwili totally oxymoronic!

Binadamu wote wana IQ sawa?Hii assertion umeitoa wapi?Binadamu wote hawafanani,na hawana IQ identical,ndio maana kuna IQ scale.

Kumbe Mungu anaongelewa kisayansi?Nikiwa mwanasheria naweza muongelea Mungu kiuanasheria na nikawa sawa na wewe mwanasayansi?Unaona raha sana kudanganya watu eee?

Hoja yangu inasimama palepale,inakuaje huyu Mungu mpaka umuelewe uwe na IQ kubwa namna hii,na uwe msomi unaejua kusoma na kuandika na mwenye kujua dunia kisayansi na elimu zingine chungu nzima!Ndio nikatoa rai,inakuaje sisi wanadamu 95% ya population ya dunia tuliumbwa na yeye yeye kama wajinga wenye IQ ndogo au wastani isiyoweza kujua elimu zote hizi za ulimwengu,ni lazima twende motoni..Nyie wasomi 5% tu ndio mtamjua yeye vizuri maana mna akili na ndio mtaenda mbinguni.

Ndio maana nikasema huyu Mungu wenu ni baguzi namba moja,mkae nae nyie vichwa!
Wewe atheist usieamini uwepo na uweza wa Mungu kaa pembeni hii Mada inawahusu wale wote waliotayari kutafuta USO wa mungu bila kuchoka na kwa gharama yeyote ile.

Kama unaweza kupangua hoja zangu kwa ufanisi mkubwa na kutafuta mwanya wa kunifanya nionekane mbabaishaji ...unataka IQ gani tena we mzee?
 
Wewe unaamini JUA,basi wewe ni atheist kwa yule aaminie MLIMA!

Kila mtu ni atheist kwa kile asichoabudu yeye!

Na kwa taarifa yako tu,binadamu wote tulizaliwa ATHEISTS siku mama zetu wanajifungua!Tulikua hatuna taarifa kabisa kama kuna lidude linaitwa Mungu au shetani.....Tulianza kubadilika tu pale wazazi na walezi zetu walipoamua kutushinikiza tunamini wanavyoamini wao eti sababu ni wazazi.Hatukuchagua,walitulazimisha!

Hivyo huna lolote la maana unaweza nieleza na huyo Mungu wako JUA.Kuna miungu chungu nzima humu ambao wewe ni atheist to them like they are to yours.

So stop eating your own butt!
 
You seems to be very depressed and stressed mpwa.
 
Wala Mpwa!

Ni wewe tu unawaza hivyo!

Im doing good mpwa!Ni kwamba tu tunatofautiana sana.

Na infact,kutofautiana ni vizuri sana na ni very healthy!

Wala usijali mpwa,tuko pamoja!
Huwa naamini utofauti wa Mawazo ndio utajiri wa Mawazo.

Ila inapofikia mtu anapinga uwepo wa the most high...supreme being huwa navurugwa ufahamu na kuhisi labda one needs psychotherapy!

Huwa naheshimu kile mtu anachoamini ni sahihi kwake na kuuacha ubongo wangu wazi kupokea mapya.. Nkiona ina make sense namuunga mkono. I'm very open minded who ponder with common sense and not IQ.
 
Mungu ni kitu cha kufikirika. Kwa upande wangu huwa sifikirii kuhusu mungu. Kwahiyo siwezi kukujibu kuhusu hilo maana mimi siamini kabisa habari za mungu
Hakuna mtu aliyekuuliza habari za Mungu kuwa ni wa kufikirika au lah.

Umesema kuwa jua ni kila kitu katika uhai wa binadamu nikakuuliza Je Maji?

Mambo ya Mungu umeyatoa wapi hapo?
 
Kwanza kabisa lazima uelewe maana ya mungu. Ukishajua maana ya mungu, ndio utapata jibu kuwa jua ni mungu au sio mungu

Kwa upande wangu mimi naamini kuwa mungu ni yupo kwenye fikra tu. Ni sawa na muda ulivyo kwenye fikra. Au mipaka ya nchi ilivyo kwenye fikra.

Yaani mtu alifikiri nini chanzo cha yote haya. Baada ya kukosa jawabu, ikabidi afikirie kuwa kuna kitu chenye uwezo mkubwa ambacho aliamua kukipa jina mungu kama utambulisho.

Kiuhalisia hakuna kitu kinaitwa mungu. Ni mawazo tu na fikra ndizo zinatambulisha uwepo wa mungu.

Hivyo basi, ukiamua kulifanya jua kuwa mungu unaweza maana sijui wewe sifa za kitu kuwa mungu ni zipi
Yani mtu atafute jawabu la jambo na hakakosa jawabu ila akaamua tu kubuni jawabu,na akaelekeza nguvu zake katika hilo jawabu la kubuni tu na ndiyo fikra hizo zimeenea duniani?
 
Wewe unaamini JUA,basi wewe ni atheist kwa yule aaminie MLIMA!

Kila mtu ni atheist kwa kile asichoabudu yeye!

Na kwa taarifa yako tu,binadamu wote tulizaliwa ATHEISTS siku mama zetu wanajifungua!Tulikua hatuna taarifa kabisa kama kuna lidude linaitwa Mungu au shetani.....Tulianza kubadilika tu pale wazazi na walezi zetu walipoamua kutushinikiza tunamini wanavyoamini wao eti sababu ni wazazi.Hatukuchagua,walitulazimisha!

Hivyo huna lolote la maana unaweza nieleza na huyo Mungu wako JUA.Kuna miungu chungu nzima humu ambao wewe ni atheist to them like they are to yours.

So stop eating your own butt!
Mkuu unataka kusema kwamba tulizaliwa tukiwa na mawazo ya kwamba hakuna mungu?
 
Mungu ni kitu cha kufikirika. Kwa upande wangu huwa sifikirii kuhusu mungu. Kwahiyo siwezi kukujibu kuhusu hilo maana mimi siamini kabisa habari za mungu
Ila hata kuona kuwa hakuna mungu ni jambo la kufikirika pia mkuu.
 
Maji yanayopatikana chini kabisa ya Ardhi yana relationship gani na jua kama ilivyo Maji ya Mvua?

Sasa kama kuna watu wanaoishi kwa kutegemea maji ya ardhini tu na wasiohitaji mvua kwa namna yoyote ile si wanaweza kusurvive bila jua inayoleta mvua?
Mbona jamaa kaeleza vizur tu uhusiano wa maji ya ardhini na jua!. Somani taratibu,elewa,tafakari halafu ndio uchangie!.

"Hayo maji ya ardhini bila jua yangekuwa barafu".
 
Back
Top Bottom