Je Kabla ya Adam na Hawa, hawa watu walioumbwa na MUNGU walikuwa kina nani?

Je Kabla ya Adam na Hawa, hawa watu walioumbwa na MUNGU walikuwa kina nani?

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Leo ningependa sana kujifunza kutoka kwenu, atakayeweza naomba mnijibu swali langu kulingana na maandiko. Siku hizi nasoma sana Biblia.

Sasa swali langu ni hapa:

Ukisoma Mwanzo 1:26 ni kwamba Mungu anasema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, na dunia yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” na akamuumba mwanaume na mwanamke. Yaani hapo, watu wanasema kwamba huyo mwanamke alikuwa Lilith. Je, mwanaume alikuwa nani?

Lakini ikumbukwe Lilith ni hadithi ya Kiyahudi inayotokana na maandiko ya Kabbalah na vyanzo vingine vya midrash. Inadaiwa kuwa Lilith alikuwa mwanamke wa kwanza aliyeumbwa pamoja na Adamu, lakini alikataa kumtii na akaondoka. Hata hivyo, hii si sehemu ya Biblia ya Kimasoretiki wala Agano la Kale, bali ni hadithi za kale ambazo hazipatikani moja kwa moja katika maandiko.

Kumbuka hapo Adam hakuwa ameumbwa mpaka pale Mwanzo 2:7-8 "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akapanda bustani mashariki mwa Edeni; huko akamweka huyo mtu aliyemfanya." ambapo sasa Mungu akamuumba mtu kutoka mavumbini, akamuweka bustanini, na kumpa pumzi. Huyu ni Adam. Lakini Mwanzo 1:26 kuna mtu aliumbwa.

Hapa nilichojifunza ni kitu kimoja: Adam hakuumbwa bustanini, aliumbwa nje ya bustanini na mule akapelekwa na kuwekwa.

Sasa hapa inaweza kuwa kuna majibu ya maswali yenu mengi tu kwamba mtoto wa Adam alipata vipi mke? Kama Adam aliumbwa nje ya bustani, hii inaonyesha nje ya hiyo bustani kulikuwa na uumbaji wa watu wengine wengi ambao Mungu aliwaumba.

Na Adam, watoto wake walijua kabisa kwamba nje ya bustani kulikuwa na watu wengine ambao Mungu aliwaumba. Ndiyo maana baada ya Kaini kumuua ndugu yake, akamwambia Mungu kwamba adhabu aliyopewa ni kubwa mno na kila atakayemuona atamuua.

Kaini alijua kabisa sehemu nyinginezo kulikuwa na watu. Inawezekana kabisa Adam aliwaambia kuhusu uwepo wa watu wengine nje ya bustani hiyo, na ndiyo maana hata Kaini aliogopa kwamba watu hao wengine watakaomuona wanaweza kumuua. Alichokifanya Mungu ni kumuwekea alama ili kwa yeyote ambaye atamuona asije akampiga. Kaini akakimbilia Nodi na kuoa huko.

Tafsiri nyingine za kidini zinaweza kusema kuwa mke wa Kaini alikuwa mmoja wa dada zake, kwa sababu Biblia inataja kuwa Adamu na Hawa walikuwa na watoto wengi (Mwanzo 5:4 -"Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane; akazaa watoto wa kiume na wa kike." ). Hata hivyo, wazo la kwamba kunaweza kuwa na kundi jingine la wanadamu nje ya Bustani linaweza kuwa na mashiko kwa kuzingatia simulizi ya Mwanzo 1:26-28

("Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, na dunia yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba; mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, mkaitiishe; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.")

Sasa hapa nimewapa majibu tu kwamba kama Adam na Hawa walikuwa na watoto wawili kipindi hicho, mke wa Kaini alitokea wapi? Jibu ni kwamba Mungu alikuwa ameumba watu wengine wengi tu ila baada ya kumuumba Adam, akaamua kumuweka ndani ya bustani. Adam hakuumbwa ndani ya bustani.

Turudi kwenye swali langu:

Wale watu wa kwanza kuumbwa, mwanamke na mwanaume wa Mwanzo 1:26-28, walikuwa akina nani? Hebu subiri, na mimi kama najipa jibu hapa... eeeeh! Inawezekana ni miongoni mwa watu ambao Mungu aliwaumba mbali na Adam na Hawa. Tena hao watu si ndiyo wakaambiwa nendeni mkazaane na kuijaza nchi? Kumbuka hayo maneno hawakuambiwa Adam na Hawa; waliambiwa watu wengine kabisa. Nenda kasome kitabu cha Mwanzo.

Kabla ya kuandika nilikuwa na hilo tu
 
Back
Top Bottom