Ubora wa wanawake waumini watakao ingia peponi kuliko Mahurul-ain.
Ummu salamah (radhia Allahu anha) alisema kwamba nilimuuliza Nabii (swallallahu alayhi wasallam)"
"Ewe Nabi wa Allah! wanawake wa Duniani ni bora zaidi au Mahurul-ain wa Peponi?
Nabi (swallallhu alyhi wasallam) akajibu: Wanawake wa Duniani watakuwa bora zaidi kuliko Mahurul-ain kama vile (Ribon) ya nje ya nguo ni bora kuliko ya ndani.
Ummu Salamah (radhia Allahu anha akauliza: kwa sababu gani?
Nabii (Swallallahu alayhi wasallam) akamjibu: Kwa sababu walitekeleza Swala, wakafunga saumu zao na wakamuabudu Allah (Azza Wa Jalla). Allah atawaweka nuru ndani ya nyuso zao na Hariri kwenye miili yao. Wanawake wa Duniani watakuwa na miili na rangi nzuri zakuvutia zilizo sawa na watavaa nguo za kijani kibichi na vito vya manjano. Vichetezo vyao vitakuwa ni vya lulu na vichana vya nywele ni dhahabu.
Watasema wanawake wa Duniani (wakishaingianPeponi) ; sisi ni wanawake tutakao kaa milele na hatutakufaa tena. Sisi ni wanawake ambayo siku zote tutakuwa na maisha mema mazuri tuliomakinika nayo na hatuna tena dhiki wala uzito wowote. Sisi ni wanawake ambao tutaketi (Peponi) wala hatuondoki tena. Sikiliza, sisi tuna furaha na hatutakuwa tena na huzuni milele. Bishara njema kwa wale wanaume ambao sisi ni wake wao na wao na waume wa sisi.
(Tabrani).
Kama vile uzuri wa Mahurul-ain ulivyo, wanawake wa Duniani watakuwa ni bora na wazuri zaidi kuliko Mahurul-ain ndani ya Pepo.
Fikiria, itakuwaje kuvutiwa na furaha na kupendezwa na wanawake wa Duniani watakao jaaliwa kuingia Peponi!
KUlingana na sifa za Mahurul-ain walivosifiwa watakuwa hawawafikii kwa uzuri wanawake wa Duniani waliokuwa wema Duniani wakaingia Peponi.
Ndani ya Qur'an na Hadith za Mtume (Swallallahu alayhi wasallam) tumesoma kuwa Hurul-ain ni mwanamke mdogo aliye mzuri sana mwenye kuonekana mwili wake mpaka ndani ya mfupa yaonekana kama misitari ya lulu na rubii. Anafana na tembo jekundu ndani ya glasi nyeupe.
(AtTirmidhi)
Hurul-ain ana macho makubwa, mazuri na mboni yake nyeusi na jicho jeupe sana.Ana haya sana na mwenye kuinamisha uso wake chini. Hawezi kumuangalia mwanamume yoyote kabisa ispokuwa mume wake tu.Atajisikia furaha na kushukuru kuwa mke wake na atakuwa mwenye kuweka amani na mumewe kila wakati. Hurul-ain ni mdogo na hawezi kufaa na umri utabaki mdogo wala hazeeki. Atakuwa hana uadui na mumewe na anazungumza kwa upole na utaratibu.Ni mweupe na hata kuwa na upungufu wala kasoro yoyote kama vile kutokwa na damu ya hedhi wala kukojoa au kutokwa na haja kubwa au kubeba mimba na mfano wa hivyo.
(AtTirmidhi)
Kwa vile ameletwa kwa Starehe , yeye mwenyewe ni starehe tosha! Ikiwa Hurul-ain ata angalia ardhini kutoka mbinguni, basi ile urefu wa masafa baina ya Mbingu na Ardhi Itajaa Nuru na harufu nzuri kutoka kwake. Uso wake unangaraa kuliko kioo na aweza mtu kujiona uso wake ndani ya machafu yake. Pindi mumewe akigeuza uso kuangalia kwingine basi uzuri wake unakuwa mzuri zaidi kwa mara sabini.
Ikiwa atatema mate ndani ya bahari kubwa saba za maji ya chumvi basi yale maji yote yatageuka kuwa tamu kuliko asali.
Hata hivyo,wanawake Waislamu wa duniani watakaoingia Peponi hawatasikia wivu kwa Mahurul-ain kwa namna watakavyokuwa wazuri sana kuliko Mahurul-ain kwa kila namna ya uzuri.Wanawake wema watakaoingia Peponi, hata kulingana na umri waliokufa nao na namna walivyo umbwa Duniani, watakuwa wanavutia sana kuliko Mahurul-ain wa Peponi. Hurul-ain ni mojawapo tu ya mapambo ya Peponi . Ameumbwa kwa ajili ya mtu fulani.
Upande mwingine wanawake Waumini wanastahiki ya kupata malipo makubwa na watapewa malipo hayo makubwa huko Peponi.
Hadithi hii inatueleza ubora wa wanawake wa Duniani kuliko Mahurul-ain wa Peponi. Na ni kwa kuwa walichagua kumuabudu Allah (Subhana Allah wa Ta'ala) hapa Duniani.
Wasia kwa madada zetu na mama zetu, Ikiwa mtaswali swala zenu tano kila siku na mkafunga saumu ya Ramadhani na mkawatii waume zenu na mkalinda tupu zenu ispokuwa kwa waume zenu basi mtaingia peponi kwa mlango mtakao nyinyi.
Allah awajaliye madada zetu na mama zetu na wake zetu ni wenye kuingia peponi . Ameen
Sent from my V2204 using
JamiiForums mobile app