Je, kampuni gani nzuri ya kuagiza magari nje ya nchi?

Je, kampuni gani nzuri ya kuagiza magari nje ya nchi?

Airmanula

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
3,527
Reaction score
5,762
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, wadau tushirikishane kampuni nzuri na best inayomfaa mteja kuagiza magari nje ya nchi.

Na pia wale ambao wamewahi kuagiza watupe uzoefu wao na waliyopitia, je gari uliyoletewa ndio yenyewe? Vifaa vya ndani je ndivyo vyenyewe?

Pia wale ambao hununua magari kutokea kwenye yard za watu nchini, mtupe uzoefu wenu, naambiwa kua kununua gari kutoka kwenye yard za hapa nchini ni risk, sababu wahusika hua magari yakifika nchini wanatoa vifaa vinavyokuja na gari ambavyo ni orijino na kuweka mafamba, je kuna ukweli wowote.

Karibuni.
 
Huu uzi ni muhimu sana kwangu kwa sababu nimepanga januari 2021 ninunue ndinga.Hivyo michango ya wanabodi ktk uzi huu itanipa mwanga wa kujua niagize nje au ninunue humuhumu nchini.
 
Raha ya kunua gari YARD anakupa warrant mda furani, pia unaweza kumshusha bei ya kununua, nenda Yard za maana sio za wabongo wenye njaa utauziwa box au body na no.

Hasara za kuagiza bei inaweza panda kuzidi ya Yard, unaweza letewa gari ina kasoro ukashindwa kuirudisha.

N.B njia zote ni salama na zina changamoto zake ni kuwa makini tu mnunuzi
 
Raha ya kunua gari YARD anakupa warrant mda furani, pia unaweza kumshusha bei ya kununua, nenda Yard za maana sio za wabongo wenye njaa utauziwa box au body na no...
Ushauri mzuri,

Ni yard gani kwa hapa Tanzania wanaweza kukupatia Warrant kwa gari zao haswa hizi used?

Na hiyo warrant ni ya muda gani ama kilometa ngapi?
 
Binafsi nimekua nikiagiza tokea mwaka 2014, takriban miaka 6 sasa ya uzoefu.

Kuna kampuni tau ninazoweza kuzi recommend

1. Be forward japan
2. Sbt Japan
3. Enhance Autos

Kwakweli naweza sema kwamba , ni miongoni mwa makampuni bora sana na hata gari nyingi zilizojaa yard nyingi hapa nchini zinanunuliwa kwenye makampuni hayo

Autocom, naisikia ina huduma nzuri ila bado sijawahi kufanya nao kazi. Mwakani Mungu akipenda nitajaribu kuagiza kwao nao nione huduma zao zilivyo

Ahsante.
 
Raha ya kunua gari YARD anakupa warrant mda furani, pia unaweza kumshusha bei ya kununua, nenda Yard za maana sio za wabongo wenye njaa utauziwa box au body na no...
Kununua yard hakuwezi kuwa nafuu kuliko kuagiza kwani hata wenye yard huagiza hukohuko, kikubwa ni kuwa na uelewa wa jinsi ya kuagiza, tafuta kampuni ya uhakika tena ukipata yenye uwezo wa kukuonyesha auction sheet hii ndio bora zaidi, kwani hizi gari used zinavyouzwa kwenye minada zipo katika grade tofauti mfano kuna grade 4.5 hii ni kama mpya kabisa ikifatiwa na grade 3.5 hii ina mapungufu kidogo, grade 3 na grade R, R ikimaanisha repair kwamba ilipata ajali then ikafanyiwa repair hivyo wengi wakati wa kuagiza wengi huangalia picha tu bila kuangalia grade ya gari
 
Binafsi nimekua nikiagiza tokea mwaka 2014, takriban miaka 6 sasa ya uzoefu.

Kuna kampuni tau ninazoweza kuzi recommend...
Autocom nimefanya nao kazi sana, uzuri wao ni bei zao... Ziko very affordable hata gari nayotumia sasa nimeagiza kwao na nikikuambia bei yake huwezi amini

Enhance ubaya wao ni mabei makubwa japo gari zao zimenyooka kiasi chake pia wako vizuri kwenye kuku update...
 
Binafsi nimekua nikiagiza tokea mwaka 2014, takriban miaka 6 sasa ya uzoefu.

Kuna kampuni tau ninazoweza kuzi recommend..
Kampuni zipo nyingi sana na hakuna mbaya wala ilimradi ipo kwenye shilikisho la wauza magari huku Japan(JADA) ingawa nilichokiona watanzania wengi wamebobea kununua magari kwa haya makampuni ambayo yenyewe huenda minadani kununua magari na kuuza tena kama aliolist mchangiaji.

Ila pia kuna makampuni mengi tu ambayo yenyewe yamesalijiwa na hufanya kazi ya kwenda kuwanunulia watu magari minadani na kuwatumia huzuri wa mfumo ni kuwa unaweza kufanya kama masihara na ukapata gari kwa bei nafuu sana, unakuta gari mnadani inaanza na zero price hivyo ukiwa na bahati unaweza weka any bid kama hakutakuwa na mshindani ukawini
 
Kununua yard za kibongo ni kubahatisha zaidi unless uwe mzoefu na si gari yako ya kwanza au uende na battalion ya mafundi waaminifu.

Kuna magari mkangafu yametumika Zanzibar baada ya kutoka Japan na yanauzwa yard kwa bei ileile ya Jp huku yameshushwa KM.

Tafuta humuhumu Jf kuna shuhuda za hadi mtu kuuziwa gari ya wizi yard.
 
Kampuni zipo nyingi sana na hakuna mbaya wala ilimradi ipo kwenye shilikisho la wauza magari huku Japan(JADA) ingawa nilichokiona watanzania wengi wamebobea kununua magari kwa haya makampuni ambayo yenyewe huenda minadani kununua magari na kuuza tena kama aliolist mchangiaji...
Hizo kampuni zimesajiliwa wapi kaka?

Na taratibu zao ni zipi.?!
 
Kampuni zipo nyingi sana na hakuna mbaya wala ilimradi ipo kwenye shilikisho la wauza magari huku Japan(JADA) ingawa nilichokiona watanzania wengi wamebobea kununua magari kwa haya makampuni ambayo yenyewe huenda minadani kununua magari na kuuza tena kama aliolist mchangiaji...
Taja hizo Kampuni wazee wa mtelezo tushuke
 
Kununua yard za kibongo ni kubahatisha zaidi unless uwe mzoefu na si gari yako ya kwanza au uende na battalion ya mafundi waaminifu...
Ile nyuzi naikumbuka aisee, polisi na mwenye yard walikuwa wanatapeli wateja kwa kubambikia kesi umenunua gari ya wizi.

Kuwa makini na yard utayonunulia gari lako na ufanye uchunguzi wa hali ya juu sana, kama huwezi agiza tu.
 
Back
Top Bottom