Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Praise and worship teams, imekuwa sehemu muhimu ya ibada katika makanisa mengi. Hata hivyo, kwa baadhi ya waumini, makundi haya yamekuwa chanzo cha kero na mzozo ndani ya kanisa. Wengine wanadai kuwa Praise and Worship ni sehemu mbaya zaidi ndani ya kanisa.
Utandawazi umefanya baadhi ya nyimbo za Injili kuanza kuiga mitindo ya muziki wa kidunia, kama vile R&B, hip-hop, na pop. Hii imefanya baadhi ya waumini kuhisi kuwa muziki huu haumheshimu Mungu kwa njia inayofaa.
Katika baadhi ya makanisa, Praise and worship wamepata nafasi kubwa sana, na mara nyingi wanaonekana kupendelewa na uongozi wa kanisa. Hii inaweza kusababisha migogoro kati ya wanakwaya wa jadi na makundi ya Injili, na pia inaweza kuwafanya baadhi ya waumini kuhisi kuwa hawajumuishwi katika ibada.
Kanisa lina kwaya ya Vijana, Kwaya ya Kina Mama pamoja na Kwaya Kuu ya Kanisa, je kuna ulazima wowote wa kuwa na Praise and Worship team? Je kwaya hizi tatu haziwezi kuongoza ibada?
Ingawa ndani ya Praise and Worship kuna watu mbalimbali wenye vipaji vya muziki, wengine wanaonekana kuzingatia zaidi kuimba kwa sauti kubwa na kucheza kuliko kuzingatia ubora wa muziki wao. Na hii imejionesha sio kitu cha kificho, watu kukata mauno, mavazi pamoja na kuonesha mitindo hatari ya uchezaji. Hii inaweza kusababisha usumbufu kwa waumini wengine ambao wanatafuta ibada ya kina na yenye utulivu.
Baadhi ya wanakwaya wanaweza kuonyesha kiburi na kujiona kuwa 'nyota' wa kanisa. Hii inaweza kuwafanya kuona wenzao wa kanisa kwa dharau na kuwadharau. Hii ni kinyume kabisa na mtazamo wa unyenyekevu ambao unapaswa kuwa tabia ya kila Mkristo. Kwa kuwa mtu yupo kwenye Praise and Worship basi hujiona ni miungu watu katika mambo mengi yanayofanyika ndani na nje ya Kanisa.
Ndani ya kundi hili, wapo watu wanaolitumia kujificha na kufichia mambo yao mabaya. Namna ambayo Kanisa limeharibika sio ajabu kumkuta mdada wa Praise akiwa amevaa Kikuku miguu yote miwili, ukimgusa atakujibu kwa hoja kuwa Mungu yupo moyoni mwake, na pia yeye ni mmaasai kuwa kuvaa kikuku ni utamaduni wake.
Muziki unaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kueneza Injili, baadhi ya nyimbo za Injili hazina ujumbe wa kiimani kabsa, wengi wanafahamu hilo. Badala yake, zinazingatia hisia za kihisia na za kimwili. Hii inaweza kusababisha baadhi ya waumini kuhisi kuwa muziki huu hauwasaidii kukua kiroho, bali upo kwa ajili ya kujipatia umaarufu tu.
Praise and Worship wanaweza kuwa chombo muhimu cha ibada, ni muhimu kuhakikisha kuwa wanatumika kwa njia inayomheshimu Mungu na kuimarisha imani ya waumini. Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa muziki wa Injili hauingii kwenye mwelekeo wa kidunia na kwamba unabeba ujumbe wa kiinjili.
Pia tukae pamoja katika kuangalia na kuzingatia umri na rika ambazo zinatakiwa kuingia, mbeleni tutaanza kutoa machozi kwenye jambo ambalo tungeweza kulitazama. Tusiwapeleke watoto wetu vichwa vichwa mkawaacha na vijana, unyanyasaji wa kijinsia upo sio wa ME wala KE.
Swali la msingi: JE KANISA LINAHITAJI UWEPO WA PRAISE AND WORSHIP TEAM?