Je, kanisa linahitaji uwepo wa praise and worship team?

Je, kanisa linahitaji uwepo wa praise and worship team?

Praise and worship teams, imekuwa sehemu muhimu ya ibada katika makanisa mengi. Hata hivyo, kwa baadhi ya waumini, makundi haya yamekuwa chanzo cha kero na mzozo ndani ya kanisa. Wengine wanadai kuwa Praise and Worship ni sehemu mbaya zaidi ndani ya kanisa.
Halafu inaleta ubaguzi na mgawanyiko makanisani, hiyo timu hujiona na kujisikia imetwaa ufalme wa Mungu tayari na kuwadharau wasio praise
 
Hapa naona ni mada ya kilokole huko kwa kina MWA... +Manabii na mitum haya mambo kwenye kanisa moja, katoliki na la mitume sijawahi yaona wala kuyasikia.
hilo kanisa halina upako, linaendeshwa kwa akili za kibinadamu
 
Bishop katunzi kuna siku aliwahi huwateremsha pale madhabauni 😀😀😀, baadhi ya vikundi vya praise vimegeuka madanguro
 
Mungu alimuagiza Daudi aandae kikundi cha kwaya yenye waimbaji watakaoongoza uimbaji wakati wa ibada. Viongozi wao walikuwa ni wakina Ethan Asafu nk. Na hata baadhi ua zaburi hawa mabwana wameandika wao.

Watu hawa walikuwa ni watu wasafi na wenye viwango vya juu vya kiroho na kimaandili
Mfano Asaph alikuwa nabii. Waliongoza kundi kubwa la kwaya ya watu 400+ na mamilioni ya waabudu.

Hawa sina shida nao isipokiwa wanapaswa kuwa watu wenye usafi wa juu. Ila kile wanachokiita praise and worship ni miziki ya kidunia yenye maneno ya Mungu. Miziki hiyo inafukuza malaika na kutoa miariko kwa majini na mapepo kwenye ibada.

Hekimq kubwa inatakiwa katika kuchagua unaimba nini kwa beats zipi na kwa sauti yenye utulivu mkubwa katika kuliongoza kanisa kwenye sifa.


Kama hawana viwango h8vi wafukuzwe wakakae huko tuimbe kwa kuongozwa na vinanda.
 
Vikundi vingi vya praise and worship wanawa target wanavyuo, dressing code zao nyingi ni kimbembe 😀😀
 
hapo ndipo hunishangaza, wanapataje ujasiri wa kuabudisha bila dhamiri zao kuwahukumu huku wanajua kabisa wananyanduana?
Kwani siku hizi kuna ibada..? ma pastor wanawatafuna, walimu wao wanawatafuna, hapo sijataja wapiga vyombo (musicians) na hili naongelea kwa uhakika
 
Miye japo sio Mkristo nafurahia copy za Ndombolo za JB Mpiana, Koffi Olomide, na Fally Ipupa zinazopigwa makanisani na mauno ya wanakwaya.
ni mambo yaliyoingizwa na wehu fulani humo wanakwaya wakayafuatisha
 
Mimi kama mpiga guitar mahiri na kijana wa kisasa niseme tu Wana Kwaya wa Jadi wakati wenu umepita ...tutawavumilia kama sehemu ya historia ya wapi kanisa limetoka ila kwa sasa Praise and Worship team ni uti wa Mgongo vinginevyo kanisani mtabakia wazee wenyewe...
Mtuache tufanye mambo kwa nyakati zetu.
 
Mimi kama mpiga guitar mahiri na kijana wa kisasa niseme tu Wana Kwaya wa Jadi wakati wenu umepita ...tutawavumilia kama sehemu ya historia ya wapi kanisa limetoka ila kwa sasa Praise and Worship team ni uti wa Mgongo vinginevyo kanisani mtabakia wazee wenyewe...
Mtuache tufanye mambo kwa nyakati zetu.
Muache kutafunana sasa,
 
Back
Top Bottom