Habari wanaJamiiForums,
Nimepata changamoto kwa mzazi wangu kwa kusumbuliwa na uvimbe katika koo na tulivyoenda hospitali ya taifa Muhimbili alifanyiwa kipimo kinachoitwa (OGD) ni kipimo hatara sana kama una moyo mdogo unaweza ukakimbia maana unasokomezwa limpira mdomoni hadi kwenye koo, baada ya kupata kipimo hicho cha OGD tulirudi nyumbani hadi majuzi tulipoenda tena hospitali kupata majibu ya vipimo na ndipo tulipoambiwa kuwa kuna tatizo la kansa kwenye koo.
Sasa basi, kitu nisichoelewa: je, kansa ya kwenye koo inatibika kwa njia ya upasuaji au kwa kupewa dawa au kwa mionzi? maana huku katika familia watu tuna hofu juu ya kutibika kwa kansa ya koo huku wengine wakisema kupona kansa ya koo ni mtihani.
Ushauri wenu jamani kuhusu ili tatizo la kansa ya koo kutibika au lah.
Sent from my iPhone using JamiiForums