Wazoefu wa mikoa ifuatayo....
Je, kati ya mikoa ifuatayo ni wapi kunamfaa kuishi mtu wa maisha ya chini na kati?
(A) DAR ES SALAAM
(B) ARUSHA
(C) MWANZA
(D) MOROGORO
(E) DODOMA
USIACHE KUTOA/KUELEZA NA SABABU.
Right Marker
Dar es salaam
MAISHA NAFUU YAKO
1. MOROGORO
Mashamba makubwa, chakula ni kingi ni njia kuu ya kuelekea Daresalaam
Ikumbukwe moro bado sio jiji ni mji mdogo kidogo kuliko ulioitaja hapo hali ya maisha bado iko chini kwenye kodi na hotel
Wageni sio wengi na hakuna taasisi nyingi za kiserikali kufanya mji kuwa na watumishi wengi hivyo bado maisha yako chini
2. MWANZA
Uwepo wa ziwa Victoria na kuzungukwa na mikoa mingine ya kanda ya ziwa ambayo ni wazalishaji wakubwa wa chakula
Lakini pia watu ni wengi hapa ndio jiji la pili kwa watu wengi nchini mfanyabiashara bado atapata faida akiuza kwa bei ya chini kwahio vitu ni bei rahisi
Kuhusu kodi na gharama za maisha ni chini kutokana na kutokuwepo na taasisi nyingi za kimataifa kama Arusha na Dar
Licha ya hivyo usijaribu kula sehemu za kishua kama waghill au malaika kama kipato chako ni cha chini utaumbuka
3. ARUSHA
Pamoja na kubarikiwa ardhi yenye rutuba ya mlima meru na mlima jirani kilimanjaro bado bei ya vyakula iko juu
Hii imechangiwa na kuwepo kwa taasisi nyingi za kimataifa, ukaribu na nchi jirani ya kenya ambao wana uhaba wa chakula kwa hiyo mara nyingi chakula kinapelekwa kenya ikifanya bei kuwa ghali
Bila kusahau utalii hivyo wageni wengi wanafanya demand inakua kubwa bei inapanda
Japo kama unajua machimbo na hautaishi maisha ya anasa, arusha ni moja ya mikoa rahisi sana ya kuishi tanzania
4. DAR ES SALAAM
Jiji kubwa la kibiashara lilishawah kuwa jiji ghali tanzania kabla ya Dodoma
Watu ni wengi na mashirika ni mengi, watu wenye hela ni wengi kuna sehemu utauziwa kinywaji hadi elfu 10 lakini sehemu nyingine utakipata kwa 500
Usafiri ni changamoto nyingine kubwa watu wengi hulazimika kupanga mbali ili kupata kodi rahisi
Lakini kama utajibana dar es salaam kuna sehemu maisha ni marahisi sana
5. Dodoma
Tofauti yake na Daresalaam ni kwamba huku utafutaji ni mgumu
Kama hujaajiriwa hapa maisha ni magumu
Vyakula vingi vinatoka mikoa mingine kunafanya bei kuwa juu
Serikali kuhamia kwa ghafla kumefanya kodi kupanda maradufu, gharama za viwanja havishkiki
Makahaba wengi wa dar es salaam sasa hivi wameamia dodoma wanasema dar hakuna hela 😄
Kwa maana nyepesi sasa hivi dodoma ni mji wa watu wenye pesa
6.ZANZIBAR
Hujaiandika hapo lakini ndio mji ghali tulionao
Ni kawaida kuuziwa parachichi 1500 hadi 3000 zanzibar
Guest ya 50000 haina hata choo ndani wakati kwa bara hiyo ni bei ya hoteli
Utalii ni mkubwa sana zanzibar umefanya bei kupanda
Lakini pia watu si wengi kwahio demand ni kubwa
*MBEYA
Pamoja na kwamba hujaiandika ni mji rahisi kuliko yote nliyoitaja hapo juu
Chakula ni rahisi kutokana na kulima kwa wingi mbeya yenyewe na mikoa jirani hata nchi jirani wakati mwingine mf sukari ya malawi 🇲🇼 n.k
Watu ni wengi na ni mji uliochangamka sana kwahio wafanyabiashara hawatapata hasara kuuza bei ya chini soko lipo
Umbali wake na dar unafanya kutokua na shughuli nyingi za wageni hivyo maisha ni ya chini
* Lindi na Mtwara
Hii mikoa ni ghali sana usijaribu
*Iringa na Moshi
Hii ndio miji bora Tanzania
Ni misafi imepangiliwa yote ni ya kitalii, ina hali ya hewa nzuri
Ila mzunguko ni mdogo hainaga watu
*Kahama, Geita + Katoro
Sehemu za kuziangalia sana
Miji inakua ajabu hiyo
*Kigoma, Tabora
Miundombinu ikikamilika huku + sgr hii mikoa naiona mbali sana
*Bukoba
Mji mzuri nnaoupenda + maisha marahisi
*Tanga
Jiji tulivu nnalolipenda na gharama zake ni nafuu
*Tunduma, Bariadi, Babati, Bunda, Makambako, mpanda, masasi, tunduru, korogwe, magu, karagwe, mafinga, chunya, kyela, ifakara, turiani, karatu, sengerema, njombe + Kasulu
Miji ya kuangaliwa sana hii
* Singida, songea na sumbawanga kwetu nlipozaliwa
Hii miji yote inaanziwa na 's' sijui inashida gani 😄
Miundombinu inayojegwa ikiisha ni miji mizuri sana kuishi
* Pwani
Pwani yote kama unahela wekeza sasa hivi nnua kiwanja utakuja kunshkuru badae
*Nmetoka nje ya mada kwa miji mingine kuleta uelewa zaidi 👏
Ps; Niliyeandika haya ni moja ya watanzania wachache nliobahatika kutembelea mikoa na wilaya zote Tanzania kwa ujumla wake