Mr Miller
JF-Expert Member
- Jan 24, 2017
- 11,449
- 25,768
Mleta mada umetumia neno “kukaimu” vibaya na neno hilo linaweza kupotosha mada nzima. Kukaimu ni kushikilia madaraka kwa muda. Rais SSH alikaimu siku toka JPM alipokufa mpaka siku anaapishwa! Baada ya kuapa alishika madaraka ya uRais.
Katiba ya Tanzania inatambua muhula kuwa miaka mitano na hairuhusu kuongoza kwa zaidi ya mihula miwili, bila kujali mhula mmoja kati ya hiyo miwili ni miaka mitano kamili au pungufu. Ndio maana inaeleza kitakachotokea kama Rais aliye madarakani atakufa na atarithiwa na makamu wake. SSH angekuwa na nafasi ya kuongoza zaidi ya miaka 10 kama Rais JPM angekuwa amekuwa madarakani kwa zaid ya robo tatu ya muhula (JPM alitufa takribani miezi 6 baada ya kuapishwa) na hivo kipindi kilichobaki kitahesabiwa kwa Rais SSH (ndio maana inaitwa Serikali ya awamu ya sita)!! Na awamu ya Rais haizidi mihula miwili.
Namna pekee ya SSH kuwa mgombea wa 2030-35 ni kufanya kama wengine walivofanya - kutumia Bunge kubadilisha matakwa ya Katiba.
Hii ni awamu ya sita na kama anataka kuwa mgombea 2030 aanze kusema hii bado ni awamu ya tano na kwamba bado anakaimu madaraka ya Rais (jambo gumu kusema kwa sababu hawezi kuwa anakaimu wakati yeye sio Makamu wa Rais kama Katiba inavyotaka).
umeiweka vizuri sana chief, shukrani