Je, Katiba yetu inamruhusu Rais Samia kukaa miaka 15 Ikulu?


umeiweka vizuri sana chief, shukrani
 
Ni kweli kabisa, hii Jf imejaa viazi vingi sana. Hasa viazi ufipa, aaaaaah vile viazi havifai kabisa.

Watu hawajui chochote zaidi ya matusi, wabishi wenye kujiona wako sawa kwa kila kitu.
Wao wanadhani hii inchi ni kama club tu😅.
Kifungu 40(4) "....Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu...."
 

kwahiyo akitaka kugombea kwa awamu nyingine ya tatu kwa katiba hii atakua anaharibu, okay.
 
Mbona hili li, efafanuluwa huko juu.
 
Inaonekana una akili nzito Sana.
Si umewekewa hadi vifungu hapo juu vibavyoeleza kuwa kama ataksimu kwa miaka mitatu na kuendelea badi hiyo itahesabiwa kama awamu yake ya kwanza
 
kwahiyo akitaka kugombea kwa awamu nyingine ya tatu kwa katiba hii atakua anaharibu, okay.
Mkuu miller, tuacheni hizi asumption mbofu mbofu za kwa Mama kutaka kugombea awamu tatu!, kwanza hata hiyo awamu ya pili, hajasema atagombea!, sasa hiyo ya awamu ya tatu unaitoa wapi?.

P
 
Mkuu Mwl.RCT , Ukweli mwingine ni mchungu kumeza ila ndio ukweli.
P
 
Mkuu miller, tuacheni hizi asumption mbofu mbofu za kwa Mama kutaka kugombea awamu tatu!, kwanza hata hiyo awamu ya pili, hajasema atagombea!, sasa hiyo ya awamu ya tatu unaitoa wapi?.

P

sawa ni asumption zetu chief, je ikitokea akitaka kugombea katiba itamruhusu au itamfunga?
 
sawa ni asumption zetu chief, je ikitokea akitaka kugombea katiba itamruhusu au itamfunga?
Hoja nyingine kiukweli zinatia hasira!. Katiba imesema mwisho ni awamu mbili. Mama ndio kwanza yuko awamu yake ya kwanza, bado hajasema kama atagombea awamu yake ya pili ya 2025-2030, sasa hili la awamu ya tatu linatokea wapi?!.

Katiba ndio imeweka ukomo wa awamu mbili, mtu unauliza " je ikitokea akitaka kugombea awamu ya tatu, jee katiba itamruhusu?", hili sasa ni swali gani?!. Katiba iko wazi mwisho awamu mbili, haiwezi kutokea mtu kutaka kugombea awamu ya tatu wakati mwisho ni awamu mbili!. Halafu watu wakiitwa viazi humu mnalalamika!.
P
 
Aliyekudanganya kuwa Katiba inafuatwa ni nani? Tangu awamu ya tano na hii ya sita Katiba imesiginwa na inaendelea kusiginwa,ukileta fyoko unamiminiwa risasi za kutosha. Hivi sasa ni undava undava tu Rais ndiye kila kitu, ukichanganya na yale mazuzu kule mjengoni ni mwendo wa kujiamulia tu akae madarakani hadi kifo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…