Naomba ufafanuzi hapa Mkuu Kiranga, unaamini hana tatizo la kukubali matokeo kwani anajua atashinda kihalali kwa nguvu zake kama Kikwete au kwa nguvu ya CCM ?
Naomba ufafanuzi mwingine Mkuu Kiranga unadai ana confidence atashinda kihalali (kiasi cha kuwatukana na kusema hahitaji kura zao) kama Mrisho Jakaya Kikwete au kama mgombea Uraisi kwa tiketi ya CCM ?
Majibu ya maswali haya mawili ni muhimu sana kabla sijaingia ndani zaidi kwa nini naamini Kikwete hana hakika kama atashinda na hana confidence kabisaa ya kushinda kihalali.
Of course Kikwete kashapitishwa na CCM na sasa hivi ndiye mgombea pekee wa CCM, kwa hiyo namuongelea Kikwete mgombea wa CCM. Kikwete si mgombea wa CHADEMA kwa hiyo huwezi kusema kwamba naongelea Kikwete mgombea wa CHADEMA. Tanzania hairuhusu ugombea binafsi, kwa hiyo huwezi kusema namuongelea Kikwete mtu binafsi.
Maswali yako yanaibua maswali ya kufikirika, vipi kama Kikwete angekataliwa na CCM, halafu CCM wakamuweka mgombea mwingine, Kikwete angekuwa na confidence aliyonayo sasa? Angekuwa na nafasi aliyonayo sasa? Of course asingekuwa navyo, kwani CCM ina party machinery na name recognition nchi nzima.
Wakati Benjamin William Mkapa anateuliwa kuwa rais wala hata hakuwa anajulikana. In fact hata katika kutangaza nia alikuwa ni mtu wa mwisho nafikiri. Na watu wengine walisema wanamjua zaidi Ken Mkapa (Mchezaji mpira wa Yanga) kuliko Benjamin Mkapa. Lakini kwa sababu alikuwa mgombea wa CCM alipita.
Vivyo hivyo Ally Hassan Mwinyi, mtu ambaye alishajiuzulu uwaziri kwa scandal la mauaji ya vibibi. Lakini CCM ikamshika mkono miezi michache tu baada ya kutangazwa kama "rais wa muda Zanzibar" baada ya kipindi cha "machafuko ya hali ya hewa ya kisiasa" huko Zanzibar yaliyomfanya Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi kujiuzulu, lakini watu wakaimba "Ally Mwinyi Ally Mwinyi, NDIYO, NDIYO, NDIYO, mwenye busara na hekima,NDIYO NDIYO NDIYO" watoto wa kihuni katika kubeza collectivism miaka ya baadaye (miaka ile hata Mzee Maharage aliogopa kumkataa) wakaja ku parody wimbo kwa kuongeza "aliku--ra migombani, NDIYO, NDIYO,NDIYO".
Kwa nini nasema haya yote ? Naonyesha umuhimu wa chama katika kampeni, chama kinaweza kumchukua mtu aliyekaa kama jiwe na kumfanya rais. Tanzania CCM ndiyo inachagua rais, si watanzania per se.
Lakini miaka hii ya karibuni, ambapo tunaona hata CCM inagawanyika katika makundi, mtu anaweza kusema hii automaton inaanza kwisha na kila mtu anaanza kujipalilia mwenyewe ndani ya chama na katika makundi haya.
Ndiyo ukauliza, huyu Kikwete ana confience yeye mwenyewe au kwa tiketi ya CCM ? Narudia, of course kwa tiketi ya CCM, kwani yeye hajaona kilichompata Mrema ?
Ila kwa sababu sasa hivi CCM hawana utamaduni wa kumkataa rais kumalizia muhula wa pili, na kwa sababu Kikwete tayari ndiye de facto / de jure mgombea wa CCM pekee (baada ya Shibuda kugwaya) as far as the campaign is concerned hakuna tofauti kati ya Jakaya Kikwete the person and the CCM candidate.
After all Tanzania hatuna utamaduni wa kufuatisha institutions kama vyama, bado tuna utamaduni wa kufuatisha strongmen.
Na Kikwete ndiye strongman wa CCM, kama si Tanzania.