Asante kwa maelezo yako ambayo kwa namna fulani yanapingana na dai lako la awali
Kitu cha kwanza kabisa nilichotaka kuweka wazi ni kwamba maelezo yangu hayapingani. Ndiyo maana nikaanza kusema kwamba Kikwete kashapitishwa na CCM, na Tanzania hairuhusu mgombea binafsi, kwa hiyo unless unaongelea hyperbolics za dunia ya kufikirika zilizo nje ya context ya uchaguzi wetu huu, mtu akimuongelea mgombea Kikwete anamuongelea Kikwete mgombea wa CCM na wala si wa CHADEMA, au mgombea binafsi Kikwete. Mimi siko interested na hypothetical hyperbolics za alternate universe na alternate futures, nikitaka kuburudishwa na hyperbolics hizi natafuta tungo za Arthuc C. Clarke, Isac Asimov, Carl Sagan, Herbert G. Wells au hata Douglass Adams katika tamthiliya zao za "Science Fiction". Kwenye ku deal na ukweli unaoendelea nadeal na ukweli.
?
Uzito wa dai la kushinda kihalali unapungua kwani unasisitiza jinsi ilivyo vigumu kuiondoa CCM madarakani kwa sababu wao ndio wanaamua nani awe Raisi wa nchi hii na siyo wananchi per se !
CCM washampitisha Kikwete, what's your point ? Mimi sikusema Kikwete ana ujanja uchawi wa kuwaroga Watanzania wampigie kura yeye bila kujali chama.Sielewi unapata wapi hisia kwamba ninavyomuongelea Kikwete namuongelea nje ya siasa za vyama. Tanzania hamna elective politics bila vyama, sasa sijui hii notion ya Kikwete anayeelea hewani bila ya kuwa na chama unaitoa wapi.
Hapa ni kama vile unakubaliana na mleta mada kuwa pamoja na wananchi kuamua tofauti,
Wananchi wetu hawana utamaduni wa kuamua tofauti, ni 1985 tu wametoka kuimbishwa "Ally Mwinyi, Ally Mwinyi, NDIYO NDIYO NDIYO". Mpaka leo Nyerere ni kama mungumtu pamoja na maovu yote aliyoyafanya (not that hakutenda mema). Mpaka leo badala ya watu kuangalia tutaleta uongozi bor, bado wanalila lia na "hero worship", wanamlilia Nyerere afufuke aje atuongoze, wasomi hao.Worse still hata upinzani wenyewe bado upo katika "hero worship" hiyo hiyo. Watu pekee mwenye uwezo wa kumsema Nyerere bila haya ni Mtikila na Wazanzibari fulani. Mpaka mara nyingine mtu unaona huyu Nyerere sasa anatumika kama mtaji wa kisiasa.Huyu Nyerere si ndiye yule yule alikuwa anakandya vyama vya upinzani huyu? Huyu Nyerere si ndiye aliyefanikisha wizi wa kura wa kumnyang'anya Seif Sharif urais wa Zanzibar huyu? Mbona wapinzani wanamuogopa hata baada ya kufa? Au ndiyo nidhamu ya woga isiyotaka kuwasema vibaya wafu, hata kama ni kina Iddi Amini ?
Kwa hiyo usijidanganye kwamba wananchi watafanya tofauti, kuna sehemu huko watu hawajui kwamba Nyerer amefariki si rais. Wengine washamsikia Nyerere miaka kibao wanafikiri kile cheo cha urais ndiyo Unyerere, ukiongea nao ukiwaambia Nyerere alifariki wanakuuliza Nyerere wetu sasa hivi nani ?
Wananchi kuamua tofauti, tofauti my foot, tofauti yenyewe iko wapi? Hivi vimikoa viwili vitatu urbanite ?
[UOTE]utamaduni wetu wa kufuatisha strongmen unaweza kumpa kiburi Kikwete (CCM) asikubali matokeo tofauti na akawa kama Mugabe. [/QUOTE]
No, you got it backwards. Ukiwa strongman Africa mara nyingine unakuwa so powerful kiasi hata huhitaji kuiba kura.Kwa sababu una control communication, una control education, una control largesse.Kila kazi muhimu inatokana na uteuzi wa rais.Kuanzia majaji (judiciary) mpaka wabunge wa kuteuliwa (legislature, in fact rais mwenyewe ni sehemu ya bunge) cabinet (executive) wakuu wa mashirika ya umma (technocrats, administrators, aristocrats) huyo huyo rais ndiye mwenyekiti wa chama (party politics) na amiri jeshi mkuu (armed forces) anateua gavana wa benki kuu na hata mabalozi (diplomatic corps). Anachagua mpaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (electoral process).Sasa unategemea mtu kama huyo atashindwa vipi kuwa na unfair influence kiasi cha kutohitaji kuiba kura ?
Hivyo kutoafiki na dai lako la awali liko pale kwamba je, kwa mtu (chama) kama huyo, hiyo confidence ya kushinda kihalali inatoka wapi kama si ukweli kuwa wananchi hata wafanye nini watalazimika kumchagua tu yeye kuwa Raisi ?
Inategemea na maana yako ya neno "halali" ni nini. Kama unamaanisha uhalali wa kutoiba kura (ambao ndio tuliokuwa tunauzungumzia hapa originally) then utaona kwamba Kikwete atashinda kihalali kwa sababu ana kila nguvu ya kufanya hivyo. Ni kama umpiganishe Tyson alipokuwa katika prime yake na kijana mchanga.
Lakini kama unasema kumpiganisha Tyson in his prime na kijana mchanga, asiye wa uzito wa Tyson wala uzoefu wake, ambaye sio professional boxer na wala hana access ya chakula na mazoezi ya Tyson, ukasema kuwapambanisha si halali, then utakuwa sawa.
Kama una object playing field haiko level, team ya Kikwete iko kilimani inasaidiwa na gravity na timu za upinzani ziko chini zina fight an uphill battle, then naweza kukubaliana na wewe, kwamba tumpunguzie rais madaraka yake ya kuteua kila mtu, tubadili katiba etc etc.Lakini hili si swali tulilokuwa tunahjadili hapa.
Tunaongelea mtu ambaye ameshindwa katika kura, na sasa anaamua kung'ang'ania Ikulu na kutaka kubadilisha matokeo.Ndiyo mimi nikasema Kikwete hawezi hata kufikia point ya kutaka kubadili matokeo, atatakaje kubadili matokeo wakati kiwanja chenyewe hakiko level na yeye yuko juu wakati wapinzani wako chini? Ni obvious ukitumia kiwanja hiki atashinda mechi.