Je, kinadharia inawezekana kila mtu duniani akawa tajiri?

Kutosha nini? Maana kinachokutosha wewe mwengine hakimtoshi

mAHITAJI YAKO YANAYO KUZUNGUKAA

NB:KWA RENKI YA KIDUNIA UKIWA NA TRILLIONI MBILI UNAWEZA UKAISHI MAISHA YAKO YOOOTE (HIGH STANDARD LIFE)BILA KUFANYA CHOCHOTE MPAKA UKAFA.HUO NDO UTAJIRI NAO UZUNGUMZIA MKUU
 

Hii ni ngumu kwasababu binadamu tunatofautiana namna ya kufikiri na hata kufanya mambo...

Kama hali ya kutafakari na kufikiri ingekuwa sawa hili lingewezekana lakini nadhani ingesumbua kwasababu tungekuwa na mambo yanayofanana,tusichokijua ni kuwa huu utofauti uliopo ndio unafanya maisha yawe matam kwa asili yake...
 
Mi nadhan wengine ni lazima wawe maskini ! Hata nikirefer Bibble Mathayo kuna sehemu alisema Heri wale masikini duniani maana mbinguni wataiona raha ya milele. Pia ukiangalia mfano wa Tajiri na Lazaro! so gepu la maskini na tajili halikwepeki.
 
Kama utajiri unao uzungumzia ni kuwa na mali nyingi, kwa hali ya kawaida haiwezekani watu wote kuwa matajiri. Sababu kila binadamu ameumbwa tofauti kuanzia kiakili hadi kiutendaji. Kuna wengine ni vichaa, walemavu, wavivu, waoga, n.k. Hata kama kinadharia ingekua hela zinaokotwa alfajiri ya saa 11.00, bado kuna wengine wangechelewa na hivyo wangekosa kuwa na pesa nyingi. Pia, kumbuka binadamu tunategemeana ili maisha yaende, hivyo kuna wengine hawataki kuwaona wenzao wamefanikiwa, wanavinyongo! Kwani definition ya utajiri ni ipi unayoizungumzia kwa muktadha huu?
 
Umasikini upi unazumgumzia❔➖WA roho au mwili❔
 

bro umetema madini tupuu,,yani ubinafsi ndo tatizo kubwa ila kila mtu hapa dunian anaweza kuwa tajiri,,ila karma nayo inachangia kuwepo kwa madaraja mana haya maisha ni cycling process
 

nakuelewa sana kaka,,i salute u
 
Utajiri unaouzungumzia ni kiasi gani?
Kuna waoona wakiwa na mil 100 ni matajiri na wengine wakiwa na bil 10 wanajiona middle class.
Utajiri unausemea ni upi? Kwa kiwango gani?
 
Madaraja katika jamii hayawezi kupotea kwa namna yeyote
Hivyo haiwezi kutokea dunia nzima wote tukawa matajiri, hata katika kufikilia tu!
Kinachoweza kutokea ni watu katika dunia kukua kimaendeleo katika ujumla wao.
 

At one point, everybody was rich.
 
Watu mnazunguka sana na kulikuza swali.
 
Watu mnazunguka sana na kulikuza swali.
Kumbe na wewe umeona mkuu...Mtoa mada ni hv,hilo haliwezekani na kama lingewezkana wewe usingeweza kuzama humu jf kwasbb mzungu asingehangaika akutengnezee simu/computer uliongilia jf wakt tayar ana mihela kibao..Hili swala la kila mtu awe tajiri hata mungu hakuthubutu litokee na hata serikali yoyte dunian haiwez kuthubutu kila raia wake awe bilionea...yan kuna madhara makubwa sn na huenda hata kula yako ingekuwa shida tupu na ungetembea uchi japo bilionea..nani akutngnezee nguo? Nani akulimie chakula...hujaelewa bado?
 
kwa uelewa wangu ni vigumu kwa kila mtu kua tajiri kwa kila kitu, ili kue na balance nzuri katika maisha ni lazima kuwe na pande mbili, yaani upande wa wasio na utajiri na upande wa wenye utajiri, ili huo utajiri uonekane ni wa maana ni lazima kuwepo na watu walioukosa, hivyo watalazimika kuutafuta kutoka kwa wale walionao, ili maisha yaendelee lazima kuwe na kutegemeana. mfano ni lazima kuwe na wabeba mizigo, wakulima, wanunuzi wa mazao ya wakulima n.k. kila kitu kikipatikana kwa wingi na kila mtu akiwa nacho, dhamani ya kitu hicho hushuka(paradox of value) ndio maana maji ni ya muhimu sana kuliko dhahabu lakini bado maji yanauzwa bei ya chini na dhahabu inauzwa bei kubwa kwa sababu inapatikana kwa shida. hivyo kama kila mtu angekua na fedha au kila kitu anachohitaji, maisha yangekua magumu, nani angefanya kazi ngumu? nani angekubali kuishi kijijini? nani angemuheshimu mwingine?
 
Umasikini ni state of mind.
Kuwa watu muda wote wanawaza kuuza walivyonavyo au kutumia hadi viishe
Wengine wanawaza kuzalisha na kuongeza vipato.

Utafiti usio rasmi unaonyesha, Leo kama utachukua pesa zote dunia nzima ukawagawia watu wote sawasawa.
Mwisho Wa siku zitarudi kwa walewale walikuwa nazo mwanzo.
 
Watu wote hawawezi kuwa tajiri lazma kuwe na balance .imagine kila mtu angekuw tajir nani angefny kaz kw mwenzie?!nani angekaa shamban alime?!mifano ipo mingi ila wote tungekuw matajir dunia isingeendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…