Je, kinadharia inawezekana kila mtu duniani akawa tajiri?

Je, kinadharia inawezekana kila mtu duniani akawa tajiri?

Mimi imani yangu kuhusu maswala ya kuwa tajiri yaani RIZKI HAINA UJANJA kuna watu wanapambana na maisha ila hawapati utajiri.me nimeona watu wamepata hadi mil 700 ila sshivi anakuomba mia5
 
Haiwezekani, kwa kuwa mtaji wa tajiri ni masikini. Masikini ndio mtaji wa tajiri, na masikini anapata riziki kutoka tajiri
 
Mimi imani yangu kuhusu maswala ya kuwa tajiri yaani RIZKI HAINA UJANJA kuna watu wanapambana na maisha ila hawapati utajiri.me nimeona watu wamepata hadi mil 700 ila sshivi anakuomba mia5
Mkuu hata uhai mbona ni hutajiri tosha?
 
Wanajamvi, Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyonipa ya uhai na afya tele kuweza kuleta swali hili kwenu.
Swali langu haliongelei kama inawezekana kila mtu akawa tajiri 'kiutendaji', la hasha. Bali je, logic inakubali kwa watu wote duniani kuwa matajiri bila kuacha masikini hata mmoja? au kwa wengine kuwa matajiri ni lazima kuwe na wahanga? (masikini)?
Nawasilisha.
"..Binadamu wotee tukiwa matajiri bado wale matajiri wa mwisho mwisho wataonekana masikini pia"
 
"..Binadamu wotee tukiwa matajiri bado wale matajiri wa mwisho mwisho wataonekana masikini pia"
Yeah.. Tajiri akizungukwa na masikini anaonekana sana.. Lakini tajiri huyu ukampeleka kwa Matajiri wengine ataonekana bado.. So utajiri utauelezea kulingana na muktadha..hata hivyo kama ilivyo hasi na chanya.. Ni vigumu wote kuwa matajiri.. Hiyo ni nature..
 
Sema sasa tukija in reality, capitalism, kitu pesa kila mtu anakomaa kuzivuta kwake kadri awezavyo, hata kama ni kubomoa nyumba za watu, kufunga watu, people don't care, kufanya watu wawe slaves etc, na ni moja ya vitu vinavyochangia vitu kama weapons manufacturing, sababu kama weapons zingekua hazilipi vya kutosha makampuni yasingejitokeza kutengeneza very advanced weapons, kwa style hii lazima baadhi ya watu waumie tu, haitotokea siku hata moja kuwe na balance sababu system nzima inaoperate kwa principle ya moja ata-gain profit moja ata-lose hamna swala la kusema nchi zote zitashirikiana kutengeneza kitu flani ku-end world hunger, coz kila mtu yuko busy kujaribu kuvuta pesa kwake hamna muda wa kufikiria kuhandle matatizo ya binadamu wengine.

Hiki ulichosema kuhusu capitalism siyo kweli. Sisi ambacho tunaona ni umaskini leo hauwezi hata kidogo kufananisha na maisha waliyokuwa wanaishi wafalme wa karne ya 15 (15th century). Yani hiyo capitalism unayo sema ndiyo inajali profit tu ndiyo iliyo kuletea umeme, dawa, ardhi, kazi, hela, internet, uhuru wa kuishi unavyo ishi saivi, nguo, elimu e.t.c. Fikra ya watu wengi wasio kuwa na mbinu au njia za kutengeneza mapato au (capital) ni kwamba capitalism inawapa fahida matajiri tu. Hilo siyo kweli. Capitalism ni kuhusu kufanya deal na kukubaliana. Kama unafikiri capitalism ni "moja ata-gain profit moja ata-lose" hapo umekosea kwasababu huo ni uwizi. Tatizo ni kwamba watu wanaangalia system ilivyo saivi alafu wanaiita capitalism. Hii current world system siyo capitalism bali ni authoritarian corpratism. Yani serikali za dunia zinawanyanyasa wananchi wao na kufanya njia ya kuanzisha biashara ziwe ngumu alafu wana ongeza kodi na kuuwa uhuru wa uchumi ili wawe wao na nguvu zaidi. Dunia ingekuwa inafanya biashara kwa sheria za pure capitalism ambayo serikali haijiusihi kila mtu angeweza kushindana. Mama ntilie angeweza kushindana na kfc na hata muuza mitumba kushindana na nakumart. Lakini serikali imeweka sheria kuzuiya watu kama mama ntilie na muuza mitumba kuingia kwenye registered market.

Siyo kweli kwamba capitalism kuna mtu ambaye hatapata faida kwenye kufanya dili kwasababu maana ya dili ni kwamba kila mtu anayehusika anahusika kwasababu anajua atapata faida hata kama yeye ndiyo anayetumia hela. Wewe mwenyewe ukiwa una nunua dukani haujalizimishwa na muuza duka kununua kitu chake lakini umechagua kukinunua kwasababu uliamini uta pata faida kwenye hicho kitu. Hii ndiyo capitalism.
 
Back
Top Bottom