Je, kipi kimefanyika kwa inspekta wa Polisi aliyeshinda tuzo ya fasihi Afrika?

Je, kipi kimefanyika kwa inspekta wa Polisi aliyeshinda tuzo ya fasihi Afrika?

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Kumekuwa na ukimya tangu Inspelta wa Jeshi la Polisi, Salim Hussein Ngazi aliposhinda Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika 2025/2026.

Hatujaona kwenye vyombo vya habari, polisi ikitangaza ushindi wake na kumpa tuzo, pongezi na hata cheo kama walivyofanyiwa akina Ibrahim Bacca na Alphonce Simbu, walipandishwa vyeo kwa vipaji vyao.

Inspekta huyu ameshinda Tuzo ya Fasihi ya Afrika kwa kushika nafasi ya kwanza upande wa Riwaya. Hii ni tuzo kubwa sana barani Afrika na hata duniani kwa ujumla.

Tulitegemea hata kumwona Inspekta Ng'anzi akitajwa tu Bungeni kwa kutambua mchango wake kwa taifa.

Riwaya aliyoshinda inakwenda kusomwa na jamii na kunufaika nayo huku vijana wakiwa kundi kubwa ambalo limeguswa na Riwaya hii ikitoa elimu kwao juu ya kuwa makini na makundi rika.

Je, Jeshi la Polisi Tanzania limemjulisha hata waziri wa vijana, Joel Nanauka kuhusu mchango huu alioufanya Inspekta huyu kwa taifa? Je, polisi wameijulisha Wizara ya Elimu kuhusu kumpa kipaumbele Inspekta huyu katika kazi yake aliyoifanya na hata kitabu chake kuingizwa kwenye mtaala wa elimu nchini?

Je, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Patrobas Katambi ana taarifa? Na kama ndiyo amefanya nini hadi sasa kwa askari wake huyu aliyeliheshimisha Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ujumla?

Je, wizara zote hizi za Vijana, Elimu na Habari, Sanaa na michezo zisingeweza kufanya jambo kwa Inspekta Salim mara baada ya polisi kuwashirikisha?

Tangu aliposhinda tuzo hiyo Julai 24, 2026 kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar hadi sasa kumekuwa na ukimya na hatujaona kilichofanyika dhidi yake.

Nafikiri muda bado upo na kwa wadau watakaoliona hili binafsi wanaweza kulifikisha kwa wahusika hasa Waziri wa Vijana, Waziri wa Elimu au Waziri wa Habari Sanaa na Michezo.

Kabla ya kushinda tuzo hii ya Fasihi, Inspekta huyu alishaandika vitabu kadhaa ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii na sasa kashinda tuzo. Je, hastahili japo kutajwa bungeni kama tunu ya taifa?

Screenshot_20261030_081014_Photos.jpg
 
Inspector tupe hata jina la kitabu na maudhui yake hata kidogo maana umeishia kusema "kazi mbali mbali"
 
Bacca sio Polisi na hatowahi kuwa
 
Back
Top Bottom