Na huo ndiyo ukweli hakuna anae weza kuupinga kielimu kwa hoja na kwa uadilifu.
Shukrani tuko pamoja.
Nilichofurahi, unajadili kwa hoja ( suala la usahihi wa hoja hilo tuliweke pembeni). Ni sawa na mimi leo hii nikitoa kauli kuhusu uislam au dhehebu lingine nisilolifaham vizuri.
Naomba niweke wazi, sitajikita kwenye mjadala wa uhalali wa kuachiwa au kutoachiwa kwa Viongozi wa uamsho na kesi ya Mbowe, la hasha.
Nilikunukuu kuhusu sifa za wakristo na ukaandika huo ndio ukweli, sikuona haja ya kukubishia au kupingana nawe bila kusikiliza hoja zako, kama hautojali, ingekua vema ukaelezea kidogo kuhusu uongo, kulalamika kuonewa na chuki ( sina uhakika kama nimekunukuu ipasavyo).
Ila nakuwekea hapa chini maandiko kutoka kitabu cha Yakobo.
Yakobo 5:7-9
7 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.
9 Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.