T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Taleban haijaigeuka Marekani. Taleban inafuata matakwa ya Marekani.Kwa Afghanistan nimetolea mfano wa Taliban kuigeuka USA kwa wao kuwa na mlengwa mkali wa kiitikadi ya kidini.
Vivyo hivyo huko Syria USA huwenda akageukwa pia.
Taleban ilikuwa inafuga magaidi, Marekani ikaivamia Afghanistan kuwaondoa Taleban ili wasiendelee kufuga magaidi. Ikiwa uko Afghanistan, US ikaunda military bases kadhaa pale Middle East. Ikapambana na kina al Qaeda ikaua kina Osama bin Laden na kupigana na kina Saddam Hussein.
Ikakaa miaka 20 Taleban wakiwa mafichonj. Ugaidi umeisha, Marekani haina purpose tena ya kukaa Afghanistan ikiwalea ikaondoka. Kwenye kuondoka US haikuielekeza Afghanistan iishije, bali ilisisitiza haitaki kufugwa gaidi wala kuharibu maslahi ya Marekani. Jambo ambalo Taleban wanalishikilia hadi leo.
Kuna siku Marekani ilifanya shambulizi la kuua magaidi ikaua kijana wa Waziri mmojawapo serikali ya Taliban, walitulia.
Russia inaondoka Tartus naval base na Hmeimin airbase. Pigia mstari hili.Bado haijafahamika kama Russia itaondoa Kambi yake Tartus na haijajulikana kama kiongozi atakayeingia atakua na mlengo gani.
Iran ina hasara. Kwa miaka zaidi ya 10 Iran imewekeza na kuikopesha serikali ya Assad zaidi ya dola bilioni 50. Zote zimeyeyuka kwa kuangushwa kwa utawala wa Assad. Iran haiwezi claim deni lake wala kurudisha investments zake wala kupata faida kidiplomasia na kiusalama kwenye axis of evil yake.Iran haina hasara yeyote kwasababu Ina uwezo wa kupifikisha silaha Lebanon pasi na kupitia ardhi ya Syria.
Houthi wanapokea silaha kwa njia ya maji na nyingi zinakuwa intercepted. Kufuatilia shipment ya majini ni rahisi kuliko ya ardhini. Kule Syria hata underground unaweza, hata kwa kutumia Kirikuu au canter unaweza. Sasa navigation ya kutoa shehena Iran hadi Yemen inatumia chombo kikubwa kidogo ambacho kitajulikana kirahisi.Ukumbuke Houthi wanapokea silaha kutoka Iran bila ya mtu wa Kati na Yemen iko mbali sana na Iran.
Pia Yemen haipakani na Israel. Syria inapakana na Israel na vilevile Lebanon ambayo nayo inapakana na Israel. Sasa Yemen wale Houthi mpaka warushe makombora yapite anga la nchi adui yao ndio yafike Israel.
Hiyo Iraq yenyewe haina hasara kwa Israel kama ilivyokuwa enzi za Saddam. Syria ikiwa kama Iraq basi ni vyema kwa Israel.Kwa Israel ni hasara kama Syria itageuka kuwa kama Iraq.
Na Syria wakilazimisha vita Israel kiurahisi kabisa unajiongezea mipaka inajimegea Quneitra. Wasijaribu huo mtego.
Iraq ya Saddam ilikuwa na jaribio la nyuklia, ilikuwa na Scud missiles, ilikuwa na fighter jets. Iraq ilikuwa na bajeti ya kununua silaha kali za kisasa. Iraq ya Saddam ilikuwa na uwezo wa kufanya mobilization hata ya wanajeshi zaidi ya 300,000 kupigana na Israel au basi Saddam mwenyewe alikuwa na uwezo wa kutoa billions of dollars kwa wanamgambo wapigane na Israel.Ufahamu kuwa ndani ya Iraq kuna makundi ambayo yameshiriki kuisaidia Hamas mkuu.
Na ndani ya Iraq USA imeshashambuliwa mara kadhaa na washika silaha.
Yote hii ni kuwa tangu utawala wa Saddam uanguke basi Iraq ikawa pro-Iran.
Ngojea tuone huyo kiongozi atayekuja atakuaje.
Hilo ndilo la kutizamwa.
Sasa hawa njaa kali wenye viroketi vichache na wapiganaji elfu kadhaa wanakuwaje tishio kwa Israel kuliko Iraq ya Saddam?