Je, kuchora tatoo ni dhambi au si dhambi kwa Wakristo?

Je, kuchora tatoo ni dhambi au si dhambi kwa Wakristo?

Siyo dhambi... Tatoo haichafui roho yako kama hujaambatanisha na mambo ya kichawi.

Hivyo kama roho yako ipo salama basi kuchora tatu si dhambi
 
Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi. 27 Nywele zenu msizikate pembeni wala kunyoa ndevu zenu. 28Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.( walawi 19.27)
 
Kila dini tatoo inakatazwa
Tatoo inaleta shida Gani haswa?
Sipendi kuchora tatoo lakini sidhani kama inamletea mchoraji dhambi yoyote labda kama hiyo tatoo anaichora ikihusiana na matendo maovu.

Yaani mtu achore picha yake au msalaba au ya mwenza wake halafu awe kafanya dhambi? Sasa dhambi hapo ni nini yaani kabisa.

Nadhani wahafidhina wa dini Huwa hawapendi vitu vipya vinavyotokea na mwanzo Huwa wanavipinga sana ila vikizoeleka inaonekana kawaida.

Hata wanawake walipoanza kuvaa suruali Ilikua changamoto ikionekana hadi ni dhambi lakini ilipozoeleka imekua ni jambo la kawaida kabisa.

Tuna amri moja tu upendo, jambo lisilo na madhara kwako na mwingine kuitwa dhambi ni ulimbukeni.

Mambo mengine sio ya kiimani wala dini ni utamaduni wa mahali.

Kwa mfano mwanamke akivaa sketi fupi akaingia kanisani kijijini Mpitimbi itaonekana ni shida haswaa, lakini mwanamke huyohuyo akivaa hivyohivyo akaingia kanisani kuu la Mtakatifu Paulo London haitakua shida hakuna atakae jali kwasababu ya utamaduni wa mahali.
 
Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi. 27 Nywele zenu msizikate pembeni wala kunyoa ndevu zenu. 28Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.( walawi 19.27)
Kama unatafsiri bibilia kirnyeji hivi, basi utaishi kwa mateso sana.
 
Twende na nabii mkuu yeye kanukuu. AMPC Bible. Isaya 44.5


Karibu tujadili.

Sijui kwa nini umeweka hiyo Isaya 44:5 ila nachojua Biblia inakataza kabisa kuchanja alama za chale au kuchora mwili

Walawi 19:28
Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
 
Usikiongelee kitu ambacho hukijui ukakitolea hukumu, utakuja beba dhambi za watu wote unaowapotosha
Elezea upande wako wewe inakuwa je dhambi?

Anza na dhambi ni nini? Kisha utajua kuwa tatoo ni dhambi au siyo dhambi
 
Nimeshtuka! Ukichora tattoo tayari ni mfuasi wa shetani? Au ndio hao freemason? Ngoja nizidi kudodosa kama kweli ni michoro ya "kishetani".
 
Back
Top Bottom